Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

nilidhani unazungumzia wasanii wanao trend kwa sasa,kumbe unazungumzia zilipendwa
 
Mtoa mada hayuko mbali na ukweli, kama una internal talent utakuwa kuwa ubauwezo wa kubadilika ktk msimu na kujua nn kinahitajika kipindi hicho, mfano rahisi koffy Olomide anasema hata kama wanamziki wake wakiondoka wote akabaki peke yake bado hawatamshinda. and u can see it's true. He is real talented musician.
Thank you brother [emoji110]
 
Swali la kitoto sana
Uzi wako ungekuwa na maana kama unge dadavua, japo kwa uchache unaelewa nini kuhusu kipaji,

Then, kwa jinsi ambavyo ungeeleza huu uzi wako ungekuwa kama hitimisho tu, kwamba kutokana na maana hii ya neno "kipaji" wasanii wafuatao hawa fit
 
Kiukweli temba hana kipaji kabisa. Nyimbo zake alikuwa anaongea ongea tu maneno hovyo na wimbo wake uliompa umaarufu zaidi nd aliongea pumba vibaya mno( ule nampenda yeye). Lakini pia nyimbo we nd mchizi wangu remix yeye alionekana kabisa kuwa sio rapper tofauti na wenzie.
Kuna uwezekano mkubwa ukawa hujuii vizurii kuhusu temba.....

Anzia kule monduli mobb....

Unajuaa kwann alijiitaa mh Temba, unamjuaa bwana mkubwa....

Unaujuaa wimbo unaitwaa nini kutuzimia...
Nakumindi
 
Kalapina,

Huyu jamaa mbali na kuwa na harakati nyingi akiwa pamoja na kundi lake la Kikosi cha mizinga .ukweli ni kwamba hana kipaji cha music. Alipata umaarufu coz ametoka kipindi wasanii ni wachache

Sugu

Huyu jamaa ana majina kibao kama Mr two, jongwe, too proud na sasa anajiita Taita licha ya kuwa na heshima kama moja ya waasisi wa music wa hiphop tanzania , ukweli ni kwamba hana kipaji cha music

Jaffarai

Huyu ni moja ya member wa wateule alitamba na wimbo wa niko bize .lakini hakuweza kudumu kwenye game kwa muda mrefu kutokana ukweli hana kipaji

Mchizi mox

Huyu pia ni member mwingine wa wateule ngoma zake zilizowahi kupata airtime ni mambo vp na chupa nyingine . lakini uwezo wake ni wa kawaida sana

Mike tee mnyalu

Huyu jamaa alipata airtime miaka ya zamani kwa ngoma zake lakini ukimskiliza ni wazi hana uwezo kabisa. Ni moja kati ya wasanii ambao huwa wanaandikiwa

Soggydog hunter

Huyu jamaa bora angebaki kwenye u presenter tuu huku kwenye music aliforce tuu hana uwezo kabisa ana ngoma nyingi ila iliyopenya ni kibanda cha simu pekee yake

Bou nako

Huyu alikua member wa N2N lakini tangu hakua na uwezo kabisa .nafkir wana walimbeba tuu kutokana na love .ila kwenye music jamaa hana kipaji

Kr mulah

Huyu ndio founder wa style ya kucheza Mapanga . ameanza sanaa muda mrefu sana lakini ukimskiliza utagundua jamaa hana uwezo wowote kwenye music kwa kifupi hana kipaji

Mh temba

Huyu ni member wa TMK wanaume family mwanzoni alibahatisha ngoma kama tatu zikaenda mjini, baadaye akaja kuungana na chege wakatoa hadi album..ila ukimfuatilia vizur jamaa hana
uwezo kabisa

Rich one

Huyu pia ni member wa TMK alitamba na ngoma moja aliyomshirikisha Juma nature inaitwa hatuna kitu.baada ya hapo hajawai kutoa hitsong tena, Jamaa anasifika kwa utapeli wa kuandaa show na wasanii fake huko mkoani afu anapiga hela

Dudu baya

Huyu jamaa aliotea ngoma kama tatu tuu ambazo zilimtambulisha vyema kwenye game .lakini alipata jina kwakua kipindi anatoka hapakua na upinzani mkali kama ilivyo sasa

Maujanja suppliers

Hawa jamaa nawakubali kwa harakati zao za street lakini kwenye music watupishe hawana vipaji .lakini wao wamekua wanalalamika wanabaniwa kitu ambacho sio ukweli

Kama unafuatilia music wa bongo fleva utakua unakubaliana na mimi hawa jamaa hawana talent za music kabisa
Nakubaliana na wewe kwa Kr Mullah.

Mwingine Enock Bela
 
Wapo wengi sana
1-Benjamin wa mambo jambo
2-Bwana misosi
3-pingu na denso
4-dark master
5-kali p
6-mrisho mpoto
7-chege
8-shilole
9-baba levo
10-masawe mtata
11-H baba
12-harmo rapa
13-queen darline
14-crazy gk
15-bonge la nyau
16-baby madaha
17-snura
18-top c
Aisee list ni ndefu
nimegundua watu wengi hamjui muziki, yaani ni watu wa upepo tu
 
Ongeza na jamaa mmoja anaitwa Wakazi. Huyu nimekuja kujua kwamba ni msanii baada ya kuingia Twitter. Pamoja na hvho bado sijua wimbi wake hata mmoja.

Halaf kuna weusi. Hao jamaa huwa wanaimba vitu ili mradi tu wapate vina lkn aaid ya hapo hakuna kitu
kama unaufatilia mziki vizuri basi wakazi ungemjua, shida yake tu anataka kufanya kama bado yupo marekani
 
Back
Top Bottom