Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Orodha ya watu wanaojiona wameyapatia maisha

Hiyo no 4. Hawa ma Dr na PhD ndiyo balaa utazani wamesoma ukoo mzima wakati kachomoka yeye tu nfugu zake wengine mambulula tu lakini sasa wanavyo kashifu wengine!
Hii hulka ya kutaka kupenda misifa sijui wanafundishwaga wapi

mbona kuna Madokta PhD wanatoa madini mazuri tu na hawana mbwembwe
 
Wanaosafiri kwa ndege hasa safari za ndani ya nchi
Hawa nao bwana hatujawaacha nyuma, unakuta kapiga zake kikaptura kifupi, vimiwani vya mchongo, kabegi kadogo ka kuburuta, visendo na visoksi vidogo halafu pembeni yuko na neck pillow eti asiumie shingo (safari yenyewe DAR-KIA) ... Tunavyowaona utasikia na swagaa zao ''about to take off, Home sweet home mara arrived safe in DAR'' yaani vurugu vurugu… Tusiopanda ndege tunabaki kusonya tu…..
😅😅😅😂
 
Sijui kwann maisha hayako fair mpaka level hii?
Maana haya mayebo akivaa msichana wa kichina au kikorea au kijapani anatokelezea kwel yan anakua kama kamdoli..ila sasa akivaa mwajuma wa yombo dovya au Salome wa boko magengeni yaam unaona kabisaa kero!![emoji23]

Hapo hua wana malizia na durag la mchongo
 
Mimi ni mmoja ya watu wakimya ila sipendi hiyo hali. Sababu ni hii: ikitokea kuna issue imetokea mtaani au kazini na ukihadithia watu wanapenda kusema..."kwa kuwa amekuona wewe mpole ndio maana akakuambia hivyo au akakufanyia hivyo"....ingekuwa mimi pangechimbika. Hivyo nikaanza kuona upole na ukimya kwa baadhi ya watu unatafsiriwa kwamba ni ubwege, uzubaifu, uoga, kutokuwa na uthubutu, ufala, uboya.

Hivyo pamoja na ukimya wangu sasa ninajitahidi kuchangamka na kujichanganya. Na pia, nimeanza kuwa na complications za maisha na kuwa mkorofi kiasi.
Inasemekana watu wakimya ni wazee wa risk taker.. Is it true?
 
Bora basi na hao wawili wapige kazi kwa moyo wote ila atakuwepo mmoja hakai akatulia kwenye dirisha lake, kila muda ni kunyanyuka na kuzunguka zunguka tu mule ndani.

Anabakia mmoja aliyeko serious....[emoji28][emoji28][emoji28]
Mkuu na wewe kumbe una uzoefu nao..hahaha miyeyusho sana
 
Back
Top Bottom