Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

mmeba maono, ulikuwa na lako. Naona jamaa wamekemea maono yako yakashindwa.

Hoja unayo kaka, ila si kwa ze commedy. Wanaoaibisha utamaduni wetu ni mashoga kikwelikweli.

Pengine post yako ingekuwa na heading hii JAMANI MASHOGA WANAAIBISHA TAIFA LETU. Kisha ungetoa mifwano michache ya existance ya ushoga TZ.

Try next time!!!!
 
Watanzania tu wanafiki! Tangu tumjue Yesu na Mtume Muhammad, tumekuwa "wasafi" kupita kiasi kwa kujitangaza usafi huku matendo yetu ni tofauti kabisa.

Kule Kanyigo wana Katerero, jando unafundishwa na kufundwa utaalam wa ngono, wazee wetu hawaishi kupigana vijembe na matusi mepesi mepesi na hata makubwa kwa kutumia fasihi.

Tunaona mashoga kama ni wakoma, wasiofaa, je wao si Binadamu?

Mwazungumzia eti ujumbe gani wanauleta? Sanaa ni fasihi, hata hao Wazungu na Waarabu wenu waliowaletea hizo dini mpya ni wanafiki kwa kudai mambo fulani yasifanywe au kutamkwa hadharani.

Kutia chumvi nitasema hivi, aliyeleta mada, nia yake si kuchukizwa na ushoga, bali katumwa na wale vigogo mafisadi ambao wanataniwa!
 

Hahahahahaaaaaa, inaonekana jamaa katoka Tandaimba leo...!! Hahahahahahaaaa...!!!

Hivi mheshimiwa ushawahi kuona vichekesho vya kina "Martin" wa Marekani..?? Hw do they do, jamaa huwa anapiga gauni kwa kwenda mbele and watu wanamfagilia kinyama. Au umeshawahi kucheki movie ya Big Mama..?? Is that a real woman or fake woman (i.e. mwanaume aliyejifanya mwanamke). Sometimes hivi vitu vinafanyika ili kuchekesha watu.

Sema kwa swala la maadili, labda uwaambie wasi-misuse nafasi yao ya kuigiza in the sense kwamba, wasianze kutumia maneno machafu ambayo kwa mara nyingi yamepelekea kuharibu hasa watoto. Kama ni mfuatiliaji wa ze comedy utakuwa umenielewa.

Apart from such acts ambazo zinaharibu watu, mi nafikiri kujifanya msichana ni part ya uchekeshaji. Unless waanze ku-misuse hiyo position ya usichana kwa kuudhalilisha usichana (i.e. kufanya mambo ambayo in real situation hayafanyiki na wasichana ambao ni descent).

Otherwise, jamaa wanaleta burrrrrrrruuuuuuudani..!!

Au mwasemaje wana JF...!!
 

Hayo maono yako hatuyaoni. Watu wanatafuta hela wewe unapiga kelele. Kwani lazima kuangalia? Kwanza inaonekana ni mpenzi mzuri sana wa hiyo show
 

Wewe ndio unakera kwani hujui ufanyacho... Angalia AGAPE channel yaishe
 
Je mtu asiye na mikono unaweza kumpa mkono wa pongezi?
Je mkulima anaweza kuwa mkulima kama halimi?
Je mchekeshaji aweza kuwa mchekeshaji kama hachekeshi?
 
ni kweli ni burudani ila kuna maneo kama kwenye comedi zote duniani, huwezi kuangalia na mkweo
 
Nafikiri hakuna watu wanaolitia aibu taifa kama akina nkapa, richmonduli, vijisenti na genge lao. Hawa wanafanya watanzania wote tunaonekana mafisadi na hamnazo. Ndio, kama zingekuwemo si tungewashughulikia?!
 
Mbeba maoni inaelekea home wewe dictator kichizi u need to go to immalaseko and buy 1kg of "Comic Relief", 2 bags of "Exposure" and 3 Cartons of "Anti-Homophobia"..... BTW they are not men actin' gay they are men impersonating women 4 the sake of comic relief... It seems to me ur biggest problem is that of homophobia although i sense u lack sense of humour as well..... or maybe u r not comfortable about ur sexuality as they are....
 

