Orodha ya matajiri duniani imenichanganya. Elon siyo namba moja, sijaona mwarabu wa mafuta hata mmoja

Mayala B

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2019
Posts
2,109
Reaction score
5,284
Amani iwe nanyi ndugu zangu

Mimi huwa najua waarabu ndo watu matajiri zaidi duniani nikiamini Mansour wa Man City atakuwa hata tajiri wa tatu au nne duniani kumbe hata kwenye matajiri mia mbili duniani hayupo nimeshangaa sana.

Lakini nilichokutana nacho huko Forbes sijaamini macho yangu kama mashabiki ya Yanga ile jana

Sijaona Mwisilam hata mmoja , Mwisilam nimeenda kumukuta namba 144 naye ni mweusi mnaigeria Aliko Dangote

Naona wapagani tu wenye majina ya kizungu, naona Wahindi tu wenye majina ya kihindi, naona wacomunist tu wenye majina ya kikorea na kichina

Wakristo na waislam tumefell wapi? Waarabu na mafuta yao wameangukia wapi?

Kumbe tena Elon Musk siyo namba moja

Duh! Nawasilisha
 

Attachments

  • Screenshot_20241208-174205.png
    96.5 KB · Views: 6
Tofautisha utajiri wa mtu na mali za ukoo. Mtu anaweza akawa Mfalme au Sultan halafu mali zote za nchi au ukoo zikawekwa chini ya uangalizi wake.
Rejea utajiri wa Sultan wa Brunei.
 
Sidhani kama wanaweka utajiri wa familia kama familia bali wa mtu mmoja mmoja ambapo mfano falme ya kifalme ya saudi arabia ina utajiri wa 1.4 tillioni hiyo ni familia. Wakati MBS utajiri wake unakadiriwa kuwa ni bilioni 25 na mtawala wa duabi anakadiriwa kuwa na utajiri wa 18 bilioni. Wakati bwana elon yeye kama yeye ana 354 bilioni. Hivyo utaona ukichambua familia za kiarabu mtu mmoja mmoja basi hakuna anayemkaribia.
Ila pia kumbuka kuna watu wana pesa ila hawapigi kelele.
 
Huyu mleta uzi wala sio Muislam

Nawanasihi mapema sana Waislam wa Jf msiingie kwenye mabishano na malumbano katika uzi huu. Ndio lengo la mleta uzi. Msiingie mtego wake.
Mbona mimi hapo juu nimetaja dini tatu wewe unaniweka kwenye dini moja tu ndugu yangu

Kwani kuna dini hapo imetukanwa?

Na nimesema kabisa wakristo na waislam tunafel wapi?

Acha mihemuko changia topic
 
Ni Elon.

Japo kuna mahali nilisoma kwamba Putin ndo tajiri mkubwa hivi sasa, ana cash ya zaidi ya $100b, na mali za zaidi ya $300b...

CIA ndo wanaweza kujua nani tajiri mkubwa kwasababu wanashirikiana na SWIFT
 
Utajiri wa billion 25 $ ukiwafitilia hao matajiri utagundua ni kiwanda kimoja tu cha dangote ambacho kipo Nigeria ndo kina thaman hiyo kwahiyo kama huyo mwana mfalme ana utajiri huo bas dangote anaweza kumwajiri hata kuosha vyombo pale lagos
 
Ni Elon.

Japo kuna mahali nilisoma kwamba Putin ndo tajiri mkubwa hivi sasa, ana cash ya zaidi ya $100b, na mali za zaidi ya $300b...

CIA ndo wanaweza kujua nani tajiri mkubwa kwasababu wanashirikiana na SWIFT
Kuna jamaa anaitwa Bernard siyo Elon ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…