Soggy Doggy hunter? Ameonewa, kibanda cha simu pamoja na story ya soggy ni ngoma zinazothibitisha ubora wake!
Kala Pina a.k.a Nabii koko? Hapana, mstari wa mbele ni moja kati ya ngoma kali za bongo hip hop za muda wote!
Mike T mnyalu? Inawezekana style yake haikukuvutia. Mike T wa "je utanipenda" na "hata kama Mnyalu" huwezi kumuweka kwenye kundi la watu wasio na vipaji.
Sugu? Pengine flow yake haikukuvutia, ila mafanikio yote aliyonayo, chimbuko lake ni mziki alioufanya. Sugu ndio mtu wa kwanza kuanzisha vita na mainstream media (chini ya Ruge) na akasurvive. Wa pili ni Lady Jaydee a.k.a Komando!
Jaffarai na Temba, sijawahi kuvutiwa na muziki wao kabisa. Ila wanazo hit songs, na mashabiki wengi waliwakubali. Siwezo kusema hawana vipaji.
DUDU BAYA a.k.a KONKI MASTA! Hapa mzee nimekosa cha kutetea. Mimi binafsi, mpaka leo sijaweza kuelewa kama dudu baya alikua anaimba au anarap. Maana kama ni kuimba, basi mwamba yuko na sauti mbaya. Na kama ni kurap, basi jamaa hajui nini maana ya vina.
Shilole a.k.a Shishi Trump. Kuna vitu vimempa umaarufu, sio muziki. Hata yeye anajua huku kwenye muziki anafosi tu. Kuna Shishi, Amber Lulu na Giggy money, wako kundi moja japo Giggy kidogo yuko na nafuu!
Nilitaka kusema kitu kuhusu AY, ila ngoja niishie hapa!