Orodha ya matukio yaliyotikisa nchi tokea uhuru

Orodha ya matukio yaliyotikisa nchi tokea uhuru

Jumbe alilazimishwa kwa sababu alitaka zanzibar ijitoe kwenye muungano. Akafungwa kifungo huru kigamboni hakuna kufanya mkutano wala kuzungumza kitu chochote kwenye kadamnasi. Huduma zote zinamkuta ndani hata akiugua madoctor wanamtibia humohumo ndani mwake. Hadi anakufa kwa vijana wasasaivi hakuna aliyemuona Jumbe.

Kuonekana akionekana sana hasa kwenye mihadhara ya Marehemu Ngariba
 
Tulitangaziwa kuwa Jumbe alijiuzulu nafasi zote alizokuwa nazo baada ya Halmashauri Kuu kumtaka afanye hivyo,

ingawa tunajua kuwa alilazimishwa😛😛
Unabisha unachokisema
 
Mkuu britanicca
  • Mauaji ya Raisi Karume yako wapi ???
  • Ule Uhaini wa wakina Hans Poppe na Maganga uko wapi ???
  • Tanzania kutengwa na Umoja wa Afrika liko wapi ???
  • Kuchomwa moto BOT je ??
  • Mauaji ya Dr Mondlane yako wapi ???
  • Mauaji ya Jenerali Kombe yako wapi ???
  • Njaa ya fungafunga na lile songombingo la ukame viko wapi ??? (Unakumbuka unga wa Yanga ??)
  • Ule uvamizi Uchwara wa Malawi kipindi cha vita ya Kagera unauacha wapi ???
  • Ule Mkwarwa bubu wa Kenya kutaka kutwangana kijeshi na Tanzania baada ya vita ya Kagera uko wapi ???
  • Ule Mkwara bubu wa Kagame kule mpakani kipindi cha Raisi Kikwete uko wapi ???
  • Kuzama kwa MV Bukoba kuko wapi ???
  • Yule jamaa Mzungu aliyesema anaweza kuiweka Serikali mfukoni akapigwa viboko je ???
  • Baba Mtakatifu John Paul wa II kutembelea Tanzania na kubusu ardhi yake ??😀😀😀
  • Raisi Nyerere kutapelewa meli na kampuni hewa la nje ya nchi ??? Bwahahahaha wakaficha 😀😀😀
  • Mauaji ya kibiti yako wapi ???
  • Mauaji ya Kilosa yako wapi ??
  • Mauaji ya Mwembechai ???
  • Mauji ya Zanzibar 2001 ???
  • Mauaji ya Dr Klerruu na bwana Mwamwindi ???
  • Kunyongwa kwa Saidi Mwamwindi ???
  • Kifo cha Mkuu wa Mkoa Mbeya Bwana Marwa kwa kuvimba tumbo baada ya kuwatukana Wanyakyusa (Wamanyafu) 😀?
  • Mabadiliko ya katiba kuruhusu haki za binadamu ???
  • Kuanguka kwa soko la katani ???
  • Ufisadi wa Richmond
  • Ufisadi wa EPA
  • Ufisadi wa RADA
  • Ufisadi TEGETA ESCROW
CC: Consigliere , chige , Palantir, Red Giant , zitto junior
Naongezea
  • Yule mama fisadi?
  • Kesi ya Kambona na bibi Titi?
  • Kuanguka azimio la Arusha?
  • Yule mkurya na Jamhuri ya Chui?
  • Uchaguzi mkuu 2015?
 
