Orodha: Serikali yawaita kazini walimu 13,130 na kada za afya. Watakaoshindwa kuripoti ndani ya siku 14 watapoteza nafasi

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewaita kazini walimu 13,130 kwa ajili ya kufundisha wanafunzi katika ngazi ya shule za msingi na sekondari.

Orodha ya Waombaji ajira iliyochapishwa leo Juni 5, 2023 katika kurasa 515 imehusisha walimu ambao pia wamesoma na kuhitimu elimu maalum.

Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki amesema Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao na nafasi hizo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Mwezi Aprili, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.
Hatimaye vizinga vitapungua , wamesota sana kitaa
 
Vijana kachapeni kazi mkisha dhibitishwa kopeni wekezeni achaneni na akina mpwayungu Hana lolote kima TU tena mkuu wa ombaomba Tanzania
 
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewaita kazini walimu 13,130 kwa ajili ya kufundisha wanafunzi katika ngazi ya shule za msingi na sekondari.

Orodha ya Waombaji ajira iliyochapishwa leo Juni 5, 2023 katika kurasa 515 imehusisha walimu ambao pia wamesoma na kuhitimu elimu maalum.

Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki amesema Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao na nafasi hizo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Mwezi Aprili, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.
Majina ya Doto yote yamefanikiwa kupata ajira 😳
 
Dogo wangu analia....anasema bora angesoma diploma ya utabibu...kwani degree yake haimsaidii....Mwaka wa 3 huu anaapply na kushindwa kuchaguliwa....nimemuambia dogo aje tufanye kazi kilingeni kwangu hapa awe anipondea dawa zangu za mitishamba...hwenda mwakani akapata inshaalah....

Msikate tamaa ndugu....maisha ni safari ndefu[emoji120]
 
Back
Top Bottom