Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Lakini tizama wanaokuunga mkono na wanaokupinga kwenye suala la Sugu ni wapi wengi. Hii hoja ya Sugu nilishaiona mara kadhaa. Ila nilichokuja kugundua ni kuwa watu wanaompinga hawapendi flow yake. Sasa rap ni flow pekee.? Ni kweli Sugu kakosa zaidi ya nusu ya vinavyohitajika katika ubora mpaka useme ni mweupe.?

Nafikiri ulipaswa kutuaminisha zaidi kwa sababu zenye nguvu kuliko ulizoandika. Watu wamekutajia nyimbo zenye ujumbe, ukongwe wake kwenye tasnia, na impact yake kwa waliomfuatia. Ukisema hana flow nzuri tu ilhali watu kibao walielewa mangoma lazima watu wahoji.

Hivi ni kweli Sugu angekuwa mbovu kwa kiasi unachosema angepata airtime na ustaa mkubwa nyakati zile ambazo radio zilikuwa chache, muda wa ngoma kupigwa ulikuwa mdogo, imani haikua kwa mashabiki, hakukua na njia nyingine za nyimbo kusikilizika na kuonekana, foleni kwa producers n.k, n.k,..?

Pamoja na yote hayo bado Sugu alikuwepo na kusimama kuwa Sugu. Wanasema Biggie alikuwa na flow na punch kali kuliko Pac ila ni wangapi utaweza kuwaaminisha kuwa Pac hakuwa bora kisa hana flow na punch kali kama Biggie ? Nazungumzia ubora mkuu..

Hakuna kitu kibovu kinachodumu kwa muda mrefu mkuu. Vibovu hujitenga mapema sana. Jiulize kwanini kwenye wengi umeungwa mkono ila kwa kwa Sugu umepingwa zaidi.

Ila ni mawazo yako tu ndugu.
 
Heee kumbe sugu alishawahi lalamika anabaniwa??
Kuhusu antivirus sugu aliingia mwishoni kusapoti ila wenye antivirus yao waanzilishi ni mapacha
 
Kuna mawazo ni ya kijinga tu. Kama yale ya kusema mkojo ni dawa ya Ukimwi.
 
Huyu ata 50 cent au Nas atasema hawana vipaji kwa ajili hawana hits sasa hivi. Mziki unachange na kila mtu na wakati wake anashindwa kuelewa
 
Hizo ngoma zote ni before 2010

Niambiea kuanzia 2011 kutoa hit song gan kama solo project
Hujulikana hasa unataka nini! Mara useme hawana vipaji mara uchague miaka unayotaka wewe! Unaji_contradict tu.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hata hawa nliowataja wote walitoka kipindi ambacho kwanza wasanii walikua wachache ilikua ukitoa ngoma lazima iende redioni
Sio kweli. Hawa wametoka kipindi ambacho BongoFleva imeshakubalika baada ya nguvu kubwa ya wasanii wa mwanzo unaodai hawana vipaji. Kipindi ambacho Radio Ststions za FM zimetapakaa kama Uyoga nchi nzima.
 
Umemaliza kila kitu,kwa kifupi uzuri wa nyimbo inategea umeupokea kwa angle ipi.
 
Umemaliza kila kitu,kwa kifupi uzuri wa nyimbo inategea umeupokea kwa angle ipi
 
Nimezaliwa 1994/, nimeanza kuskiliza bongo fleva 1999 so nna experience kubwa sana
Sikuwa nimeona hapa mkuu.. Hapa umemaliza kila kitu. Nafikiri bado unapaswa kuusikiliza ukwaju wa kitambo kwa kina zaidi ndio uje kuandika uliyoandika mkuu.

Ndio maana sikushangaa ulivyomjibu mtu kuwa ipo siku G Nako atafananiswa na Juma kisa tu wingi wa chorus.

Pale nilisikitika sana na si kushangazwa.
 
boss wangu huna unalolijua kaa sikiliza mziki natamaan ukae umsikilize sugu kwa makin nimescreenshot my playlistView attachment 2582478
12_600_lettres imo, aisee una taste nzuri sana ya muziki. Kuna watu ukiwa unasikiliza miziki wao wasioielewa wanakushangaa. Wanaona huyu vipi huyu. Wanasahau muziki ni universal language. Unaweza sikiliza mpaka bhangra ya mhindi kama umeielewa.
 
Umemuelewesha vizuri sana mkuu. Kama mtu hukielewi kitu huna haki ya kusema si bora kabisa ilhali kile kitu kinatumika na watu wenye akili timamu na kimejitengeneza ma kuwepo kwa miaka mingi.

Wapo watu wenye flow kali zaidi ya Sugu na hilo halipingwi. Lakini Sugu kutokuwa na flow nzuri na mengineyo hakuhalalishi eti kuwa hana kipaji. Jamaa angesema yeye binafsi hamuelewi ingekuwa sawa. Ila kusimamia kuwa Sugu ni mweupe tu si sawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…