Orodha ya Simu ambazo ifikapo mwezi Novemba 2021 hazitaweza kuingia WhatsApp

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
MAELFU Ya watu duniani wanatumia mtandao maarufu wa WhatsApp kuwasiliana na ndugu, jamaa na watu wao wa karibu kwa meseji na video lakini watu wengi watashindwa kuitumia huduma hiyo kutokana na mifumo ya simu zao kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na chapisho la 'The Sun' la nchini Uingereza limeeleza kuwa program ya WhatsApp haitafanya kazi wa baadhi ya simu janja kuanzia Novemba 2021.

Kwa mujibu wa chapisho hilo imeelezwa kuwa program hiyo haitafanya kazi kwa baadhi ya simu za iPhone na Android na watumiaji wa simu hizo wameshauriwa kununua simu mpya au kusasisha simu zao (software updating.)

Imeelezwa kuwa aina 40 za simu janja hazitapata huduma hiyo huku huduma ya kusasisha ( software updating,) kwa watumiaji wa simu hizo utafikia ukomo Novemba mosi mwaka huu.

Ili watumiaji kuweza kutumia huduma hiyo watumiaji wa simu za Android wanatakiwa kutumia Android 4.1 na zaidi na watumiaji wa iPhone kutumia iOs 10 na zaidi.

Simu ambazo zitakosa huduma ya WhatsApp kuanzia Novemba ni pamoja na :

IPHONE
1. iPhone 5
2. iPhone 6S Plus
3. iPhone SE

SAMSUNG
1. Galaxy Trend Lite
2. Galaxy Trend II
3. Galaxy SIII
4. Galaxy S3 Mini
5. Galaxy Xcover 2
6. Galaxy Core
7. Galaxy Ace 2

LG
1. Lucid 2
2. Optimus F7
3. Optimus F5
4. Optimus L2 II Dual
5. Optimus L5
6. Best L5 II
7. Optimus L5 Dual
8. Best L3 II
9. Optimus L7
10. Optimus L7 II Dual
11. Best L7 II
Optimus F6, Enact
12. Optimus L4 II Dual
13. Optimus F3
14. Best L4 II
15. Best L2 II
16. Optimus Nitro HD
17. Optimus 4X HD
18. Optimus F3Q

ZTE
1. ZTE V956
2. Grand X Quad V987
3. Grand Memo

SONY
1. Xperia Miro
2. Xperia Neo L
3. Xperia Arc S

HUAWEI
1. Ascend G740
2. Ascend Mate
3. Ascend D Quad XL
4. Ascend D1 Quad XL
5. Ascend P1 S
6. Ascend D2

SIMU ZINGINEZO NI PAMOJA NA
1. Alcatel
2. Archos 53 Platinum
3. HTC Desire 500
4. Caterpillar Cat B15
5. Wiko Cink Five
6. Wiko Darknight
7. Lenovo A820
8. UMi X2
9. Run Fl1
10. THL W8
 
Sawa
 


Tecno Ni Brand Kubwa Isiyojulikana Kutokana Na Mambo Yake Ya Ajabu

TECNO wako vizuri ila wanadharaulika kutokana na kutengeneza pia simu za bei ya chini kwa watu wengi wa kipato cha chini ndio maana bidhaa zao zote zinaonekana ni za kawaida. Watu wanaona ufahari kumiliki brand ambayo bei yake iko juu na ina watu wachache wanazozimiliki kama fasheni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…