Orodha ya Watu ambao hata wakikukosea huwezi kushindwa nao zaidi ya kumuachia Mungu

Orodha ya Watu ambao hata wakikukosea huwezi kushindwa nao zaidi ya kumuachia Mungu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
ORODHA YA WATU AMBAO HATA WAKIKUKOSEA HUWEZI KUSHINDANA NAO ZAIDI YA KUMUACHIA MUNGU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuna watu kwenye hii dunia wamepewa mamlaka makubwa mno. Wanaweza kukufanya Jambo lolote lakini wewe usiwe na chochote cha kuwafanya. Mara nyingi watu hawa unashauriwa uende nao Kwa akili Kwa ajili ya usalama wako.

Ifuatayo ni orodha ya watu ambao hata wakikukosea huna chochote chakuwafanya;

1. Mama na Baba yako
Asije akakudanganya Mtu mama au Baba yako hata wakikukosea huna chochote unachoweza kuwafanya. Namaanisha huwezi shindana nao ukawashinda dunia ingalipo. Mzazi wako hata kama umeona yupo Wrong unachoweza kufanya ni Kucheza na saikolojia yake katika Kupunguza madhara ya kile anachotaka kukifanya.

Mzazi hakaripiwi, Mzazi hapigwi, Mzazi hanyoshewi kidole. Kamwe usinyanyue Mkono wako kumpiga au kumsema vibaya na kumtukana mzazi wako. Hiyo mechi kivyovyote umepigwa tena umepigwa vibaya Mno.

Nafahamu wapo wazazi wapumbavu ambao hutumia nafasi hiyo kuwanyanyasa watoto wao. Namna Bora ya kuwaepuka wazazi wa namna hiyo sio kushindana nao isipokuwa unapaswa uondoke na ukae mbali nao, ikiwezekana nenda mahali ambako hawatajua.

Mzazi anauwezo wa kuharibu maisha yako kama hutotumia akili vizuri ku-deal Naye. Kamwe mtoto hawezi shindana na Mzazi wake akashinda dunia ingalipo. Unaweza muua au mpiga mzazi wako na ukaona hakuna madhara yoyote yanayokutokea lakini kumbuka maisha sio siku moja na maisha yanaendelea.

Ukiona mama na Baba wanapigana au kugombana, kamwe usimpige yeyote Kati Yao. Hata kama umeona yupo mmoja wao anakosea.
Mzazi hapigwi.

2. Mpakwa Mafuta wa Mungu
Hapa tunazungumzia manabii, mitume, makuhani na mtu yeyote mwenye roho wa Mungu. Watu wa hivyo achana nao. Huwezi ukashindana nao ukashinda kivyovyote vile.

Vijana wote waliofunzwa wanafahamu Jambo hili vyema Kabisa. Mtu yeyote mwenye Dalili ya uwepo wa roho wa Mungu sio anayejiita au kujitangaza kuwa anaroho wa Mungu. Nop Bali Kwa matendo yake utamjua tuu.
Mtu Haki, mwenye upendo, anayependa mambo Mema huyo kaa Naye Mbali. Huwezi shindana Naye ukashinda.

Kabla hujapambana na watu wa namna hiyo ni afadhali ukauliza watangulizi wako waliowahi kupambana na wapakwa Mafuta na Mungu nini walikipata au nini wanaendelea kulipa.

3. Mfalme au Rais

Huna lolote utakaloweza fanya endapo mfalme atakukosea. Huwezi shindana Naye ukashinda kivyovyote vile labda uwe kundi Namba mbili hapo yaani Mpakwa Mafuta wa Bwana. Kamwe usipende kujiingiza kwenye Ligi zisizo na maana na makundi hayo matatu hapo juu. Ni hatari sana na uwezekano wa kushinda haupo kivyovyote.

Makundi hayo matatu yenyewe Kwa yenyewe ndio yanaweza kuparangana na mshindi anaweza kupatikana.

Nakutakia maandalizi Mema ya SABATO.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hiyo namba afutatu hatujasahau Mkuu inawezekana kabisa sema tu inategemea we ni nani na sababu bt mengine ni issue ya timing tu.

Mengine hayo siwezi kufanya na Wala sababu ya kufanya Hivyo hakuna.
 
namba 2 haina mantiki zaidi ya kutishana tu. Watu wanauza madawa ya kulevya wamepakwa mafuta ya bangi au? NILISHARE MWANAMKE NA BOYA MMOJA NIKAMTUKANA NA MAFUTA HATA MIMI NIMEPAKWA SANA. Gwajima, masanja, myamba, lusekelo na padri mbakaji walipakwa mafuta yanayonuka.
 
Back
Top Bottom