Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Mimi na wewe hatujui labda tupate wadau toka jikoni kabisa, maana haiwezekani kabisa kwa miaka yote hiyo asiweze kuuliza swali hata moja.. hata la kizushi tu
 
Kupiga domo sana bungeni bila na mipango mkakati wa ufatiliaji manedeleo ya jimbo haisaidii, kwa wanaokumbuka enzi za kina Msuya wa jimbo la Mwanga walikuwa hawapigi kelele saaana lakini hadi leo hii sijui kama kuna jimbo Tanzania ambalo lina maendeleo kuzidi Mwanga, ni kama vile chatu akiwa porini habweki lakini anahakikisha halali njaa, Msanii Mrisho Mpoto katika moja ya tungo zake kaongelea swala la kuuza sura runingani nadhani alikuwa na maana pana kuliko ambavyo wengi twaweza fikiri!
 
Haya wapiga debe wa fisadi Rostam, kama FairPlayer na Game Theory kazi kwenu kumtetea huyu kilaza na jizi.

Acheni kutubabaisha, kwani huko Igunga kuna maendeleo gani ya kutolea mfano? Au mifuko yenu imetuna kwa kumpigia debe?

Kuchangia bungeni kuna umuhimu mkubwa sana. Sababu yake ni kwamba moja ya kazi kubwa ya wabunge ni kutunga sheria. Na hizi sheria hutungwa kwenye vikao vya bunge.
 
Hapa Ndipo tunapoingia Chaka ,tunadhani kazi ya Mbunge ni kujenge miundombimu n.k
hata kama ni FISADI kama RA,Mkono,EL just to list a few .Hii imesababisha mafisadi kujificha ktk kivuli cha siasa ,wanaiba sana wanarudisha kidogo tu kama misaada katika jimbo na Nchi inaendelea kuteketea
 
Muda mwingi sana alikuwa anafanya mambo yake na kuona na kupambana na wabaya wake, yaani mzee wa Kichaga. hivyo na kujua miradi yake inakwendaje, jamani mwenye data za kutoka Igunga aje nazo ili tupime mambo haya. maana kuna shule ngapi?? Zahanati ngapi zimejengwa?? au vitu gani vya maendeleo
 
Nadhani ingekuwa vema wasifike kabisa bungeni mara baada ya kuwakilisha hojas zao kwa maandishi...!

Kila dakika 1 , i mean kila mshale wa saa unapozunguka kwa mbunge kuwepo pale Bungeni ni fedha ya mlala hoi inazunguka na kutumika..

why should those kind of NANA`S kuwa pale ?

Wakishauliza unataka wakawajibishwe huko ndani ya chama chao? nadhani tutakuwa tunakosea sana kuwaamuru waulize maswali bila tija, tusisahau hiki ni kipindi cha mpito hapa Tanzania kwani haya tunayoyaona hayakuwahi kuwepo!
 
Muda mwingi sana alikuwa anafanya mambo yake na kuona na kupambana na wabaya wake, yaani mzee wa Kichaga. hivyo na kujua miradi yake inakwendaje, jamani mwenye data za kutoka Igunga aje nazo ili tupime mambo haya. maana kuna shule ngapi?? Zahanati ngapi zimejengwa?? au vitu gani vya maendeleo
Asikudanganye mtu, kama ni kuleta maendeleo jimboni RA amefanya makubwa kuliko baadhi ya wabunge wanaoongea sana Bungeni
 
Upande mwingine ujue kuwa kuuliza maswali sana si kipimo cha kuwajibika.
Kuuliza maswali ni kitu kimoja, na kuwajibika ni kitu kingine.
 
Kupiga domo sana bungeni bila na mipango mkakati wa ufatiliaji manedeleo ya jimbo haisaidii, kwa wanaokumbuka enzi za kina Msuya wa jimbo la Mwanga walikuwa hawapigi kelele saaana lakini hadi leo hii sijui kama kuna jimbo Tanzania ambalo lina maendeleo kuzidi Mwanga, ni kama vile chatu akiwa porini habweki lakini anahakikisha halali njaa, Msanii Mrisho Mpoto katika moja ya tungo zake kaongelea swala la kuuza sura runingani nadhani alikuwa na maana pana kuliko ambavyo wengi twaweza fikiri!

