Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,712
Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua mikopo tangu enzi katika kutimiza majukumu yake ya kimaendeleo na kila siku. Deni la Taifa limekuwa likikua huku Serikali ya awamu ya sita ikilifikisha trilioni 91 kwa miaka 3 iliyokuwa madarakani kutoka trilioni 60 iliyoachwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
Hili ni ongezeko la zaidi ya 50% ya deni lililoachwa March 17, 2021 kwa miaka mitatu. Pamoja na kuwa himilivu, kuna sehemu kubwa ya bajeti ya nchi inatumika kulipa madeni haya na kupelekea mchezo wa kukopa hela kutimiza mipango huku hela unazokusanya zikienda kulipa madeni mpaka kupelekea kuwa giza tuendako.
Mwenendo wa deni wa Taifa ulipelekea spika wa Bunge, Job Ndugai kujiuzulu nafasi yake baada ya kusema Ipo siku Tanzania itapigwa mnada baada ya kupelekea mjadala na sintofahamu kubwa.
Nikaona tuweke orodha na itakuwa inaongezeka kulingana na mwenendo wa deni letu, ikianza na deni la mwanzo kulekea mwisho
==========
Hili ni ongezeko la zaidi ya 50% ya deni lililoachwa March 17, 2021 kwa miaka mitatu. Pamoja na kuwa himilivu, kuna sehemu kubwa ya bajeti ya nchi inatumika kulipa madeni haya na kupelekea mchezo wa kukopa hela kutimiza mipango huku hela unazokusanya zikienda kulipa madeni mpaka kupelekea kuwa giza tuendako.
Mwenendo wa deni wa Taifa ulipelekea spika wa Bunge, Job Ndugai kujiuzulu nafasi yake baada ya kusema Ipo siku Tanzania itapigwa mnada baada ya kupelekea mjadala na sintofahamu kubwa.
Nikaona tuweke orodha na itakuwa inaongezeka kulingana na mwenendo wa deni letu, ikianza na deni la mwanzo kulekea mwisho
==========
- Mbunge Josephine Genzabuke, aishukuru Serikali ya CCM kwa kupata Mkopo wa Sh. Bilioni Laki Tatu-Jun 3, 2021
- Tanzania yakopa Benki ya Dunia tsh 2.7 trilioni kwa ajili ya Elimu, Barabara na Mawasiliano!-Aug 19, 2021
- IMF yaidhinisha mkopo wa Tsh Trilioni 1.2 kwa ajili ya Corona Tanzania-Sep 8, 2021
- Tanzania imepokea bilioni 67.82 kutoka Serikali ya Ujerumani kupitia Benki yake ya Maendeleo ya KfW-Sep 8, 2021
- Japan yaipatia Tanzania mkopo wa Shilingi bilioni 761.8. Zanzibar yapata mgao wa Tsh bilioni 218-Feb 4, 2022
- Ziara ya Rais Samia Ufaransa: Tanzania yasaini Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wa Euro Milioni 178-Feb 12, 2022
- Benki ya Dunia yaipa Tanzania mkopo wa Tsh Trilioni 1.5-Feb 21, 2022
- Tanzania yapokea mkopo wa trilioni 1.2 kutoka Benki ya Dunia. Kuboresha tabia nchi, usalama na barabara-May 27, 2022
- Tanzania yapata Mkopo wa Dola Mil 278 kutoka Benki ya Dunia-Jun 16, 2022
- Ufaransa yaikopesha Tanzania shilingi bilioni 195 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Usambazaji wa Maji safi Shinyanga-Jun 21, 2022
- IMF yaidhinishia Tanzania mkopo wa Trilioni 2.4-Jul 19, 2022
- Tanzania yapewa mkopo nafuu wa trilion 1.24 kutekeleza mradi wa REA na daraja la Jangwani mto Msimbazi-Nov 21, 2022
- Benki ya Dunia yaidhinisha Mkopo wa Shilingi Trilioni oni 1.8 kwa Tanzania kwa ajili ya Sekta ya Afya na kuimarisha Uchumi-Dec 22, 2022
- Serikali yapata mkopo wa Tsh. Bilioni 650 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mradi wa BRT awamu ya 4 & 5 mwaka 2023-Dec 29, 2022
- Tanzania kupata mkopo mwingine wa Tsh. Bilioni 353.3 kutoka IMF ili kusaidia Uchumi-Feb 28, 2023
- StanChart Bank Yaipatia Tanzania Mkopo Nafuu wa Shilingi Bilioni 1.4 Kwa Ajili ya Sgr Lot 3 & 4-Mar 15, 2023
- Tanzania yapata mkopo wa nyongeza Dola Mil 153 kutoka shirika la fedha duniani (IMF)-Apr 25, 2023
- Benki ya Dunia imetoa Mkopo wa zaidi ya Shilingi Bilioni 700 Kwenye Kilimo-Jun 1, 2023
- Uingereza Yaipa Zanzibar Mkopo wa Sh.Tilioni 1 Kujenga Uwanja wa Ndege Pemba-Jun 20, 2023
- Zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kujenga upya Hospitali ya Muhimbili, Mkopo utalipwa baada ya miaka 25-Aug 11, 2023
- Benki ya AfDB yaidhinisha Mkopo wa Tsh. Bilioni 165.6 kwaajili ya kusaidia Benki ya Kilimo Tanzania (TADB)-Dec 11, 2023
- African Development Bank yaidhinisha mkopo wa zaidi ya trilioni 1.4 kujenga reli itakayounganisha Burundi na Tanzania-Dec 13, 2023
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51-May 30, 2024
- Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar-Jun 5, 2024
- IMF yaidhinisha ufadhili wa Dola Milioni 900 kwa Tanzania kwa ajili ya Bajeti na kukabiliana na Mabadiliko ya hali ya Hewa-Jun 21, 2024