Orodha ya watu wanaojiona wajanja nchi hii

Orodha ya watu wanaojiona wajanja nchi hii

Wanaokula tunda kimasihara je?
... kuna jamaa alikuja mgeni kitaa akatumia nafasi yake ya ugeni sababu zamani ukiwa mgeni kitaa pisi zinapapatika akala pisi moja kimasihara akaja kujigamba kijiweni kaitafuna kirahisi watu wakamuambia mbona huyo demu kaungua kitambo na anajijua anachofanya saizi ni kusambaza upendo makusudi, alitoa macho kama konokono ujanja wote mfukoni, mwezi tu kaanza kupungua bahati yake alipima akawa hana jambo, akakatisha likizo akaondoka kesho yake baada ya kumaliza kupima na kurudi alipokuwa na mimi nikajifunza ukifika mahali mgeni usikimbilie kula pisi.
 
... kuna jamaa alikuja mgeni kitaa akatumia nafasi yake ya ugeni sababu zamani ukiwa mgeni kitaa pisi zinapapatika akala pisi moja kimasihara akaja kujigamba kijiweni kaitafuna kirahisi watu wakamuambia mbona huyo demu kaungua kitambo na anajijua anachofanya saizi ni kusambaza upendo makusudi, alitoa macho kama konokono ujanja wote mfukoni, mwezi tu kaanza kupungua bahati yake alipima akakuwa hana jambo, akakatisha likizo akaondoka kesho yake kurudi alipokuwa.
Mademu wa vifurushi ni hatari
 
ORODHA YA WATU WANAOJIONA WAJANJA NCHI HII!

Anaandika, Robert Heriel!

Nchi hii inamambo Sana. Leo sina mengi ya kusema, nijikite kwenye Uzi.
Ifuatayo ni orodha ya Watu wanaojiona ni wajanja na Werevu.

1. Wasanii wa Muziki, BongoFleva
Kundi hili ndilo linaongoza Kwa kudhani kuwa wao ndio wajanja, ujanja wao unategemea zaidi Miwani nyeusi, pamba, cheni na mikufu waivaayo, viatu na madundo, N.k.
Ujanja wao unaimarika zaidi na kuwa na nguvu hasa wakiwa mbele ya Kamera😊 Kwani wengi wanakuwa wamejiandaa.
Lakini kundi hili ujanja wao unaisha pale unapokutana nao Live/Mubashara kwani hawaonekani vile wanavyoonekana kwenye Luninga. Na hili wanalijua fika.

Kundi hili linadhani kuwa ni maarufu na kila mtanzania anawajua. Kumbe kuna watu hata Diamond Platinum hawamjui tena wanaishi mjini kabisa😀😀

Ni Vijana wetu tuwapende na kuwasapoti kwani wanatupa burudani.

2. Waigizaji wa Bongomovie
Hawa ni ndugu na kundi la Kwanza. Hawa ujanja wao wanajifikiri na Kujiona ni wazuri au mashalobaro kumbe wengi wao hamna kitu. Wanachotegemea ni Vipodozi, Vijana kujichubua n.k
Ujanja wa kundi hili upo kwenye Luninga Kwa kweli hapo hakuna wakuwasumbua.
Wao mtazamo wao kuonekana tuu kwenye Luninga hiyo tuu inawafanya wajione wajanja.

Hawa ni Vijana ambao wanahitaji sapoti yetu ili waendelee kutupa burudani.

3. Wanachuo wa Chuo kikuu
Kundi hili bhana Lina vituko, wanachuo hasa wanaosoma Udsm hujiona wao ndio wajanja kisa usomi wao.
Ujanja wao zaidi ni wakiwa vyuoni hapo huwaona Watu wote ambao hawasomi kuwa hawajawahi kusoma, alafu wakipita sehemu wanafikiri kila mtu anajua wao ni wasomi kumbe 😂.
Kundi hili linatia huruma pale vyuo vinapofungwa wakarudi nyumbani😀. ..
Wakimaliza Chuo ndio wanatamani wajifiche hasa Kwa wale waliokuwa wanawaringishia.

Hawa ni Vijana wetu bado wanandoto nyingi tuwasaidie kuwapa connection za kazi ili wapunguze wenge

4. Wanajamii Forum.
😂😂😂 kundi hili linachekesha Sana. Kwanza wengi hawajuani kutokana na ID Fake. Kila mmoja anajiona ana Akili kuliko mwenzake. Wenyewe wanajiita Ma-Great Thinker ambao huwadharau watu wa mitandao mingine Hasa Facebook.
Ujanja wao hawa watu upo Ndani ya Jamii Forum tuu, nje ya hapa wengi wao wanayajua maisha Yao.
Mbwembwe za kila mtu msomi, sijui anagari, sijui ananyumba ni humu humu ndani.

