Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah we jamaa uko deep sana , thank you
 
“Sugu kama angekua na uwezo basi huo uwezo tungeuona kwa kubaki kwenye mainstream kwa muda mrefu”

Kwa hii point yako Ina maana watu kama Dola Soul na Pig black hawana uwezo kwa sababu tu hawakubaki mainstream kwa muda mrefu?
Dola soul na pig black washaachana na maswala ya muziki kitambo .

Sugu mpaka leo anafanya ngoma yake ya mwisho kutoa inaitwa Mtiti kafanya na stara thomas
 
Hayo maoni yako...lakini ukweli ni kwamba hana uwezo wowote ni msanii wakawaida
 
Kufanya tu mashairi yanayoeleweka kwa watu kirahisi na hiyo choice of topics hiyo nayo ni kipaji.
UKirudia kusoma nilichoandika nakubaliana na wewe ana kipaji, ila sio kama wasanii wengine Fid, FA, etc japo alianza kufanya mziki mapema ila kipaji chake ni cha kawaida.
Ugumu wa mashairi au mashairi ya kuungaunga yasiyo direct sidhani ndio kunafanya uwe msanii bora.
Ni kweli kama yupo msanii anayefanya hivyo hatokuwa bora, lakini msanii mzuri sio yule anayeandika mashairi kama kijana wa form three no "punchlines " at all. Wordplay ni muhimu hii ni sifa ya msanii mzuri.
Kama watu wanam_rate higher wewe mtu mmoja unawaona wao hawajui muziki na wewe ndio unajua!?
Ni mjadala huru, sidhani kama tukijadili ujuzi wangu wa mziki au kutokujua in relation na hao watu wanao mrate itasaidia kitu........

Napokea hoja, Why unadhani SUGU ni msanii mzuri kama inavyozungumzwa?
 
Dola soul na pig black washaachana na maswala ya muziki kitambo .

Sugu mpaka leo anafanya ngoma yake ya mwisho kutoa inaitwa Mtiti kafanya na stara thomas
Hata Sugu alishamaliza yote kwenye muziki. Unadhani akomae kutafuta Nini?
 
Hata Sugu alishamaliza yote kwenye muziki. Unadhani akomae kutafuta Nini?
Sugu ni yule yule miaka yote hana uwezo kiuandishi wala flow , ukimskiliza sugu wa niko mikononi mwa polisi na huyu wa mtiti unapata test ile ile , sasa ukisema sahv sugu anafanya muziki for fan nashindwa kukuelewa , huko nyuma alipokua ana kaza mbona ana sound the same na sasa
 
Alikopi kwa 2 pac
We kweli hamnazo

Jina la too proud historia yake lilitokana na ushamba wa Sugu mwenyewe , iko hivi sugu kama kawaida yake ni mtu wa majigambo sana tangu zamani, sasa kipindi hiko kuna siku alikua yeye , master jay na Mzungu mmoja walikua somewhere nafkiri coco beach , kama kawaida yake akawa anaendelea na matambo yake basi yule mzungu akamwambia master jay

" Your friend is too proud" Sugu akamwambia master jay hilo jina design kama nimelipenda huku hata akiwa hajui maana yake , ndo master jay akamwambia maana yake na Sugu akaona aishi nalo
Hiyo ndo historia ya too proud ilipoanzia

Ila yeye akaamua kujiita Mr two proud ...baadaye akaamua abaki na Mr two mpaka yalipokuja majina mengine
 
Uwasilishaji wake ni wakawaida mnoo mtu yoyote anafanya
Hip hop ya zamani utashi ulikua mdgo sana wachache kma wakina prof jize,jaymoe,fid q ndo walikua na utashi mkubwa kulinganisha wengine ila hip hop inabadilika kulingana na wakat pia teknolojia
Mshua Fa hana kipaji???
Ko sugu ana majina mangapi🤣🤣 ananichanganya sana😅😅
 
Tuanze na

Too proud
Mr two
Sugu
Jongwe
Taita

Na mengine ambayo siyafahamu
 
Nimesema kina FA wanakipaji kuliko SUGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…