Ziko kazi kuu tatu za mbunge ambazo ni

  1. Kutunga sheria
  2. Kuwakilisha wananchi wa jimbo lake (sera sheria, mipango inayoandaliwa na serikali)
  3. Kusimamia (kudhibiti) serikali
Aidha ipo kazi nyingine moja (ndogo na ni jukumu mtambuka) ambayo ni kujadili na kupitisha/kutopitisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya serikali (bajeti).

Ufanisi wa mbunge kutekeleza kazi zake kama inavyoainishwa hapo juu ndio unaotegemewa kuleta maendeleo katika majimbo yao na maendeleo nchini kwa ujumla. Ufanisi huu hautegemewi kupatikana kwa njia ya mbunge kutoa pesa yake mfukoni kufanyia shughuli za meendeleo ya umma wala kunyemelea serikalini hadi kufanikisha 'allocations' ya fedha za umma kutumika katika jimbo lake pekee pasipo kwenda katika majimbo mengine. Kitendo hiki ni mojawapo ya bainisho la ufisadi, ambapo wananchi wanatumika kama ngao ya kufanikisha ufisadi. Iwapo Msuya alifanikisha maendeleo ya Willaya ya Mwanga kupitia njia hiyo, ilikuwa ni kosa kubwa; ole wake wabunge wenzake hawakuwahi kung'amua ufisadi huo.

Kwa kifupi ni kwamba haiyamkini kwa mbunge kufanikisha uwajibikaji katika jimbo lake bila kuuliza maswali na kuchangia hoja. Watu hawawakilishwi kimyakimya, sheria hazitungwi kimyakimya na wala serikali haidhibitiwi kimyakimya. Hata bajeti haiwezi kujadiliwa kimyakimya. Kilicho bayana ni kuwa Rostam Aziz hakuingia bungeni kumwakilisha yeyote bali kulinda biashara zake. Kinachoitwa maendeleo katika jimbo lake la Igunga ni njia ya kununua uhalali. 'Raia halali hawezi kununua uraia'. Fumbo mfumbie mjinga..
 
Asikudanganye mtu, kama ni kuleta maendeleo jimboni RA amefanya makubwa kuliko baadhi ya wabunge wanaoongea sana Bungeni
Lete data kamili kuliko kusema kwa maneno tu.. maana inawezekana amefanya makubwa na ni kiasi kidogo sana ikilinganishwa na pesa ambazo za umma wa Watanzania zilizochukuliwa . Lete data kutokea akiwa mbunge na sio hivyo ilivyo leo
 
Who is this RA?? Tanzania needs serious people who can solve serious issues? why on earth our mind is only thinking about this so called RA?

If government is in his pocket so as our mind???

Lets discuss big issues , how we can move these CCM and their roosta in power, we have tried them for forty years but in vain.Lets employ another party, which one, how, when, strategies etc.
 
Katika gazeti la Leo Jumapili la Mwananchi kuna Habari kwamba Mbunge wa Igunga Mr. Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali hata moja akiwa Bungeni, Lakini wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema kuwa pengine imechangiwa na ubusy alikuwa nao Mbunge huyo wa Igunga.

Kwa Mara nyingi yeye mwenyewe amekaririwa na baadhi na vyombo vya habari kuwa amekuwa yeye amefanya mambo makubwa sana katika Jimbo la Igunga Mjini Tabora.
OLD NEWS
Berlin-Wall-Tumbles-Print-C10109746-705422.jpeg

Na wewe mara ya mwisho umeuliza swali Bungeni lini?
 
Umenena ndugu yangu, hakuna anayejali. RA anaogopwa sana na serikali ya CCM -- anaweza hata kuamrisha JK ajiuzulu -- na kweli JK akajiuzulu, kwani anaogopa asije RA akamwaga mambo -- you know Kagoda, Afriteiner, Richmond etc -- kutoa evidence walikuwa pamoja - Hard Hitter

Hii nimeichukua kwa mwanaJF mwingine! RA is everything amedumaza hata watu kufikiria, ukiulizia uraia wake ama elimu yake huwezi pata jibu....watakuja vibaraka wake hapa....nakumbuka ile thread ya mwanakijiji nani hayuko kwenye circle za RA?
 
