Vishu Mtata
JF-Expert Member
- Dec 15, 2019
- 15,954
- 35,415
😀😀 Nchi nzima na wilaya zake.Nchi nzima Mkuu nimetembea.
Hii kamba hii.
Kikubwa uzi ushapandishwa tayari.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😀😀 Nchi nzima na wilaya zake.Nchi nzima Mkuu nimetembea.
😀😀 Nchi nzima na wilaya zake.
Hii kamba hii.
Kikubwa uzi ushapandishwa tayari.
Unaiongeleaje wilaya ya ileje mkuu!?Nchi hii ni kubwa kama haupo interested kwa ishu za kutembea.
Wilaya zote nimezivuruga Mkuu. Japo zipo ambazo sijakaa hata kwa wiki lakini walau siku mbili tatu nimetembea.
Kama ningekuwa na pesa nafikiri ningezunguka kila nchi hapa duniani, hiyo ndio starehe kwangu, nikitumia usafiri wa ndege, Treni, boat, na magari huwa najisikia raha mno
Maskini hana cha kupoteza ,ndo sababu kila siku ana furahaInaonekana wilaya maskini ndo zinaongoza kwa furaha
Hiyo ya 7 si kweli, mbona Mama Diamond anawaletea nuksi waume zake? Akiachana nao ndiyo wanakuwa na furaha zaidi.Herehoa Wakuu!
Baada ya kusoma orodha ya mataifa ishirini yanayoongoza Kwa furaha Duniani. Nikaona nami nilete orodha ya wilaya za watu wenye furaha hapa TANZANIA.
Ni Kama ifuatavyo;
1. Wilaya ya Morogoro Mjini.
Kama ulikuwa haujui Morogoro ndio sehemu pekee ambapo watu wake wanaishi Kwa furaha, hata Mgeni ukifika Morogoro mjini utajikuta unafurahia maisha.
2. Wilaya ya Kisarawe.
Huku nilipatembelea mwaka 2018 nikabaki kushangaa. Watu wa kisarawe wengi wao wanaishi Kwa furaha. Hapana maendeleo makubwa lakini watu wake watakushangaza. Wanafuraha tuu mpaka unajikuta nawe unafuraha.
3. Wilaya ya Kyela
Huku nilipatembelea miaka ya 2012.
Wanyakyusa bhana! Watu wa eneo hili wanashikilia nafasi ya tatu Kwa furaha hapa Tanzania. Sio kama ni matajiri au wanamaisha mazuri Sana lakini ukiishi nao siku tatu tuu hata Kama ulikuwa unahuzuni utashangaa furaha imekufunika.
4. Wilaya ya Tanga mjini.
Hawa jamaa wanafurahisha Sana. Wao hawana stress za kijinga jinga, maisha hawayachukulii Sirius ati yawapasue kichwa. Tanga mjini Raha Sana. Watu wake hata awe hana Mia mfukoni lakini huwezi msikia akinuna.
5. Wilaya ya Mufindi
Hawa jamaa licha ya baridi kuwa Kali lakini wanaishi maisha ya furaha mno. Sio watu wa kujitukukuza, wakazi wa Mafinga na viunga vyake licha ya kuwa baadhi Yao ni masikini lakini bado wanaishi Kwa Furaha.
6. Wilaya ya Bagamoyo
Hawa watu wa Pwani bhana! Unaweza sema wanapesa au matajiri kutokana na maisha furaha waliyonayo. Wao hupenda mizaha, kucheka na kucheza bao.
7. Wilaya za kigoma karibu zote.
Hawa watu wakigoma licha ya umasikini wa Maeneo Yao lakini sijui furaha wanaitolea wapi.
Kuna wakati naona furaha ya kweli hutoka moyoni mwa mtu.
Ukioa Mkigoma nakuhakikishia lazima uwe na furaha.
8. Wilaya ya Mbeya Mjini.
Watu wa Mbeya Mjini pia ni miongoni mwa watu wanaoishi Kwa furaha. Sio rahisi umkute Mtu wa Mbeya amenuna hata Kama anasura ngumu lakini bado utaiona ikiwa na furaha.
9. Wilaya ya Mafia
Hawa jamaa unaweza ukadhani hawapo nchini. Wanaishi Kwa furaha licha ya kuwa mazingira Yao sio mazuri kivile.
10. Wilaya ya Kibaha
Ajabu ni kuwa zile wilaya zilizotoa watu wanaojitahidi kuhangaika na maisha ya Duniani na zenye maendeleo ndio hizohizo zinaongoza Kwa kutokuwa na Furaha.
Nawasilisha
Wow,,,,,,,mbinga[emoji7]Mbinga, Njombe
Tanga raha, Karibuni Tanga tunywe Al kasusu,gawaha na kashata,Supu ya pweza.
Ingizo hili limenifanya nisisome hii threadWilaya ya Morogoro Mjini.
Kama ulikuwa haujui Morogoro ndio sehemu pekee ambapo watu wake wanaishi Kwa furaha, hata Mgeni ukifika Morogoro mjini utajikuta unafurahia maisha.