Mkuu.....
Since Hip hop ni mziki wa mapokeo, asili yake sio hapa. Tunapokea ready "evolved" kwahiyo suala la "evolution" ya mziki linakwenda sambamba na mziki wa US umefika wapi.
Nimesikiliza album ya SUGU "Ni mimi " najua umeiskiliza pia, kwa ambaye hajaiskiliza aende Spotify ipo pia. Hii album ni ya 1995.
By 1995 hiphop ilikuwa katika level gani? Nadhani ndio katika peak yake.
,mfano Inayosadikika kuwa ni Album bora ya mda wote "Illmatic" ilikuwa tayari ina mwaka kabisa.
Je tuseme Ngoma zinazohit US zilikuwa hazijaskika bado bongo? Sugu alikuwa hajaziskia? Mbona beat zake zilikuwa kali tu?
Hoja yako ningeielewa kama Hiphop ingekuwa imeanzia Bongo, so wao ndio wanapambana kuikuza.
Hoja ya uchanga wa hiphop ( uchache wa maarifa) inakuwa applied kwa kina LL cool J kwa kuwa wao ndio waliokuwa wanaanza. No where to refer to, au tuseme hakuna aliyefanya better.
Pia uchache wa maarifa ungeeleweka kama Msanii husika angekuwa anakua na Muziki.
Lakini haipo kivyo kwa Mr II, mziki ulienda unakua lakini yeye akabaki hivyo hivyo.
Hili inaonesha kuwa tatizo sio la uhaba wa maarifa ila tatizo lake binafsi.
Lakini ukimsikiliza Sugu wa kwenye "Ni mimi_1995" na Sugu wa kwenye "Sugu_2004" ni yule yule hakuna kilichobadilika.
Tofauti na walioface tatizo la uchache wa maarifa kweli, ntamtumia LL cool J
LL wa kwenye "radio" sio LL wa kwenye "The definition_ 2004"