Ndugu zangu watanzania,
Leo nimeona niwaletee makatibu wakuu wa CCM tangia kuasisiwa kwa CCM Mwaka 1977. Nitaweka uchambuzi wangu binafsi kidogo kuwaonyesha waliohudumu kwa muda mrefu na wale waliohudumu kwa muda mfupi sana na sababu zake .orodha ni kama ifuatavyo.
1977-1981=Pius Msekwa .huyu ndiye
katibu mkuu wa kwanza
Tangia CCM
ilipoasisiwa
baada ya kuunganisha
chama cha TANU na
ASP (5-2_1977)
1981-1982= Ndugu Balozi Daudi
Mwakawago.
1982-1990=Ndugu Rashidi Kawawa.
1990-1995= Ndugu Horrace
Kolimba.
1995-1997= Ndugu Laurence Gama.
1997-2007= Ndugu Philip Mangula.
2007-2011= Ndugu Yusuphu
Makamba.
2011-2012= Ndugu Dr Willson
Mukama.
2012-2018=Ndugu Abrahamani
Kinana.
2018-2021=Ndugu Dr Bashiru Ally
2021-2023=Ndugu Daniel Chongolo.
2024 Ni Ndugu Dr Emmanuel Nchimbi.
Sasa ndugu zangu ukiangalia katika orodha hiyo na miaka yake utagundua ya kuwa mzee Philipo Mangula ndiye katibu mkuu aliyedumu na kuhudumu kwa muda mrefu katika nafasi hiyo tokea kuasisiwa kwa CCM .Ambapo Alikaa kwa takribani miaka kumi .katika kufanya uchambuzi wangu na tathmini yangu binafsi nimegundua kuwa kwanza alihudumu kipindi cha Hayati Mzee Benjamini Mkapa,Ambapo nikabaini ya kuwa ni kiongozi ambaye katika nafasi nyeti na kubwa serikalini na chamani alikuwa hapendi kubadilisha badilisha watu.yaani ilikuwa kama kakuamini na kukupitisha basi alitamani na kuwa na dhamira ya kufanya kazi na wewe mpaka mwisho wa uongozi au utawala wake wa miaka kumi unapokoma kikatiba.
Hii nimefanya na kufika hitimisho hilo baada ya kuangalia pia katika nafasi ya waziri mkuu wake ambapo alifanya kazi na waziri mkuu mmoja tu kwa miaka yake yote kumi uongozini .ambapo alifanya kazi na mheshimiwa Frederick Sumaye anayeshikilia rekodi hiyo mpaka sasa ya kukaa miaka mingi kama waziri mkuu.
Pili ni katika nafasi ya waziri wa mambo ya nje ambapo pia katika miaka yake yote kumi ya Urais wake alifanya kazi na Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete ,ambaye pia ndiye mpaka sasa anayeshikilia rekodi ya kuwa waziri wa mambo ya nje aliyehudumu kwa muda mrefu sana wa miaka kumi.ambapo mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kufikia rekodi yake hata kwa nusu tu ya miaka yake.
Kwa hiyo nikagundua kuwa Hayati Mzee Benjamini Mkapa ni kiongozi ambaye alikuwa akikuamini anakuamini kwelikweli na akifikia uamuzi wa kukupa nafasi basi anakuwa anamatarajio makubwa kutoka kwako ya kusaidiana nawewe mpaka mwisho. Na kwa upande mwingine utaratibu huu ni mzuri kwa kuwa unawapa utulivu wa kazi wasaidizi wako yakufanya kazi kwa kujiamini na pasipo mawazo au hofu ya kuondolewa wakati wowote ule .tofauti na ile kila mtu akilala usiku kucha anawaza kama kesho kutakucha akiwa katika kiti chake au nafasi yake ya uongozi ,yaani anakuwa anafanya kazi kwa presha na kutokujiamini kabisa na wakati mwingine inaweza ikamfanya aamue ajipendekezage tu na kukuabudu tu muda wote kama Mungu ili kujihakikishia uwepo wake katika uongozi uliomteua.
Lakini athari yake kwa upande mwingine ni kuwa mtu akijuwa wewe hunaga tabia ya kubadilisha badilisha au maamuzi magumu ya kumtoa mtu mahali bila kuangalia sura inaweza kupelekea watu kufanya kazi kwa mazoea bila hofu wala uoga wala ubunifu wala kujituma.yaani mtu anakuwa anafanya kazi anavyotaka yeye .anakuwa anadumu katika eneo moja kwa kujitengenezea na kujichimbia mizizi chini ili asitoke na hata akitoka basi aache watu wa kumlinda yeye na maslahi yake na Madudu yake yote aliyoyafanya akiwa katika nafasi husika.
Lakini pia inaweza kupelekea kuwadhoofisha kiuongozi wale wanaoonekana kufanya kazi kwa bidii na kuja na ubunifu mpya utaakaoonekana kufunika utendaji wa yule aliyedumu kwa mda mrefu . hivyo ili kutokuhatarisha nafasi yake inaweza anza kupigwa fitina na Majungu ya kumuondoa yule anayeonekana ni wakuja au mgeni ikiwepo kulazimisha ahamishwe na fitina zingine kibao hadi michezo ya nyuma ya pazia ya kiafrika.
Kwa hiyo yote kwa yote ni lazima uwe kiongozi ambaye wasaidizi wako na watendaji wako wote wafahamu ya kuwa kitakachokubakisha na kukuhakikishia kudumu katika uongozi ni uchapa kazi wako na ubunifu wako unaoleta matokeo chanya,kufanya kazi kwa bidii,kujituma kwa hali ya juu na kutokusubili au kuwa mtu wa kufanya kazi kwa kusukumwa sukumwa tu.
Ni lazima wasaidizi wako na watendaji wote wa serikali wafahamu kuwa ukiharibu kazi unaweza kuondolewa muda na wakati wowote ule hata ndani ya mwezi mmoja tu bila kuangalia sura yako wala ukubwa wa jina lako wala la wazazi wako.ni lazima kila mtu afanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu,katiba na miongozo mbalimbali.
Wakati mwingine nitakuja kuwachambulia wale waliodumu kwa muda mfupi na sababu zake kwa maoni yangu hasa kwa mzee Dr Willson Mukama.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.