Orodha ya magonjwa ambayo ukiyapata hayatibiki kwa hapa Tanzania

Uko sahihi kabisa, pia kua na njia nzuri ya kukabiliana na msongo wa mawazo.

Unapona kabisa
 
Hilo ni somo refu. Kiufupi tu RA ni kifupisho cha Rheumatoid Arthritis au kwa Kiswahili unaitwa Baridi Yabisi.


Ugonjwa huu hutokana na kinga ya mwili kuanza kushambulia joints( viungio) za mwili. Hii hutokana na mabadiliko mbalimbali ndani ya mwili na wengine huwa ni ugonjwa wa kurithi unaotembea ndani ya familia.

Hii hupelekea kuvimba, kuuma na kushindwa kufanya kazi kwa viungio( joints) mbalimbali vya miguu na mikono
 
Tatizo kubwa kwetu ni kwamba tiba huanza baada ya ugonjwa kuwa umeshakomaa sana. Bado uwezo wetu wa kutambua magonjwa na kuyatibu yangali hayajakomaa hauridhishi. Halafu tatizo jingine nadhani vipimo vyetu vingi havijitoshelezi. Yaani dakatari anaweza kukupa dawa ya ugonjwa fulani kutokana na kipimo kimoja bila kuangalia kama kipimo hicho kinakubaliana na vipimo vingine; kwa hiyo tiba inakuwa ya trial and error.
 
Well said kaka
 
Mkuu Jaundice inatibika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…