Tetesi: Orodha ya Maafisa wa ngazi za juu wa Urusi waliouawa, kujeruhiwa na kutekwa na Jeshi la Ukraine

Tetesi: Orodha ya Maafisa wa ngazi za juu wa Urusi waliouawa, kujeruhiwa na kutekwa na Jeshi la Ukraine

Sasa wewe unaushauidi gani kuwa hao waliotajwa Ni kweli wameuawa?
Sasa kama mpaka huyu Mwamba "Chief of staff" mkuu wa majeshi wa Urusi,anajeruhiwa kwenye battlefield,kwanini usiamini kilichoandikwa?
Screenshot_20220504-075533.png
 
Ushahidi si umewekwa hapo majina vyeo na idara zao?

Wewe kanusha kwa ushahidi kwamba fulani wa idara fulani yupo hai.
Hiyo ni orodha ya majina na haina ugumu wowote kuipata ama kuitengeneza na Wala huitaji kuwa na idara ya ujasusi yenye weledi mkubwa

Hoja Ni ushahidi kuwa watu hao Ni kweli wamekufa
 
Sasa wewe unaushauidi gani kuwa hao waliotajwa Ni kweli wameuawa?
... Russia yenye watu wao waliotajwa kwa majina na vyeo hawajapinga anatokea mbogo asiyejua hili wala anaanza kupinga.

Mleta mada hajajitungia; kayatoa kwenye vyanzo vya kuaminika na yako public. Hoja hapa wewe unayepinga tupe chanzo chochote kile kinachopinga taarifa hiyo. Very simple.
 
UKRAINE wametoa list yenye majina,vyeo na vitengo vyao katika Jeshi la Urusi.Ni jukumu la Russia and proPutin kuelezea kwamba hiyo list ni ya uongo Kwa sababu Moja,mbili,tatu...wakiwa na DATA na sio kubisha tu kama uko kwenye vijiwe vya kahawa,ubishi wa Simba na Yanga🤔
... umefunga mjadala Chief. Jamaa wanachojua kwa sasa ni neno moja PROPAGANDA. Wamemaliza.
 
Comedian zelensky anatoa dozi huku analia.
Anajifanya kama amezidiwa hivi huku behind the scene anatoa kipigo cha kufa mtu.
... dogo anatoa dozi ya maana haswa. Wakati mwehu Putin anaua raia na chekechea wasio na hatia; Zelensky anapasua wenye combat na nembo tu; wengine wote wako salama.
 
Chini Russia imepoteza wanajeshi wengi kuliko Ukraine ila wameua raia wengi Kwa kurusha makombora Yao kwenye maeneo ya raia.Majina yamewekwa na vyeo vyao paomoja na vitengo walivyokuwepo.Sasa uongo utoke wapi?
Labda tuangalie data zinasemaje kuhusu nani wamepoteza wanajeshi wengi, hizo data ni mpaka jana may 3 ni za pande zote mbili, Russia na Ukraine fanya comparison utaona nani anapoteza wanajeshi sana.

Suala la Russia kurusha makombora kwenye maeneo ya kiraia unaijua sababu? Kosa lilianzia kwa zelensky kuwapa raia silaha, sheria za kivita ni kwamba unatakiwa ushambulie pale ambapo unashambuliwa.

Sasa raia kapewa silaha amejificha kwenye apartment yake anashambulia msafara wa Russian army then Russian army wakirudisha majibu Ukraine wanaanza kusema wanashambuliwa kwenye maeneo ya raia.

Hao watu wa haki za binadamu, EU na UN huwezi ona wakilipigia kelele hilo la kushambuliwa maeneo ya kiraia kwa sababu wanajua ni kwa nini Russia anashambulia maeneo hayo na wanajua sheria za kivita zinasemaje yaninwatabaki wanaongea ongea tu ila ukweli wanaujua.

Hilo suala limeshajadiliwa sana humu sijajua ni kwamba hamtaki kulielewa au kwenda na upepo wa kutafuta huruma ya jamii kwamba Russia inarusha kombora kwenye makazi ya raia.
IMG_20220504_081747_681.jpg
IMG_20220504_081749_920.jpg
 
Itakuwa ni mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia kwa nchi moja kupoteza viongozi wakuu waandamizi wa jeshi wengi kiasi kikubwa namna hii, ni pigo kubwa sana kwa Russia.
 
Hiyo ni orodha ya majina na haina ugumu wowote kuipata ama kuitengeneza na Wala huitaji kuwa na idara ya ujasusi yenye weledi mkubwa

Hoja Ni ushahidi kuwa watu hao Ni kweli wamekufa
Kweli ww ni Thomaso, dah! Unataka mpaka uletewe maiti zao au uoneshwe.
Kwa mantiki hiyo basi ww huamini kwamba kuna vita kwa sababu hujaenda huko Ukraine kushuhudia.
 
Mkuu kuna propaganda nyingi sana kwemye hii vita ikiongozwa na western media mfano ona hii
 
Back
Top Bottom