Wana JF kutokana na kujiona wajanja sio ajabu kuwaona wakimuona mpaka Rais wa Nchi kuwa ni mtu mdogo au Hana uwezo wowote. Huku IGP au CDF au Mtawala yeyote anaweza kuchezea makofi na michambo alafu huyo anayefanya hivyo ukimtoa JF ukamuona unabaki unacheka tuu.

Kundi hili ni muhimu Kwa sababu linatoa Elimu na hoja kupitia Makala zenye Nondo ambazo hata Chuoni hazipo.

5. Wanawake wanaopaka Makeup na kusuka mitindo au kuvaa mawigi.
Kundi hili 😂😂😂 tena ukute kabandi vikucha vyake😀 Yaani anajiona mjanja wengine wote ni Mbuzi mee.

6. Wanachadema
Kwanza kundi hili ndilo linaamini ndio wao pekee wanaojua nchi hii, wanajua kipi ni halali na kipi sio halali katika nchi hii.
Kundi hili ndilo linajiona wajanja wa kuchambua na mabingwa wa kupambana na ndugu zao WA CCM.

Wanachadema ndio wanaojiona wao ndio wajanja wa Siasa za nchi hii. Wao ndio wanaoijua Siasa za nchi hii.
Ujanja wao unaishaga pale viongozi wao wanapiga U-turn au kubadilisha Gia angani.
Wanachadema wao huwaona watu wengine wajinga hasa wasipowasapoti, wanawaona kana kwamba hawaelewi lolote kuhusu kinachoendelea na kitakachotokea.

7. Wanaume wa Dar.
Hawa wanaamini wao ndio wenye nchi hii. Wanaamini pia kuwa wao ndio wajanja sio kama Watu wa mikoani.
Wanaume wa Dar ujanja wao upo kwenye simu au mitandao ya kijamii.
Lakini ni nadra na ngumu Sana wanaume wa Dar akukaribishe mahali anapoishi. Ni wachache Sana wanaweza fanya hivyo. Hii ni kutokana wengi wao wanaishi maisha yasiyoendana na vile wanavyojitambulisha mbele ya watu. Wana-Fake maisha.
Ujanja wa wanaume wa Dar upo Insta, Facebook, Twitter, na JF. Pia upo Kwenye viwanja vya STAREHE iwe Club, Pub, au Casino. Nyumbani hawatakubali uende labda uwe mzazi wake.

8. Wadangaji
Wanawake wanaokula nauli na pesa za wanaume burebure ni moja ya watu wanaojiona wajanja Sana.

9. Wanaccm
Hawa wao akili zao zinajiona Kama wao ndio wenye nchi. Wao hawanaga kelele sijui blah! Blah! Nyie pigeni kelele wao wanakusubiri kwenye Sanduku la kura, ukiwashinda wakuibie Kura, kwao huo wanauita ujanja. Ujanja wa 2020 ndio uliovunja rekodi.


10. Madalali wa Kariakoo.
Hawa wanajiona wajanja Sana Kwa kuzingira na kudhibiti Maeneo muhimu ya bidhaa, yaani ni ngumu kuwakwepa hawa madalali unapoenda kununua bidhaa pale Kariakoo labda uwe mwenyeji Mjanja. Wao ndio hujigeuza wamiliki wa maduka ukifika kitu cha elfu 20 sio ajabu ukakinunua elfu 35 alafu watajifanya wanakupungizia mpaka 30 au 25.
Ukiondoka wanajiona wajanja kumbe uhuni mtupu.

Hata hivyo ni sehemu ya Ajira kwao.

11. Walokole, Maostadhi na maostadhati.
Hawa hujiona wao ndio wameyapatia maisha. Yaani wao hujiona ndio wajanja Kwa kushika dini. Nyie wengine wanawaona Kama wajinga Fulani mnaopoteza muda wenu.
Ujanja wao ni pale wawapo Makanisani na miskitini au Mazingira yasiyo na purukushani.
Ujanja unaishaga pale Tatizo linalohitaji pesa nyingi wasizo nazo linapotekea.

12. Walevi.
Kundi hili sina haja ya kulieleza.

Kundi gani nimeliacha?
Kundi namba 4 kiongozi wetu ni GENTAMYCINE
 
Back
Top Bottom