Nyote hamjui kitu: RA yu bubu Bungeni kwa sababu huwa anazisoma hoja za Wabunge wengine ili aone vipi anaweza kuanzisha kampuni nyingi "hewa" za ukwapuaji wa mapesa ya wananchi bila kugundulika. Anasikiliza tu ajue Wabunge "wabwatukaji" wanagusa sehemu zipi na zipi hawazigusi. Hii pekee inataka utulivu na concentration ya hali ya juu na siyo kusema sema sana Bungeni.

Lakini hao wanaosemasema sana wameleta faida kubwa kwa nchi, na si lazima kwa majimbo yao: Mfano mkubwa ni kufanikisha kutinga kwa vigogo Keko. nani alitarajia akina Mramba na Yona wangekwenda kula dona kule?

Pili -- wamefanikiwa kumg'oa PM mmoja kiburi ambaye hakuna aliyetegemea angebwaga manyanga kiulaini vile. hakika ile ilikuwa ni nishai kubwa katika historia ya nchi hii.

Wabunge, endeleeni kusema Bungeni, hoja zenu zimeleta mabadiliko makubwa ya kihistoria!
 
Umenena mkuu,
Kelele za akina Slaa tumeona matokeo yake ikiwemo EPA, Richmond etc. Kama wasingepiga kelele unategemea serikali wangefanya lolote? Si wangeendelea kutafuna kimya kimya tu. Wabunge lazima waongee bana.
 
Kupiga domo sana bungeni bila na mipango mkakati wa ufatiliaji manedeleo ya jimbo haisaidii, kwa wanaokumbuka enzi za kina Msuya wa jimbo la Mwanga walikuwa hawapigi kelele saaana lakini hadi leo hii sijui kama kuna jimbo Tanzania ambalo lina maendeleo kuzidi Mwanga, ni kama vile chatu akiwa porini habweki lakini anahakikisha halali njaa, Msanii Mrisho Mpoto katika moja ya tungo zake kaongelea swala la kuuza sura runingani nadhani alikuwa na maana pana kuliko ambavyo wengi twaweza fikiri!

Mkuu,
Naona wewe umesahau kuwa Msuya alikuwa na nyadhifa zipi hata kuleta maendeleo huko jimboni kwake na kwa nini alikuwa haongei sana bungeni. Sikumbuki nyadhifa zake zote lakini angalau nakumbuka mbili i.e Waziri mkuu na waziri wa fedha. Sasa unategemea waziri mkuu au waziri wa fedha apige kelele za nini bungeni? Na haya leo tunayaona pia kwa Mramba ambaye akiwa waziri wa fedha amepeleka miradi ya ujenzi wa barabara jimboni kwake pesa ambazo zilitakiwa zitumike kujenga barabara sehemu nyingine. Kwahiyo msiwafananishe wabunge wa kawaida na mawaziri wenye uamuzi wa kupeleka miradi majimbo mwao.
 
Majimbo ya hawa waheshimiwa yakoje?

1. Mgana Msindai (34)
2. William Shellukindo (29)
3. Diana Chilolo (28)
4. Paschal Degera (28)
5. George Lubelege (25)
6. Raphael Mwalyosi (24)
7. Mhoga Ruhwanya (23)
 
Mfano mzuri wa waliochangia na kuzungumza sana bungeni ni pamoja na AMINA CHIFUPA,CHACHA WANGWE,ZITTO ZUBER KABWE,MUDHIHIR M.MUDHIHIR N.K Unafahamu yaliyowakuta?
 
FUYA GODWIN KIMBITA. ambaye jimboni kwake hai ajafanya chochote na bungeni yeye ni wa kuchapa tu ucngizi.amejisahau kwamba ubunge aliupata kwa mbinde sana.
 
haya mambo ya kulazimishana kusema sijui yametokea wapi

Mwakyembe na kelele zake kawapelekea wananchi wa jimbo lake maendeleo gani?
 
Back
Top Bottom