Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Kuna wale wazee "Much Know" yaani wanaamini wanajua kila kitu kwenye huu ulimwengu , alafu hawapendi kuitwa wazee. Ukiwabishia kidogo tu utasikia " Huko shule mlienda kusomea ujinga" hahahaha
Ningekuwa nafanya HiP Hop ningemtaja [emoji23][emoji23][emoji23]

Watu wa aina hii huwa wanazingua..Kwa nini? Kwa sababu wanaamini kile wasemacho wao ni sahihi, hawataki kupingwa na kupokea mtazamo tofauti ni ngumu..

Wangejua kujifunza ni kila siku na ukikubali kwamba hujui kitu fulani haikushushi basi wangekuwa Humble
 
Kuna hawa Ma Secretary wanajikutaga wao ndio boss katika ofisi
Unaenda na issue ya kuonana na boss wake
Anakujibu boss hayupo nieleze mim huku kamebana pua
Utafikir wanaweza kutatua issue uliyoenda nayo
Umepiga mulemule mkuu, hii nakubali kabisa wanakuwaga na nyodo kumbe maisha hawajayamaliza
 
Hahaha namba 16 isingekuepo ningeiongezeaa mkuu..kweli Kuna madereva wa Malory wakishakaa kwenye cabin zile af awe na chuma mpya hujionaga wamefiiiikaaaa..madereva wa ST ndo usiseme
Ongezea na wale wa mabasi ya mkoa.. Chombo kikiwa kipya wanavyokifanyia sifa na mbwembwe
 
Hao interectual arrogant ni pamoja na mchumi namba Moja anayeshauri wabunge waongelee uganga wa kienyeji hayo mambo mengine yamo kwenye mipango Yao ya trap na Nini sijui lakini akiulizwa trap ni Nini anapata kigugumizi hadi ana kaa
 
Hujwahi kukutana na wafanyakazi wa TTCL pale kibo complex ww.
Mtu unafika pale anakuangalia kuanzia juu hadi chini kisha anakuuliza kwa sauti ya usingizini "eeh unasemaje!".
Haki ya nani ile siku nilitukana mtu kum**#ke
Utadhani moyo wa shirika wameushikilia wao kumbe hamna kitu, shirika lenyewe tia maji tia maji linapigwa gap na private
 
Sijasoma yote ila kwa wapata siti za daladala ni uhakika hundred percent
[emoji23][emoji119][emoji23] mkuu ilishakukuta hii


Yaani yule aliyopo kwenye siti anaposhuka sisi tulioshika bomba tunavyomlia timing na kupiga mahesabu kichwani acha tu... Ukikaa tu kwanza unashusha pumzi na kama ni ya dirishani unaweka kishoka kabisa [emoji119][emoji119][emoji119]
 
Back
Top Bottom