Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Konda anakwambia inajaa ndoo ya maji ila gari haijai sogeeni huko😀😀
Hapo umetoka zako kwenye kibarua chako umechoka umevurugwa na boss/wateja halafu konda nae anakuvuruga zaidi... kituoni mnakaa zaidi ya dakika 10 mmebanana kama mkungu wa ndizi, huko nje unamsikia konda anabamiza gari ubavuni '' oya ngoja apande gari bado nyeupe"
 
Na ukimfokea konda anakujibu si ungenunua gari lako kama hutaki public transport au ita uber😀😀 basi tu ili mradi akukere😀
 
True story ilishawahi kunikuta pia mimi, nalazimishwa niende mkesha na hizo sio pigo zangu kabisa, kusimama saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi kesho yake huku mnaimba.. Kuhusu kuokoka aliniambia pia nikamwambia niache tu na imani yangu inanitosha, mmmh kwangu ilikuwa ngumu kumeza
 
Nimecheka mno sana!!

Maafisa kwenye halmashauri zetu njaa tupu lakini wanavojiona sasa acha kabisa!!
Niliwahi kwenda halmashauri moja kufatilia vibali na leseni aisee kuna watu wana nyodo sana, tena umkute kwenye ofisi yenye AC na kapangaboi ka mchongo ndio utaelewa mkuu, sijui wanaonaga pale watakaa mazima

Wanapenda urasimu mwingiii. yaani vile wewe unavyosumbuka ndio furaha yake na anataka umnyenyekee
 
Hiyo no 4. Hawa ma Dr na PhD ndiyo balaa utazani wamesoma ukoo mzima wakati kachomoka yeye tu nfugu zake wengine mambulula tu lakini sasa wanavyo kashifu wengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…