toriyama
JF-Expert Member
- Feb 18, 2014
- 1,566
- 3,234
Nov 23,2025
Orodha ya matukio yanayoenda tokea aftermath MO29 ili kuwapumbaza GEN-Z NA na Wananchi kiujumla nilichelewa kuandika matukio haya awali nikiwa na mashaka either wataufuta uzi, naomba thread hii isiunganishwe ili iwe rahisi ku update maana sitatumia links aina yeyote chini ya haya maelezo nitakuwa naweka sauti ili iwe Rahisi kwa wasikilizaji na wasomaji ambao hawana acces ya kumsikiliza mtoa taarifa.
habari Mtanzania, mambo vipi , lakini una mambo muhimu yanakwenda kutokea. Mambo ninayoyasema sasa hivi ni mambo ambayo yatatokea baadaye ; kwa sasa bado hayajaanza kujitokeza waziwazi, lakini yatatokea.
Kuna jambo linalokwenda kutokea kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan. Ameanza kuwatuma mawaziri wafanye ziara maeneo mbalimbali, lakini mara nyingi wanapangiwa “script” ili waonyeshe kwamba Serikali inawafikia wananchi moja kwa moja. Kuna mambo mengine makubwa atakayokuja kuyafanya Paul Makonda ndani ya siku chache zijazo—labda chini ya siku nne au tano, ndani ya huu mwezi. Atakuwa na ziara ambazo atajionyesha mkali katika kupambana na maovu yanayoendelea katika sekta mbalimbali za serikali.
Ziara hizi, pamoja na mambo mengine yanayofanywa sasa, yanalenga kuwapumbaza wananchi ili waone kwamba huu ndio muda wa kushirikiana na serikali kujenga taifa. Lakini tukianza kushirikiana nao sasa, baada ya kama miaka miwili mbele, wanaweza kubadilika na kuurudisha mfumo ule ule wa zamani. Wanatengeneza mazingira ya kuja kubananga Taifa hapo baadaye, baada ya kuwa tayari wameshapata uhalali wa kisiasa kutoka kwa wananchi.
Mambo haya yanatarajiwa kutokea kabla ya mwisho wa mwezi huu au siku za karibuni sana. Samia atafanya ziara katika sekta mbili au tatu kubwa nchini Tanzania: sekta ya madini au gesi, bandari, au hospitali. Katika ziara hizo kutakuwa na jambo fulani litakalofanywa ambalo litaonekana lina manufaa moja kwa moja kwa Watanzania. Hapo ndipo tutakapoweza kupumbazwa na kuchukulia kama msaada mkubwa, kumbe ni kama “kiini macho”.
Inawezekana pia usishangazwe na hatua za Samia kufuta baadhi ya kodi zilizokuwa kero kwa wafanyabiashara. Kodi hizo zinaweza kufutwa kwa muda mfupi ili kupunguza malalamiko, lakini baadaye zikarudishwa kama ilivyokuwa mwanzo. Hivyo, tunatakiwa kuwa makini tusipigiwe “vini macho” na matamko ya muda mfupi tu.
Kabla ya tarehe 31 Desemba, kuna uwezekano mkubwa wa ziara katika maeneo yanayohusu afya, bandari na madini. Lengo lake ni kupunguza makali na hasira za Watanzania ili baadaye iwe rahisi kuubana taifa bila upinzani mkubwa. Wakati huohuo, jeshi la wananchi nalo limegawanyika; kuna masuala ya kijeshi ambayo yataanza kuwekwa hadharani kupitia baadhi ya watu mtandaoni, na video mbalimbali zitaendelea kuelezea mambo hayo mpaka mwisho.
Kuna ushauri utakaotolewa kwa wananchi kuhusu namna ya kuzuia mapato ya serikali ili kuonesha kutoridhika, kama vile:
Lengo la mashauri haya ni kuifanya serikali isipate mapato yake, ishindwe kuongoza taifa, halafu hapo ndipo paonekane kama taifa linaenda kuokolewa kwa nguvu za nje au kwa mfumo mwingine. Mawazo haya ya kijeshi na ya kimkakati yataendelea kusambazwa mitandaoni na watu kama kina Mange Kimambi na wengine, ili kuwashauri Watanzania jinsi ya “kumpinga” au “kumnyima fursa” Samia.
Kwa sasa, tunapaswa kusubiri kuona hizi ziara za kushtukiza za Samia katika sekta kubwa za taifa, kwa sababu atazitangaza kama juhudi za kulinda rasilimali za nchi. Lakini ndani yake kuna mkakati wa kutafuta njia ya kujipatia uhalali wa kisiasa (political right) na kujionyesha kwamba yeye ndiye Rais halali mwenye mamlaka kamili mbele ya macho ya wananchi.
Kwa ufupi, usishangazwe ukimsikia Samia anatoa misaada hospitalini, anapunguza kodi fulani, au anatangaza hatua zinazoonekana ni za huruma kwa wafanyabiashara na wananchi. Anafanya hivyo ili kujijengea taswira mpya mbele ya wananchi na kutoka kwenye mtego wa kuchukiwa. Ni mkakati wa kisiasa wa kufikia wananchi moja kwa moja na kuonekana kama kiongozi mwema, ilhali malengo ya mbali yanaweza kuwa tofauti.
Kuhusu suala la maridhiano ya kitaifa, hilo nitalizungumza katika video inayofuata (hii ikiwa ni sehemu ya pili, part 2; video inayofuata itakuwa part 3). Nitazungumzia kinachoenda kutokea katika suala la maridhiano, majibu ya Samia, na ujanja utakaozunguka namna ya kukwepa kuwajibika kwa makosa yaliyofanyika dhidi ya wananchi. Njia atakazotumia kujinasua tayari zinaanza kuonekana kupitia mashauri yanayotolewa mitandaoni na watu wanaoonekana kama wametengwa au wanapingana na mfumo, lakini kiuhalisia wanachelewesha tu ufikaji wa ukweli.

- Wananchi kukwepa kodi kwa makusudi,
- Au kuhamasisha watu wasije Tanzania kwa utalii, kwa madai kwamba Tanzania ina matatizo makubwa ya uvunjifu wa haki au “inamwaga damu”.