Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Ni Maajabu watu waimbe Nchi nzima tuwasikie na kuwaelewa halafu aseme hawana Kipaji sijui nini.... Tena Enzi ambazo hakukua na Digital platforms kama sasa.
 
Hahaha sister alizingua pakubwa sana, yaani KCC inarekodiwa akina Mama Muyaone! Haikiwa haki kabisa.
 
Mtoa mada ni moja ya wapumbavu wachache wanao jiona wajuaji,kwanza hawajui wasanii na sanaa yenyewe ilivyo,siku za nyuma mziki ulikuwa mgumu sana tofauti na sasa.

Mr 2 sio mtu wa kumkebehi hata kidogo katika tasinia ya muziki
 
Mtoa mada ni moja ya wapumbavu wachache wanao jiona wajuaji,kwanza hawajui wasanii na sanaa yenyewe ilivyo,siku za nyuma mziki ulikuwa mgumu sana tofauti na sasa.

Mr 2 sio mtu wa kumkebehi hata kidogo katika tasinia ya muziki
Oya jiheshimu , mpumbavu ni wewe unayejibu kimhemko
 
Umemuacha KI THE THE
 
Soggy Doggy hunter? Ameonewa, kibanda cha simu pamoja na story ya soggy ni ngoma zinazothibitisha ubora wake!

Kala Pina a.k.a Nabii koko? Hapana, mstari wa mbele ni moja kati ya ngoma kali za bongo hip hop za muda wote!

Mike T mnyalu? Inawezekana style yake haikukuvutia. Mike T wa "je utanipenda" na "hata kama Mnyalu" huwezi kumuweka kwenye kundi la watu wasio na vipaji.

Sugu? Pengine flow yake haikukuvutia, ila mafanikio yote aliyonayo, chimbuko lake ni mziki alioufanya. Sugu ndio mtu wa kwanza kuanzisha vita na mainstream media (chini ya Ruge) na akasurvive. Wa pili ni Lady Jaydee a.k.a Komando!

Jaffarai na Temba, sijawahi kuvutiwa na muziki wao kabisa. Ila wanazo hit songs, na mashabiki wengi waliwakubali. Siwezo kusema hawana vipaji.

DUDU BAYA a.k.a KONKI MASTA! Hapa mzee nimekosa cha kutetea. Mimi binafsi, mpaka leo sijaweza kuelewa kama dudu baya alikua anaimba au anarap. Maana kama ni kuimba, basi mwamba yuko na sauti mbaya. Na kama ni kurap, basi jamaa hajui nini maana ya vina.

Shilole a.k.a Shishi Trump. Kuna vitu vimempa umaarufu, sio muziki. Hata yeye anajua huku kwenye muziki anafosi tu. Kuna Shishi, Amber Lulu na Giggy money, wako kundi moja japo Giggy kidogo yuko na nafuu!

Nilitaka kusema kitu kuhusu AY, ila ngoja niishie hapa!
 
Yaani ukisikiliza sintobadilika..utajua mtoa mada kazingua kwa mnyalu
 
Kila mtu ana taste yake..hapo kwa AY na Mimi simkubali Sana.. lakini siwezi kusema Hana kibaji wakati anangoma nyingi zilivuma Sana..Kama Zigo..Leo..n.k
 
Jamaa kwa harakati za music tunampa heshima yake .lakini tukibaki kwenye ukweli ni kuwa hana kipaji cha music..
Ndo maana hajapewa heshima ya Godfather wa bongo fleva ila proffessor jay kapewa
Ukweli mchungu ,japo anapambana sana
 
Mkuu kuhusu AY hebu funguka kidogo
 
Nimecheka huyo namba 3 [emoji16] [emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…