Haya ni matukio muhim yaliyotokea na kutikisa nchi

1962: Mwalimu Nyerere kujiuzuru uwaziri mkuu wakati ameijenga Tanganyika kwa heshima, wengi walishangaa kumbe alikuwa na malengo yake,

1962: kilianzishwa chuo kikuu cha kwanza UDSM pale Lumumba kabla ya kuhamia kilipo sasa hivi,

1963: Jaribio la kwanza la Kumpindua mwalimu Nyerere , kwa bahati nzuri halikufanikiwa, na Nyerere akaomba usaidizi wa waingereza,

1964 : Mapinduzi makubwa ya mfumo ndani ya jeshi , mwalimu karibia alifukuza jeshi zima na recruitment ikaanza upya chini ya jeshi la waingereza,

1964 : Kubadiri jina la nchi kutoka Tanganyika na kuwa Tanzania kutokana na muungano na Zanzibar

1965 : Uanzishwaji wa Benki kuu ya Tanzania, baada ya EACB kuvunjwa,

1967: Azimio la arusha lilitikisa nchi na kuja na mpango wa utaifishaji,

1971: Tanzania iliingia mgogoro kwa mara ya kwanza na Uganda, lakin mwalimu Nyerere akajiandaa kwenda urusi kuomba silaha baada ya kugundua jamaa aliyekuja ni upuuzi, Amini mwaka huo alitikisa kiberiti kwanza kwa kuichapa kyaka,

1972 : Waziri Fundikira alitandikwa viboko na kufungwa jela kwa kosa la rushwa,

1977: Kujiondoa katika EAC
1978: Vita na Uganda ambayo iliacha matatizo makubwa sana,

1980: Mwalimu Nyerere aliatoa pendekezo la kung'atuka , watanzania wa karibu yake wakakataa na kusema mwalimu itaonekana unayakimbia matatizo haya, akahairisha,

1982: Ndege ya Air Tanzania ilitekwa na kupelekwa uingereza, na vijana machachari wa Tanzania,

1983: Kuwekwa kizuizini kwa aliyekuwa rais wa Zanzibar na makamu wa rais wa JMT kwa kipindi hicho Aboud Jumbe, kwa kutaka kuiuza Zanzibar uarabuni,

1984: Ajari ya gari na kumuondoa Moringe Sokoine, waziri mkuu wa Tanzania ambaye alitisha sana,

1985: Mwalimu Nyerere aling'atuka na kumuachia mzee Mwinyi,

1992: Uanzishwaji wa Vyama vingi vya siasa,

1994 : Kujiuzuru kwa Bwana Augustine Lyatonga Mrema, ilitikisa sana, na kuleta tahamaki kwa nchi,

1995: Uchaguzi wa Vyama vingi kwa mara ya kwanza Tanzania,

1996: Ajari ya Mv Bukoba iliua maelf ya watu

1999: Kifo cha mwanzilishi wa Taifa ili Mwalimu Nyerere huko London,

2002 : Ajali ya Treni Dodoma na kuua namia ya watu,

Hayo ndo matukio ambayo so rahisi kufutika vichwani mwa watanzania walio wengi

Ongeza mengine unayojua,

Britannica
1990 : Kuja kwa Baba Mtakatifu Papa Yohane Paulo wa Pili
 
Ila una kumbukumbu aseh hadi Mzee kifimbo kuingizwa mjini [emoji23]
Hahahaha, Babu ali-mind kinoma.
Nadhani walimfanyia uzandiki wa maksudi kabisa ili kukwamisha juhudi zake maana alikuwa anawaweza kweli.
 
kama walivyomzidi kwenye poromoko la uchumi baada ya vita ya kagera!..
Walimbana sana, tena kwa kumkomoa!
Alikuja kuwatolea gesi miaka ya 90 kwenye mkutano moja hivi. Akawauliza hivi ninyi mlipigia debe zana Structural Adjustment Programmes mkatudharau sisi, sasa nawauliza mbona na ninyi hamjafanikiwa ??? Wakabaki wanatoleana macho tu. Naona alikuwa amejaa gesi muda mrefu sasa akaamua kuwatolea uvivu......
 
2017 mnafiki mmoja hivi domo kubwa anashirikiana na wamarekani kuihujumu nchi...
 
Back
Top Bottom