Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
Mimi na wewe hatujui labda tupate wadau toka jikoni kabisa, maana haiwezekani kabisa kwa miaka yote hiyo asiweze kuuliza swali hata moja.. hata la kizushi tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nadhani ingekuwa vema wasifike kabisa bungeni mara baada ya kuwakilisha hojas zao kwa maandishi...!
Kila dakika 1 , i mean kila mshale wa saa unapozunguka kwa mbunge kuwepo pale Bungeni ni fedha ya mlala hoi inazunguka na kutumika..
why should those kind of NANA`S kuwa pale ?
Asikudanganye mtu, kama ni kuleta maendeleo jimboni RA amefanya makubwa kuliko baadhi ya wabunge wanaoongea sana BungeniMuda mwingi sana alikuwa anafanya mambo yake na kuona na kupambana na wabaya wake, yaani mzee wa Kichaga. hivyo na kujua miradi yake inakwendaje, jamani mwenye data za kutoka Igunga aje nazo ili tupime mambo haya. maana kuna shule ngapi?? Zahanati ngapi zimejengwa?? au vitu gani vya maendeleo
Kupiga domo sana bungeni bila na mipango mkakati wa ufatiliaji manedeleo ya jimbo haisaidii, kwa wanaokumbuka enzi za kina Msuya wa jimbo la Mwanga walikuwa hawapigi kelele saaana lakini hadi leo hii sijui kama kuna jimbo Tanzania ambalo lina maendeleo kuzidi Mwanga, ni kama vile chatu akiwa porini habweki lakini anahakikisha halali njaa, Msanii Mrisho Mpoto katika moja ya tungo zake kaongelea swala la kuuza sura runingani nadhani alikuwa na maana pana kuliko ambavyo wengi twaweza fikiri!
Lete data kamili kuliko kusema kwa maneno tu.. maana inawezekana amefanya makubwa na ni kiasi kidogo sana ikilinganishwa na pesa ambazo za umma wa Watanzania zilizochukuliwa . Lete data kutokea akiwa mbunge na sio hivyo ilivyo leoAsikudanganye mtu, kama ni kuleta maendeleo jimboni RA amefanya makubwa kuliko baadhi ya wabunge wanaoongea sana Bungeni
OLD NEWSKatika gazeti la Leo Jumapili la Mwananchi kuna Habari kwamba Mbunge wa Igunga Mr. Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali hata moja akiwa Bungeni, Lakini wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa pengine imechangiwa na ubusy alikuwa nao Mbunge huyo wa Igunga.
Kwa Mara nyingi yeye mwenyewe amekaririwa na baadhi na vyombo vya habari kuwa amekuwa yeye amefanya mambo makubwa sana katika Jimbo la Igunga Mjini Tabora.
Umenena ndugu yangu, hakuna anayejali. RA anaogopwa sana na serikali ya CCM -- anaweza hata kuamrisha JK ajiuzulu -- na kweli JK akajiuzulu, kwani anaogopa asije RA akamwaga mambo -- you know Kagoda, Afriteiner, Richmond etc -- kutoa evidence walikuwa pamoja - Hard Hitter
Nyote hamjui kitu: RA yu bubu Bungeni kwa sababu huwa anazisoma hoja za Wabunge wengine ili aone vipi anaweza kuanzisha kampuni nyingi "hewa" za ukwapuaji wa mapesa ya wananchi bila kugundulika. Anasikiliza tu ajue Wabunge "wabwatukaji" wanagusa sehemu zipi na zipi hawazigusi. Hii pekee inataka utulivu na concentration ya hali ya juu na siyo kusema sema sana Bungeni.
Lakini hao wanaosemasema sana wameleta faida kubwa kwa nchi, na si lazima kwa majimbo yao: Mfano mkubwa ni kufanikisha kutinga kwa vigogo Keko. nani alitarajia akina Mramba na Yona wangekwenda kula dona kule?
Pili -- wamefanikiwa kumg'oa PM mmoja kiburi ambaye hakuna aliyetegemea angebwaga manyanga kiulaini vile. hakika ile ilikuwa ni nishai kubwa katika historia ya nchi hii.
Wabunge, endeleeni kusema Bungeni, hoja zenu zimeleta mabadiliko makubwa ya kihistoria!
Kupiga domo sana bungeni bila na mipango mkakati wa ufatiliaji manedeleo ya jimbo haisaidii, kwa wanaokumbuka enzi za kina Msuya wa jimbo la Mwanga walikuwa hawapigi kelele saaana lakini hadi leo hii sijui kama kuna jimbo Tanzania ambalo lina maendeleo kuzidi Mwanga, ni kama vile chatu akiwa porini habweki lakini anahakikisha halali njaa, Msanii Mrisho Mpoto katika moja ya tungo zake kaongelea swala la kuuza sura runingani nadhani alikuwa na maana pana kuliko ambavyo wengi twaweza fikiri!