Orodha ya matukio yaliyotikisa nchi tokea uhuru

Kuna kitu kinafikirisha kidogo though kwa mawazo ya KIJADI; kwanini mwaka mmoja tu baada ya uchaguzi unao mfanya Mkapa kua madarakani watu wengi wana kufa vifo vya AJALI? 1996 MV BUkoba, 2001 Reli ya kati inapiga tukio!? Is it just a coincidence!!????? Nawaza tu kipumbavu
 
Mkuu britanicca
  • Mauaji ya Raisi Karume yako wapi ???
  • Ule Uhaini wa wakina Hans Poppe na Maganga uko wapi ???
  • Tanzania kutengwa na Umoja wa Afrika liko wapi ???
  • Kuchomwa moto BOT je ??
  • Mauaji ya Dr Mondlane yako wapi ???
  • Mauaji ya Jenerali Kombe yako wapi ???
  • Njaa ya fungafunga na lile songombingo la ukame viko wapi ??? (Unakumbuka unga wa Yanga ??)
  • Ule uvamizi Uchwara wa Malawi kipindi cha vita ya Kagera unauacha wapi ???
  • Ule Mkwarwa bubu wa Kenya kutaka kutwangana kijeshi na Tanzania baada ya vita ya Kagera uko wapi ???
  • Ule Mkwara bubu wa Kagame kule mpakani kipindi cha Raisi Kikwete uko wapi ???
  • Kuzama kwa MV Bukoba kuko wapi ???
  • Yule jamaa Mzungu aliyesema anaweza kuiweka Serikali mfukoni akapigwa viboko je ???
  • Baba Mtakatifu John Paul wa II kutembelea Tanzania na kubusu ardhi yake ??😀😀😀
  • Raisi Nyerere kutapelewa meli na kampuni hewa la nje ya nchi ??? Bwahahahaha wakaficha 😀😀😀
  • Mauaji ya kibiti yako wapi ???
  • Mauaji ya Kilosa yako wapi ??
  • Mauaji ya Mwembechai ???
  • Mauji ya Zanzibar 2001 ???
  • Mauaji ya Dr Klerruu na bwana Mwamwindi ???
  • Kunyongwa kwa Saidi Mwamwindi ???
  • Kifo cha Mkuu wa Mkoa Mbeya Bwana Marwa kwa kuvimba tumbo baada ya kuwatukana Wanyakyusa (Wamanyafu) 😀?
  • Mabadiliko ya katiba kuruhusu haki za binadamu ???
  • Kuanguka kwa soko la katani ???
  • Ufisadi wa Richmond
  • Ufisadi wa EPA
  • Ufisadi wa RADA
  • Ufisadi TEGETA ESCROW
CC: Consigliere , chige , Palantir, Red Giant , zitto junior
 
Haha yaweke sawa
 
Jaribio la kupindua serikali lililomuhusisha Lugakingira,Hatty Maghee,na wenzao.Mwaka sina uhakika sana ila no miaka ya themanini.
Ongezea na ajali ya MV Bukoba.
Ni Pius Lugangira a.k.a Uncle Thom acha kuchafua majina ya watu.
 
1983 - hakuna tukio hilo ,

Jumbe alijiuzulu uraisi mwaka 1984 tena sijasikia kuwa alitaka kuiuza Zanzibar Uarabuni , Mimi nilikuwepo , Kosa lake alikuja kuamka na kutaka kuitoa Zanzibar kutoka kwenye uvamizi wa mkoloni Tanganyika ili iwe huru
Alikuwa ameandaa walaka wa kuitaka mahakama ya kikatiba kama ilivyo kwenye Hati ya Muungano na Sheria zake ,kuhusu tafsiri na muundo wa Muungano.
 
Yote yamefunikwa na tundu lissu kupigwa risasi, kila mtu alijua kuanzia mtoto, na kupotea kwa ben wa saanane!
 
*Kifo cha Christopher Mtikila
*Mzee vijisenti apata ajali na vimwana kwenye bajaji.
*Bomba dear yapaki kwa zaidi ya mwezi bila kutembea hewani.
*Babu seya na watoto wake waachiwa huru.
 
Kuhusu kusema kuwa hayo ni masuala yasofutika vichwani mwa watanzania, Inategemea sana rika la hao watanzania, maana sehemu kubwa ya watanzania sio tu hawakuwako miaka hiyo ya matukio mengi,bbali pia hawaelewi uzito wake, na baadhi hayafundishwi mashuleni katika historia
 
1983 - hakuna tukio hilo ,

Jumbe alijiuzulu uraisi mwaka 1984 tena sijasikia kuwa alitaka kuiuza Zanzibar Uarabuni , Mimi nilikuwepo , Kosa lake alikuja kuamka na kutaka kuitoa Zanzibar kutoka kwenye uvamizi wa mkoloni Tanganyika ili iwe huru
Jumbe alilazimishwa kwa sababu alitaka zanzibar ijitoe kwenye muungano. Akafungwa kifungo huru kigamboni hakuna kufanya mkutano wala kuzungumza kitu chochote kwenye kadamnasi. Huduma zote zinamkuta ndani hata akiugua madoctor wanamtibia humohumo ndani mwake. Hadi anakufa kwa vijana wasasaivi hakuna aliyemuona Jumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…