Orodha ya majiji, miji na wilaya zenye mzunguko mkubwa wa hela Tanzania

Mbeya tunahitaji Mabadiliko ya DED,Mbeya sio ya kuzidiwa na Tanga..

Huu ni mwaka wa 3 mfululizo Jiji la Mbeya lime stack kwenye 15bln..

Je hakuna uwekezaji mpya? Hakuna biashara mpya? Watu hawaongeseki?

Huu ni uzembe wa Hali ya Juu.
[emoji16][emoji16][emoji28]...mbeya ,,level za wilaya ya kahama
 
Mapato ya halmashauri ni parking, guest house, stendi na cross border.
Sasa hizo zinawagusaje wananchi?
Ushuru wa mazo,leseni za biashara,mapato ya stand,service levies,vibali vya ujenzi,ushuru wa machimbo ya bidhaa za ujenzi nk..

Sasa Hizi sio shughuli za Moja kwa Moja za Wananchi? Hata hivyo hata TRA wanachukua pesa kwenye vyanzo hivyo hivyo,mfano kwenye Duka leseni inaenda Halmashauri ila Kodi ya mapato TRA.

Kwa mwaka 2021/22 Parking haukuwepo ilikuwa kwa TARURA na pesa ilienda Makao Makuu..

Mwaka huu wa 2022/23 ndio Parking zimerudishwa na hivyo zitakusanywa na Halmashauri so mwakani figures zitaongezeka..

Zamani hadi Kodi za majengo zilikuwa za Halmashauri serikali ilizipoka sasa sina Hakika kama mwaka huu zimerudishwa.
 
Wewe unaona biashara mpya Mbeya?
Ukiona sehemu hakuna ujenzi wa miundo mbinu ya biashara, ujue hali siyo.
Hata nyumba za kuishi tu ujenzi umestacka au upo kidogo sana.
Sasa ndio unaongea nini Mkuu,kwa hiyo hakuna baishara mpya,hakuna Ujenzi mpya,hakuna kupima viwanja nk?

Hizi sasa ni Chuki binafsi.
 
Unganisha mapato ya msalala,ushetu na kahama Mc ndo useme hayo maneno ..maana hizi halmashauri ziko wilaya moja
Sasa tukiunganisha tuite mapato ya Wilaya au?

Ikiwa hivyo tunaanza upya kupanga jedwali na hapo Wilaya za Mufindi,Njombe zitakuwa Juu zaidi maana maana Njombe ina Halmashauri 4 za NjombeTC ,Makambako TC,Njombe DC na Wanging'ombe..
 
Halmashauri za Wilaya ya Mbeya ndizo zinazofanya vizuri na kote kuna some specific reason kama ifuatavyo:
1. Chunya - Uchimbaji wa dhahabu
2. Kyela- Cross border( fees(ada ya getini) pale mpakani na Malawi(Kasumulu).
3. Mbarali-Kilimo cha Mpunga na ada ya stendi pale Igawa.
4. Rungwe na Busokelo hazifanyi vizuri sana kwa sababu ya kukosa hizo specific aspects. Wao wanapambana na vyanzo traditional ambazo halmashauri nyingi hupambana nazo.
 
Aisee nimeshangaa ,Dodoma inawezaje ipiku Mwanza, ??? Basi viongozi wa Mwanza ni wapigaji,au maana vyanzo vya mapato Dodoma ni vipi? bila kujali Serikali ipo pale,
Mwanza ikipata viongozi wabunifu, inatakiwa kuanza kimbizana na Dar,
 
Aisee nimeshangaa ,Dodoma inawezaje ipiku Mwanza, ??? Basi viongozi wa Mwanza ni wapigaji,au maana vyanzo vya mapato Dodoma ni vipi? bila kujali Serikali ipo pale,
Mwanza ikipata viongozi wabunifu, inatakiwa kuanza kimbizana na Dar,
Watakuja kujibu mkuu πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†..
 
Poleni sana Baasheee

Nimefurahishwa na Mafinga TC na Mufindi DC kama wasingetenganishwa hii Wilaya ya Mufindi ingekuwa na mapato ya 14.538Bil ambapo ingekuwa ya 7 Kitaifa...hatari sana kwa kweli.

Miaka miwili ijayo Makambako nayo itaingia top 50
Iringa manispaa ya 30
 
Wewe ndiye una shida kubwa sana kichwani kwako, maana mwanzoni ulituambia wilaya zote za Dar zimeunganishwa kwenye ile 75bn lakini sasa hivi umeshuka na figure nyingine!
Hiyo bil.75 umeitoa wapi? Wapi nilipoiandika kwenye Orodha hapo juu?.

Nimekwambia kwenye bil.167 ya Dar imehusisha Halmashauri zote za Dar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…