Orodha ya wachezaji 17 waliotemwa simba, orodha ya wachezaji 12 waliosajiliwa simba, orodha ya wachezaji 12 wa kigeni waliosajiliwa simba

Orodha ya wachezaji 17 waliotemwa simba, orodha ya wachezaji 12 waliosajiliwa simba, orodha ya wachezaji 12 wa kigeni waliosajiliwa simba

Ongeza na list ya wachezaji walioitema simba
1. inonga
2. Chama
3.
4.
 
Kabisa, sema ilitakiwa muda kama huu wote wawe kambini, walau miezi 2 wakilwa na mazoezi ya kutosha na mechi za majaribio. Vinginevyo itakuwa tabu tupu.
Imebidi kufanya kutokana na matokeo yalivyo msimu uliopita, hamna namna, uongozi utakuwa umejipanga!
 
Imebidi kufanya kutokana na matokeo yalivyo msimu uliopita, hamna namna, uongozi utakuwa umejipanga!
Nakubaliana nao wanachokifanya, ila maandaliz ya muda mrefu ni mhm kuipa timu uwiano. Tutakuja kuambiwa hapa tuvumilie timu inajengwa. Miaka 3 hii imetosha kuvumilia 😂
 
Wadau hamjamboni nyote?

Pitia takwimu mpya hapo chini:

Wachezaji (17) walioondoka Simba 24 | 25

◉ Aishi Manula (Loan) ›› Azam FC
◉ Feruz (Loan)
◉ David Kameta 'Duchu' (Loan)
◉ Clatous Chama ›› Yanga SC.
◉ Abdallah Hamiss.
◉ Aubin Kramo.
◉ Babakar Sar.
◎ Sadio Kanoute ›› Mazungumzo.
◉ Moses Phiri.
◉ Luis Miquissone.
◉ Pa Omary Jobe.
◉ Willy Esomba Onana.
◉ Hennock Inonga.
◉ Saido Ntibazonkiza.
◉ John Bocco.
◉ Jimmyson Mwanuke.
◉ Shaban Chilunda.
◉ Kennedy Juma.

Wachezaji (12) waliosajiliwa Simba 24 | 25

◉ Lameck Lawi ›› ⚠️
◉ Joshua Mutale.
◉ Steven Mukwala.
◎ Elie Mpanzu 🇨🇩 ›› ⚠️
◉ Jean Charles Ahoua.
◉ Abdulrazack Hamza.
◎ Debora Mavambo.
◉ Augustine Okejepha.
◎ Omary Abdallah Omary.
◎ Valentine Nouma.
◉ Valentino Mashaka.
◎ Chamou Karaboue.

Wachezaji (12) wa kigeni Simba 24 | 25

◉ Ayoub Lakred 🇲🇦
◎ Chamou Karaboue 🇨🇮
◉ Che Fondoh Malone.🇨🇲
◎ Valentine Nouma 🇧🇫
◉ Fabrice Ngoma 🇨🇩
◎ Debora Mavambo 🇨🇬
◉ Augustine Okejepha 🇳🇬
◉ Freddy Michael 🇨🇮
◉ Joshua Mutale 🇿🇲
◉ Steven Mukwala 🇺🇬
◉ Jean Charles Ahoua 🇨🇮
◎ Elie Mpanzu 🇨🇩 ›› ⚠️

Key 🔑
___________________

◉ Waliotambulishwa.
◎ Ambao bado kutambulishwa.

⚠️ Amesajiliwa lakini kuna utata.

Tom Cruz facts 🧠
sijawahi kuwakubali wachezaji wa kinaijeria, naona ni matapeli tu
Augustine Okejepha 🇳🇬...........hapa sio tumepigwa kweli
 
MTOA MADA NAOMBA UKIONA INAKUPENDEZA UTUWEKEE POST/THREAD YA WASIFU WA KILA MCHEZAJI WAKIGEN ALIYESAJILIWA, TO BE HONEST WENGI WETU HATUWAJUI KABISA ANGALAU BASICS MFANO, USHIRIKI WAO WA LIGI ZA KIMATAIFA, GAME TIME, GOALS, NK
INGETUSAIDIA, UNAJUA WENGI WALIOSAJILIWA WA YANGA TUNAWAJUA SANA HADI MADEMU ZAO
NAOMBA KUWASILISHA HOJA
 
Hii timu haijawahi kutengenezwa timu kama hii tnagu dunia iumbwe
 
Mkuu, unakumbuka wachezaji wapya waliosajiliwa Yanga msimu wa 2021-2022 na kuchukua ubingwa? Tena na Kocha akiwa mpya!
Huo Msimu Kocha hakuwa mpya. Nabi aliishakaa na timu tangu Dec 2020, yaani nusu msimu. Na Yanga haikuwa na maingizo 12, illingiza wachezaji wachache Wakongo, na Diara na Aucho.
 
Huwezi kufanya overhaul ya hivi ukawa bingwa wa ligi. Nawaona simba kwenye nafasi ile ile ya msimu ulioisha.
Uko sahihi, nadhani hata wao Simba wanajua hili. Iliwachukua Yanga 5 years kufika hapo kwa mateso na kilio. Ndio maana Simba pia kwakuwa wanajua walikuwa juu, lazima wafanye overhaul kurudi kule.
 
Hata mimi najiuliza sana hili swali, kwa performance gani aliyoionesha Simba mpaka wambakishe?
Simba wamefanya usajili mkubwa sana lakini wamekuja haribu hapa mwishoni kwa kuwabakisha Freddy na Onana. Hapo tu ndio wamefeli kabisa. Kama huyo Onana bonge la mchezaji lakini utoto na ubishoo mwingi unamharibia yaani hayupo "serious" kabisa. Akishafunga goli moja tu la muhimu mechi inayofuata mabega juu na madoido kibao. Kwa Simba hii inayokuja ambayo ina kiu ya mataji huyo Onana haihitajikii

Kwa Fred huyo ndio hata sielewi kamati ya usajili imembakisha kwa nini kwani katika nafasi tano anafunga moja. Sasa kwenye mechi za shirikisho kwenye makundi unakuta mechi nzima nafasi za wazi labda moja au mbili halafu mshambuliaji wako ndio Fred "funga funga" si majanga hayo. Wasiojua mpira wanakuhesabia magoli aliyofunga Zambia wanajumlisha na aliyofunga hapa bongo lakini wanasahau nafasi za wazi alizokosa. Iwapo Freddy angekuwa mshambuliaji anayejua kutumia basi msimu uliopita Simba wangeshika nafasi walau ya pili na wala siyo ya tatu kwani huyo Freddy na mwenzake Jobe waliikosesha Simba magoli kibao ya wazi na kuinyima timu matokeo matokeo yake ikapitwa na Azam
 
Back
Top Bottom