Tutajie kabila lako tutafute neno comedy uwelewe maana ya comedy naona kwa kiswahili na kimombo haviikuingie
 
Mbeba Maono ana ya kwake.
Lakini pamoja na hivyo ni makosa kuunganisha na masuala ya EATV hapa si kuitendea haki channel hiyo. Maana kila mtu ana haki ya kusema analoona.
Ze comedy kazi yao nzuri na mahali wanakosea ni kawaida tu maana wanatumia vipaji na hakuna shule hapo.
Twawashauri wafanye kama wenzao wa Kenya. Waende shule ili wafanye vizuri zaidi.
Mbeba maono kwa hapa huwezi kushauri kitu na hoja yako imekataliwa.
 
Kuna comedian wengi sana nje ya Tanzania wanaoact kinyume cha maumbile yao. Cha msingi ni lengo la kuburisha lifikiwe. Kama wewe ndugu maono unakaa zaidi ya saa nzima kuangalia Ze Comedy wakifanya vimbwanga vyao, basi bila shaka unavutiwa nao, na kwa maana hiyo lengo la msanii limetia. Swali jepesi, unajisikia vipi pale msanii wa kike anapoigiza kama mwanaume, tena dume la mbegu??!!
 
mwaka mzima umeagalia ze comedy leo unajidai maadili ???!
mhh una lako jambo weye!
au ni sizitaki mbichi hizi?
 
Sasa hivi namsikiliza Remmy kwenye KLH News akinung'unika kama mwanamke kuwa akijipodoa wanasema anaringa, na jirani yake anataka kumtongoza n.k n.k na ya kuwa anampakazia ana Ukimwi wakati hana. Nikikumbuka nyimbo nyingi kuna watu walioimba wakitumia sauti ya kike (kama wanawake).. na wao hawakuwa wachekeshaji, sasa tuwachukuliaje hao wote.
 
Nachelea ya kwamba wewe bwana una uvivu wa kurikiri sababu the name itself goes without saying .Duh ngumu kukuelimisha mpaka inaboa yaani watu wengine inaonekani wanachojua ni kuandika na kusoma....................kuna mawili ni ama wewe hamnazo ama umetumwa kuwapaka hawa jamaa matope ,,,,na nani unajua ww!
 


Mbeba maono tena ushindwe na ulegee na maono yako haya uliyobeba sijui kutoka wapi na kuyaleta hapa.

Wewe una lako jambo sio siri.
 

Pia kuna huu wimbo "Tulizaliwa wote kijiji kimoja, lakini ulishindwa kunioa kwa sababu, ulisema sina tabia nzuri ee!!!. Sasa nimeolewa kaka unaanza kuleta maneno na chokochoko..................!!!!!"
Muimbaji wa wimbo huu ni mwanaume, tunakushangaa kwamba wanaume walishaanza siku nyingi ku-act kama wanawake.
Kuhusu Ze Comedy kwanza nikwambie kwamba sisi Watanzania tumechoshwa na mambo ya siasa, baada ya kudanganywa sana kwa wiki nzima na hawa wanasiasa, tunajiliwaza na vijana wa Ze Comedy. Mwenye kuona kachoka ama hawapendi kuna chanel kama chanel ten, ITV ama ukiona umekereka hata kuona TV yako hapo nyumbani basi fungulia radio kama Wapo Radio, Radio One, TBC, Radio Tumaini nk.
Ze Comedy wanapendwa si Tanzania tu bali East Africa kwa ujumla, ukiona wewe tu huwapendi, basi ujue unakajikasoro katika socio-mingling.
 
Yaani Mbeba Maono, umekaa katika computer yako na kudhani unatoa maono, kwa JF na jamii kwa ujumla kwa kuzungumzia suala kuwakandia Ze Comedy, wewe sasa ndiyo stage kwa leo. Kam walivyosema wenzangu huko nyuma kwamba inaonyesha wewe ni MBABE SANA. Na ninadhani hata jina lako ulikosea kuandika ulidhamiria kuandika MBABE WA MAONO. Mbele yako pale sebuleni watoto wako hawaongei kwa sauti bali kwa kunong'ona unadhani ni kwanini? Ubabe wako. Sasa nakuamuru, "Ondoka Ubabe wako Umekuponza....."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…