Ni kweli ila kama una Imani ktk Yesu Kristo unaweza badilishaaa kwa maombi ktk Jina la Yesu na hayatatokea ktk Hali ya kifizikia.. Au mwili. La msingi uwahi tu kuomba Mara unapoamka.
Nakukumbusha pia kuwa ndoto si laana kuwa mara zote uikemee, bali ndoto ni ujumbe na hili uote ina maana kama binadamu umepewa kibali cha kujua yanayotokea katika ulimwengu wako wa mwili na kiroho ili ujiandae, ubariki au ukabiliane na tatizo, na mtu ambaye haoti ni sawa na mtu asiye hai.
 
Ni ishara anataka utambue kuwa hauko peke yako na pengine hakupata muda wa kukuonesha mapenzi yake yote kipindi cha uhai wake,(kujihisi upweke) roho yake bado hii pamoja nawe ikikulinda kwa upendo na kukutakia mema kila siku (ishara ya kukuvulia vazi lake la pekee na la heshima bila kujijali yeye),

Ni muda sasa wa kuachana na yaliyopita (mwonekano wa uzee) na kufurahia wakati wako/kuishi wakati uliopo (ubinti).

NB: Usiache kumwombea mara kwa mara na kutembelea mara moja moja malalio yake kutoa heshima na kumjulia hali kwa kukumbuka mema yake.
 
No 18...kuota unaongea Kingreza..😌😌🤔😁😁
 
Nakumbuka ni Shehe Yahya ndiye alikua anaongea hizi ishu Channel Ten
 
Mimi na ndoto nyingi huota nyingine hutokea ka nilivoota ila Kuna ndoto Huwa naota mara nyingi napambana na wanawake wananishtumu Kwa vitu vya uongo na kunitupia vitu hatari, hao hao wanawake nikiwa napigana nao hubadilika na kuwa nyoka, napigana naye then anabadilika kuwa dubu, in short ndoto hii ya kupambana na wanawake nakuletewa mashtaka inanitesa sana Tena heri mashtaka ya kweli Sasa ya uongo
 
Nakumbuka ni Shehe Yahya ndiye alikua anaongea hizi ishu Channel Ten
Yap, Ni karama ambayo mtu yeyote anaweza kujaaliwa nayo, hata wewe hapo ulipo unaweza kututafsiria ndoto zetu.
 
Niliota nimepew ela hii imekaaje
 
Kuna hatua fulani ya mabadiliko ya kimaisha ulipaswa uwe umeshapiga lakini tabia yako ya kujishuku ambayo umeshindwa kuiacha inakufanya ushindwe kupiga hatua. Usiogope kukabiliana na hali au watu au jambo jipya ambalo haujalizoea katika maisha yako badala yake keep fighting-pambana na changamoto hii na uweze kufanikiwa.
 
Asante sana
 
Mimi niseme tu hivi kama nimelala sober sijanywa pombe wala kuvuta sigara na marijuana sana nitaota lkn nikitumia hivyo vitu sioti kabisa...Na nikiota ndoto zangu hutokea kabisa hii inaweza kuchukua hata miezi ndipo naona ile njozi inajitokeza kwenye hali halisi ya maisha...

Swali: Ni kwanini nikitumia pombe, Sigara na marijuana sioti kabisa?
 
Juzi nimeota natembea barabarani uchiii kabisa cha ajabu hakuna anaenishangaa na mimi nipo natembea tu hata sijizibi watu wasione....kwamba ndio nitaaibika maana yake???[emoji848]
Soon unafedheheka eva [emoji1][emoji1][emoji1787][emoji1787]
 
Sijajua kama ntakujibu vyema mkuu kwa kuwa swali lako linahitaji majibu ya kisayansi ila ntakujibu kwa kadri ninavyoelewa;

Si kweli kuwa hauoti unapokuwa umetumia vileo au mihadarati bali unakuwa huwezi kukumbuka ulichoota wakati ukiwa katika hali hiyo.

