Mkuu, nakukubalia kwa asilimia fulani na kukukatalia kwa asilimia. Hata iweje, UDSM ndo chuo baba Tanzania, kwa sasa! Kwa lugha nyepesi, ubora wa chuo unapimwa na Idadi ya Pofs, PhDs, na walimu wengi wenye Masters Level na Ukongwe wao katika fani ya kufundisha. Anayebisha kwa hili hana jipya.
Kwa upande mwingine, si kweli kwamba wanafunzi wa waliohitim vyuo vingine ni vilaza. Si wote, na ujue kuwa kuna watu wengi tu wamesoma UDSM lakini wako shallow. Si kila aliyesoma UDSM ni genius. Kwa sasa, unaweza ukawa na Div 1.3 na ukapelekwa UDOM au Mzumbe au IFM! Kwa hiyo dhana ya kuwa UDSM ni kila kitu kwa sasa siyo sahihi! Kwa tulioingia chuo miaka ya 2000 kurudi nyuma, na one zetu tuliende UDSM straight kwa kuwa hakukuwa na mbadala, waliofeli ndo walienda huko IFM, MU, CBE na kwingineko.
Pia, elewa kuwa, UDSM haikuwa mbele na kinara kwa fani zote. Sheria ilikuwa na imetawaliwa na UDSM hii haina ubishi. Kozi za Uhasibu zilitawaliwa sana na IDM na IFM, ndo maana ukiangalia kwa kipindi kile Technical Guys wa NBAA walikuwa wanatoka IFM/IDM-Mzumbe na waliokuwa wamesoma ACCA-UK na Kenya.
Kozi za engineering, kwa dhana ya Utawala, UDSM wako juu sana, lakini kwa dhana ya utendaji, Dar Tech, Mbeya Tech, Arusha Tech walikuwa vinara sana, hata watu amabao walitoka Form Four kwenda vyuo hivi na kupiga FTC na akapata Grade B and above, then kujiunga UDSM walikuwa majembe ya kufa mtu!
Hii topic ni pana sana, lakini ukweli bado ni ule ule kuwa, UDSM is the best University so far in Tanzania!