Elections 2015 Orodha ya waliogombana na Magufuli na hatma zao

Makufuli hawezi kuwa raisi wa nchi hii na haita tokea.

Bado siku chache upopo wa kisiasa utabadidilika na dira thabiti ya nani anaenda kuwa raisi wa hii nchi ya Kambarage atakuwa wazi

Mark my ward

Mkuu naona huzifahamu siasa za nchi hii! Watu wanaposema Chama kwanza umaarufu wa mtu baadaye wanakuwa na maana yao. Nakuambia ukiwa ndani ya chama ndio unapata nguvu ukitoka unabaki kuwa kama Samson.

Unaweza ukatoka ukadhani una watu wanakuunga mkono kumbe ghafla wakakutosa. Nina kumbukumbu za Mpendazoe!
 
Kwa hiyo kumkosoa Magufuli ni kutangaza vita!.. Duu!!!!!!! hii tena habari nyingine.

Magufuli ni makali na hataki mchezo wala kucheka yeye ni kazi tu. Hana visasi wala nini ila ukikosea haoni aibu wala hana ajizi atakutosa tu hata kama ni swaiba wake. kwa kifupi hana rafiki wa kujuana ila ana marafiki wa kazi.
 
Nilipigwa BAN kwa kupost bandiko hili la Ocampo Four ... Nauliza? JF imenunuliwa? maana tuliambiwa kuwa kuna Bilioni 150 zimetengwa kwaajili ya kuvuruga mageuzi mwaka huu ... Wadau nisaidieni kujua kuwa nilikosea wapi hadi waniandike eti nilikuwa na kosa la Spamming!!! Grrrrrrrrrrrrrrrrr
 

Wewe unatuletea mambo ya mwaka 47 wakati huu ni mwaka 2015. Unadhani wanadamu ni mawe? Watu wanabadilika kutokana na mazingira na misukumo inayotokea katika maisha yao ya kila siku. Ni nani aliefikiri kwamba ngome tiifu ya ccm monduli ingechafuka kama MKONDO WA ATLANTIC??!
 
Magufuli ni makali na hataki mchezo wala kucheka yeye ni kazi tu. Hana visasi wala nini ila ukikosea haoni aibu wala hana ajizi atakutosa tu hata kama ni swaiba wake. kwa kifupi hana rafiki wa kujuana ila ana marafiki wa kazi.

Kimbunga, je maguguli aliyeelezwa hapa naye unamfahamu?

Magufuli ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza umma wa watu katika kulipa visasi. Kwa wasiomjua, mh. Magufuli alipata kugombea ubunge Jimbo la Biharamulo mara mbili bila kupita. Mara zote aliangushwa na kina marehemu Phares Kabuye kwa kura nyingi sana. Aliweza kupata ubunge pale tu wilaya ya Biharamulo ilipogawanywa na kuwa majimbo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo Mashariki. Hivyo akafanikiwa kuingia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo Mashariki wakati upande wa Biharamulo Magharibi akiwa Mh. Choya.

Baada ya kupata ubunge aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuli alipata unaibu waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na kwa influence miradi yote mikubwa ya wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri. Watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote. Kama mnakumbuka vizuri alifikia kugombana na mbunge mwenzake wa Mashariki aliyefikia kusema kama Magufuli anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilichomuudhi sana Magufuli na kuhakikisha na kufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi. Alifikia kuwa analeta wageni wa kitaifa direct jimboni kwake hata bila kupitia makao makuu ya wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua Biharamulo Magharibi kwa kumnyima ubunge mara ya pili. Hapa nataka kuwaonyesha kuwa kiongozi huyu mcheshi na mchapa kazi ni mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee, wanawake na watoto.

Je, mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form. Mpokea form alijificha na alijitokeza wakati muda wa kurudisha form umekwisha, akaonekana mrudisha form amerudisha too late. Lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali wilayani Biharamulo kuwa atakaepokea form za bwana huyo basi yeye ni naibu waziri atahakikisha hana kazi. Watu wakatii na wakafanya dhuluma ya kumpitisha Magufuli bila kupingwa. Je, mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka 2005 kijana mdogo (nahifadhi jina lake) kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF wilayani Biharamulo alichukua form kugombea jimbo la Biharamulo Mashariki kwa Magufuli huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho. Alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi Mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere. Walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mume wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana. Alipofika Mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa. Kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench mh. waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam. Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli. Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa. Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa. Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindishia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambalo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa Magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihula takribani miwili, alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuharasi uongozi wa wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye halmashauri za wilaya migodi ilipo alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato. Huyu ndiye Mh. Magufuli, je rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