Unywaji wa pombe kupita kiasi upelekea hali ya 'kuzimia usingizini' ambapo mnywaji kwa wakati huu hawezi kuota wala kuisi chochote zaidi ya kukoroma katika usingizi mzito sana, mara nyingi sumu inaposhuka katika damu muhusika ushtuka ghafla usingizini normally saa 10 alfajiri na hapo kibofu umfosi kuwahi chooni.

Ukirejea kitandani ni usingizi unaitwa wa mang'amung'amu yaani nusu umelala nusu haujalala kwa kuwa pombe au mihadarati uliyotumia inakuwa imekata mawasiliano ya ubongo na uvuruga usingizi na kufanya shughuli za ubongo zisiwe katika utaratibu wa kawaida na hivyo ubongo unakuwa na kiu ya kukamilisha kazi yake iliyokatishwa ya kuhifadhi data.

Huu ndiyo muda ambao ubongo unajaribu kurudi katika 'REM sleep' hii ndiyo hatua ya usingizi tunapoota (kwa maana ya kumbukumbu za muda mfupi zinaporejelewa hili kunakiliwa katika memory ya muda mrefu)

Sasa ikitokea kwa bahati ukaota ndoto katika hatua hii mara nyingi ndoto unazoota ni lucid au ndoto ambazo hazina rangi yaani ni black and white hivyo unashindwa kujua kama unaota au huko macho au huko kwenye tafakuri isiyokoma.
 
Majibu yako kwa asilimia flani kipindi cha nyuma sana ndio nilikua na hio hali lkn kwa sasa sio hivyo...Nilijaribu kufanya uchunguzi kwamba nikiwa normally nakua kwenye hali gani na nikiwa nipo higher nakua kwenye hali gani hivyo nilibadili hali yangu nakuchagua namna ya tofauti ninapokuwa usingizini hivyo sioti ndoto bali napata njozi na mara nyingi hujitokeza kwenye maisha yangu halisi, Nakama ni swala la ndoto hapo awali nilikua kila nikiamka navuta hisia na kukumbuka yale yote niliyaona usingizini kwani mimi binafsi ni muoga sana wa kupoteza kumbukumbu iwe kwenye matendo halisia au ndotoni na nadhani baada ya kuwa na nadharia hiyo ndoto zangu zimebadilika na kuwa njozi..!!
 
Ni kweli binadamu yeyote anauwezo wa ku-train ubungo wake ku-respond kulingana na kile anachotaka kiwe (ndiyo maana watu wanafanya tahajudi) japo haiondoi uhalisia kuwa nje ya ndoto ambazo unazikumbuka na ukutokea katika maisha ya uhalisia bado unaota makumi kwa mamia elfu ya ndoto ambazo huwezi zikumbuka kama ilivyo tu kwa binadamu wote,

Mara nyingi katika hali kama hii (watu wengi wanaokunywa pombe hasa wanaume usupress fahamu zao ziendelee kubakiwa na utambuzi hata pale watakapokuwa wamelewa chakari hili kujilinda na kulinda wenza wao)

Wahusika ujikuta wakiujengea ubongo wao utaratibu wa tafakari thabiti ya ndani na mlengo fulani wa mawazo ambayo uleta matokea ya ndoto za njozi kama unazozisemea, hivyo ubongo unajaribu kuchagua unachotakiwa kukumbuka lakini vingine ubongo una-ignore japo unaota ila ubongo unatambua kuwa hauviitaji.

Wenzetu wazungu katika hili wapo mbali kidogo wanaweza kukuwekea vifaa vinavyorekodi mwenendo wako mzima wa usingizini na ukaweza kujua asubuhi utakapoamka uliota mara ngapi hata kama ukumbuki hata kimoja.
 

Nakusii usiache uelekeo huo kwa kuwa ubongo wetu una hazina kubwa sana ambayo haitumiwi na wengi wetu kujikomboa kifikra na ukiwa na nia utafika mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…