Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Shida ni kwamba vijana wa siku hizi wanadhania kila kitu bora ni kile kinatokea kwenye era yao

Nilicheka sana nikataka nimjibu lakini nikampotezea eti jina la 2 proud limetokana na mzungu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Fatilia utajua huu ukweli ambao malimbukeni wengi km nyie hamuujui
 

Nilikua naiangalia list ya Billboards/VIBE ya Rapa bora 50 wa muda wote(simaanishi kama wako perfect)
Wangekua wanatumia vigezo kama vyako rapa wengi sana wa kitambo wasinge ingia
Tatizo letu hatuna utaratibu mzuri wa kuweka rekodi zetu
Leo hii ukimwambia mtu wa kizazi kipya hakuna na hajatokea rapa Tz aliyewahi kuvuma na kutingisha kama Juma nature watakukatalia kwasababu hakuna rekodi mahali zinaonyesha hivyo

Kulinganisha uandishi wa Jongwe na Vina au Fif Q au FA au wakina Nikki utakua unamuonea sana
Maarifa hayakua makubwa kama walionayo wakina Vina
Ukitaka kujua ubora wa Hongwe akiwa kwenye peak yake basi mlinganishe na aliokua nao kipindi hicho

Kuna majina kwenye 50 GOAT ya Billboards hata huyajui lakini ukiwa google utaona walifanya makubwa enzi zao tena wakiwa kama waandishi mahiri lakini ukiaja kulinganisha uandishi wao na labda J cole, Big sean utaona wameachwa mbali

So kwa era ya akina Jongwe jamaa alikua anakipaji kikubwa sana tu
 
Mkuu.....
Since Hip hop ni mziki wa mapokeo, asili yake sio hapa. Tunapokea ready "evolved" kwahiyo suala la "evolution" ya mziki linakwenda sambamba na mziki wa US umefika wapi.
Nimesikiliza album ya SUGU "Ni mimi " najua umeiskiliza pia, kwa ambaye hajaiskiliza aende Spotify ipo pia. Hii album ni ya 1995.
By 1995 hiphop ilikuwa katika level gani? Nadhani ndio katika peak yake.

,mfano Inayosadikika kuwa ni Album bora ya mda wote "Illmatic" ilikuwa tayari ina mwaka kabisa.
Je tuseme Ngoma zinazohit US zilikuwa hazijaskika bado bongo? Sugu alikuwa hajaziskia? Mbona beat zake zilikuwa kali tu?

Hoja yako ningeielewa kama Hiphop ingekuwa imeanzia Bongo, so wao ndio wanapambana kuikuza.
Hoja ya uchanga wa hiphop ( uchache wa maarifa) inakuwa applied kwa kina LL cool J kwa kuwa wao ndio waliokuwa wanaanza. No where to refer to, au tuseme hakuna aliyefanya better.

Pia uchache wa maarifa ungeeleweka kama Msanii husika angekuwa anakua na Muziki.
Lakini haipo kivyo kwa Mr II, mziki ulienda unakua lakini yeye akabaki hivyo hivyo.
Hili inaonesha kuwa tatizo sio la uhaba wa maarifa ila tatizo lake binafsi.
Lakini ukimsikiliza Sugu wa kwenye "Ni mimi_1995" na Sugu wa kwenye "Sugu_2004" ni yule yule hakuna kilichobadilika.
Tofauti na walioface tatizo la uchache wa maarifa kweli, ntamtumia LL cool J
LL wa kwenye "radio" sio LL wa kwenye "The definition_ 2004"
 
Hili ndo jawabu lake
Me naujua muziki vizuri , na nna uwezo wa kutambua msanii flan ni mkali au ni wa hovyo kupitia ngoma zake hata mbili tuu
 
Msanii mwanamuziki mzuri ni kufanya kazi nzuri nyingi zenye ushawishi tena kwa muda mrefu (miaka mingi). Huwezi last kwenye game kama muziki wako haukubaliki. Huwezi. Utapotea. Hilo Sugu kathibitisha.

Unaweza ona hata ile album ya Millenia(2000) imetoka tayari Sugu hana tena ile njaa ya 1994/95 lakini ina mawe kibao yenye akili. Huwezi sema huyo mtu anaotea (hana kipaji ya hiko anachofanya), huo utakuwa ni unafiki.
 
Profesa Jay wa "Bongo Dsm"na huyu wa "kipi sijasikia" ana taste tofauti!?
 
Vigezo vikiwa vingi against wewe ndipo watu wanahitimisha kuwa kipaji chako ni kidogo.
Kipaji kidogo au hana kipaji.!? Mtoa mada hajasema kuhusu "kipaji kidogo" lakini!
 
Ninachojua mtoto bwabwa Mchelemchele huwezi kuona vipaji vya hao watu
 
Umefunga mjadala Mkuu.
 
Tunaweza kujadilia bila kutumia lugha za kuudhi mkuu

We’re just doing it for fun...... no hard feelings

Relax mkuu
Huyu jamaa kuna majina ya dharau ameyatumia sana kuwaita watu humu. Na mimi nimeenda naye hivyo hivyo anavyotaka. Actually ni MPUMBAVU flani hiiivi. Maana haiingii akilini kuwakosoa wadau wengine kwa lugha za kukera.
 
Sugu yupi? huyu wa Mikononi mwa police, Chini ya 18, Hayakua maepenzi, mambo ya fedha, Dar, moto chini,?
 
Huwezi kuwa serious Aisee! Naona kabisa wewe ndio huna sikio la muziki.
Unataka kusema prof jay chemshabongo ndo huyo huyo wa Hapo vp hapo sawa?

Hauko serious mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…