Iliposhindikana akiwa waziri wa ardhi Mh. Magufuli kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama waziri wa ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya wilaya ya Chato hivyo siku si nyingi Chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapora haki ya wana Biharamulo. Swala hili lipo wazi kabisa halmashauri ya wilaya kupitia baraza la madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa Magufuli. Huyu ndiyo mtu anaweza kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Mwaka jana katika mpaka mwingine wa Biharamulo na Chato kijiji cha Biharamulo kinachopakana na Chato huko kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo. Mh. Magufuli yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie wilayani Chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye. Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa rais. Rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya Magufuli ni mengi kuliko mafanikio. Mtakumbuka kilio cha nyumba za serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango kktk ujenzi lakini yote tisa kumi mh. anajenga ghorofa pale kwake anapoishi Osterbay. Nendeni mkaone maajabu ya Mussa, wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni vibarua mchundo, huyu ndiyo Mh. Magufuli.

Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yalioidhinishwa na serikali bila hata serikali kujua kuzipeleka Chato. Hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu. Waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa wilaya ya Biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya mtu namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa

Huko jimboni kwake wafanyakazi wa serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye. Kwa ufupi hajawahi kupita bila kupingwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

Naomba kuwasilisha ili tumpime kwa pamoja. Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

====================================== Zaidi ===================================

Ninakubaliana na wewe kwa asilimia nyingi. Magufuli hajawahi ku inspire watu wakajituma kufanya alichotaka wafanye kwa vile wanapenda.
Hakuna sehemu ameacha sustainable changes in working culture.
Hajawahi kuunda team ikasimama naye zaidi ya watu kufanya kazi kwa woga na unafiki.
Kila sehemu alipokuwa akiondoka mahali, aliyokuwa anayaasisi yalikufa mara moja.

Sasa hapa ni jumla ya masuala mawili. Hulka yake, udhaifu katika uongozi, kukosa uwezo wa kidiplomasia pamoja na kiburi, ubeberu, na failure za chama chake ambazo zimeshindwa kujenga nidhamu za kazi na kusimamia uwajibikaji wa viwango.

Yeye kama Magufuli uongozi hawezi hasa linapokuja suala la maamuzi, mahusiano na raslimali watu, ukiachana na nia zake binafsi. Chama kinachompeleka ni kile kile klichokumbaitia mauti ya Watanzania kiasi cha kushindwa katika kila hali ikiwemo uundaji na usimamizi wa serikali. Mafisadi, wazembe, wadanganyifu, malaghai, mauaji, madhurumati, majizi n.k ndiyo yale yale yamekaa mkao wa kula yanasubiri ashinde, ayateue kuunda serikali na kufanya nayo kazi.
Hapa ni nini kama si mauti kwa taifa?
 
Huyo kijana hakuwa mgombea ubunge bali msaka tonge. Mkuu unataka kusema Biharamulo haina barabara ya Lami?
 


Umeandika ukweli 100% wala hujamuonea mtu. Tatizo la magufuli siyo kiongozi ni mnyampara. Mnyampara has knowledge, a little bit of understanding but completrely Zero wisdom. Wisdom is the ability to use knowledge and understanding to consistently make good decisons. How many good decisions has the guy made in his ministrial posts?
 
Khaa!! Tiifu kwa nani? Hilo lenye sura ya kibaguzi??.Na hilo kimahesabu linazidi kumjenga tingatinga
 
Khaa!! Na tulipofikia sasa kwa nchi yetu tunahitaji kiongozi wa namna hiyo 100% ili irudi kwenye msitari! Btw ungeeandika kiswahili ingekaa poa zaidi
 
nakumbusha tuliko toka
 
Makufuli hawezi kuwa raisi wa nchi hii na haita tokea.

Bado siku chache upopo wa kisiasa utabadidilika na dira thabiti ya nani anaenda kuwa raisi wa hii nchi ya Kambarage atakuwa wazi

Mark my ward
Hahahahahahaaaaaaa
 
Iweje hiyo hatma?
 
Mhh haya ngoja tuone ukweli wa thread yenu hii. So far tathmini ikoje?
 
naendelea kupita tuu
 
Magufuli ni makali na hataki mchezo wala kucheka yeye ni kazi tu. Hana visasi wala nini ila ukikosea haoni aibu wala hana ajizi atakutosa tu hata kama ni swaiba wake. kwa kifupi hana rafiki wa kujuana ila ana marafiki wa kazi.
Kazi gani wewe, acha kumpamba mtu. Kazi kumzidi nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…