1. DIAMOND PLATNUMZ - CEO wa wasafi fm na tv + label, msanii pekee mwenye msururu wa ndinga za kwenda mbele
View attachment 2908478
2. MR NICE - Ni Diamond pekee ndie alieweza kumfikia ukwasi akiwa peak, miaka hio ya 2003 inasemekana alikuwa anamiliki ukwasi wa bilioni 1 ya enzi hizo
View attachment 2908479
3. AY - Mzee wa commercial alikuwa kawaida kiuchumi kwa upande wa muziki ila alijiongeza kutumia pesa alizopata kwenye muziki kufanya investments kadhaa kujiongezea kipato, yupo low key anafanya mambo yake kimya kimya, Kuna kesi yeye na FA walilipwa fidia ya bilioni 2.1 na Tigo, inakadiriwa kila moja aliondoka na milioni 800 baada ya gharama za wanasheria na asante za wazito waliotoa misaada yao (wazee wa mgao), lakini hata bila hii kesi AY alikuwa vizuri kiuchumi, aliwahi kuwa msanii wa kwanza kushoot video ya milioni 50 hata kabla ya hizo fidia.
View attachment 2908482
4. PROFESSOR JAY - Jifunze, ona, sema, elimika, pitia, hamasika... Joseph a.k.a Professor Jay, inasemekana mwamba huyu alikwa analipia kazi zake, alikataa unyonyaji wa album zake kuwa chini ya label, kama ni maokoto mshua huyu kayapiga, miaka hiyo 2004 analipwa milioni 400 advance ya kuuza nakala zake, hio ni kama bilioni ya sasa.
View attachment 2908480
5. ALI KIBA - akiwa kijana mdogo kabisa alishaanza kushika milioni 200 enzi za muhindi wa GMC, yeye anakwambia ziliisha zote kisa "utoto", lakini haikuwa mwisho wa safari yake, huyu ni msanii ambae yupo kwenye game kitambo sana japo kuna kipindi huwa anapoa sana
View attachment 2908481
6. MWANA FA - Ni kesi ya Tigo waliyopewa fidia ya bilioni 2 yeye na AY ndio imemweka kwenye hii orodha, kila moja wao yasemekana aliondoka na milioni 800 baada ya gharama za mawakili na asante za mnyororo wa watu wazito waliowasaidia kwa namna moja ama nyingine (wazee wa mgao)
View attachment 2908576
7. LADY JAY DEE - Binti machozi kautendea haki mziki wetu wa bongo nao mziki ukambarikia mafanikio makubwa,
View attachment 2908483
8. JUMA NATURE - Kwa album zake alizotoa zilizohit hata namba hii pengine haimfai, nadhani alikosa tu usimamizi mzuri wa kusimamia mapato ya kazi zake, mziki wake uliwafaidisha zaidi wengine lakini hata kwa alichoambulia ilikuwa pesa ndefu.
View attachment 2908484
BONUS kutoka Bongo Gospel
ROSE MUHANDO - Tatizo ni mashetani yaliyomo kwenye music industry lakini huyu mama ilibidi awe juu sana, katimila sana kutajirisha wengine, pengine kaambulia 20 % ya mafanikio yake
View attachment 2908588