Jambo rafiki!
Moja kwa moja kwenye mada. Hii ndiyo orodha yangu ya Maraisi bora kuanzia wa kwanza mpaka wa mwisho tangu tupate uhuru.
NB: Mimi ni mtoto wa 90's, kwahiyo wengine nimefanya utafiti kwa mapokeo ya mdomo kupitia wazee wangu.
1. Ali Hassan Mwinyi
Huyu kwangu ndiyo raisi bora tangu uhuru kwasababu;
a) Aliipokea nchi katika hali ngumu kuwahi kutokea kiuchumi, yaani idadi ya watu ilikuwa inaongezeka lakini uchumi haukui kwa kasi sambamba kuikidhi idadi, thamani ya shillingi ilkuwa bei ya juu (sawa na dola😆), kwahiyo watu wa nchi za nje hawakuitaka shillingi na ikawa ngumu kununua bidhaa kwao.
Kwahiyo Mwinyi kaipokea nchi hakuna hata bidhaa muhimu kama sabunu, mafuta, sukari, nguo n.k. Watu walikuwa wanaogea majani ya mipapai, watu nguo zina vilaka kuliko kitambaa, sukari ni anasa za matajiri, mafuta ni ya pamba na yenyewe ni mbinde kuyapata tena kwa foleni, sahani za udongo ni za matajiri n.k, uzalishaji wa kilimo ulikuwa mdogo sana kukidhi hata mahitaji ya ndani.
Aliipokea nchi kipindi imetoka kufirisiwa na vita vya Uganda ambapo deni la taifa lilikuwa zaidi ya dola billioni 3 kipindi hicho.
b) Kapokea nchi kipindi siasa za Ujamaa za Nyerere zilionekana zimeshafeli. Mambo ya vijiji vya ujamaa, Chama kimoja na umiliki wa serikali katika nyanja kuu za uzalishaji (kinyume cha ubinafsishaji), mabifu na IMF na WB.
Kwahiyo alipoingia alichofanya ni mageuzi ya uchumi mzima, kushusha thamani ya fedha, kufungulia bidhaa toka nje, kukubali masharti ya IMF na WB akafanikiwa kupewa mikopo, na muhula wa pili akaanza mchakato wa kuruhusu siasa za vyama vingi.
Watu sasa wakaanza kuona nuru ya maisha, wakaanza kuona sukari, mafuta, sahani, viatu, nguo, n.k, madukani. Hali kidogo ikabadilika na watu wakaanza kufanya biashara kwa ruksa wakaanza kuleta vitu kutoka nje na kupeleka vitu nje, hapa akawa amefungulia madirisha ya uchumi wa nchi.
Lakini kama binadamu tulivyo, na yeye hakuwa mkamilifu. Kipindi chake kwa upole wake Mzee wa Ruksa kulipelekea rushwa, ufisadi na wizi kutamalaki katika serikali yake vitu ambavyo havikuwepo kwenye serikali ya Nyerere.
2. Benjamin William Mkapa
Huyu jamaa aliingia kwa kiki za kuzuia rushwa iliyokuwa imetamalaki kwenye utawala wa Mwinyi na pia alikuwa ana vinasaba vya Unyerere kwahiyo akapita.
kupambana na rushwa Alifanikiwa kuziimarisha PCC (ya Warioba) PCB hii ambayo iliwafurahisha IMF na WB mpaka wakafuta madeni ya taifa, alifanikiwa kubinafsisha taasisi za serikali na kufungulia soko huru (free market), hivi vyote vilifanya uchumi wa nchi ukue.
Kwahyo miundombinu mingi alitengeneza ikiwemo mabarabara ya kuunganisha mikoa, mahospitali na mengineyo. Mkapa alianzisha utaratibu wa mabenki kutoa mikopo na sasa wafanyakazi wakaanza kukopa na kufanya biashara na hii iliongeza ubora wa maisha ya Mtanzania.
Kitu ambacho mzee mmoja nilimhoji anasema "Kipindi cha Nyerere hatukuona hata sahani madukani, kipindi cha Mwinyi tukaziona madukani ila wenye uwezo tu ndiyo walinunua, kipindi cha Mkapa tukanunua sahani" Lakini kama tulivyo binadamu Mkapa naye hakuwa mkamilifu, yeye pia alikuwa na shutma za wizi wa mali za umma na rushwa kwenye serikali yake.
3.Jakaya Mrisho Kikwete
Huyu jamaa aliendeleza alipoacha Mkapa lakini alifungua nchi zaidi na zaidi. Alilegeza masharti ya uwekezaji, aliiboresha sekta ya elimu kwa kuongeza udadi ya walimu, kujenga shule na madarasa, kuongeza mikopo vyuoni na idadi ya wanufaika wenye uhitaji, kuongeza ufaulu wa wanafunzi primary na sekondari n.k.
Kipindi chake maisha ya Mtanzania yakawa marahisi zaidi, ilikuwa rahisi kuanzisha biashara na kupata faida maana hela ilikuwepo kwenye mzunguko. Hapa ndiyo watu wengi walijenga na kuishi yale maisha ya keki ya nchi.
Mapungufu yake ni ufisadi na rushwa vilikithiri sana kipindi chake na yeye mwenyewe alipiga sana alipopata nafasi.
4. John Pombe Magufuli
Huyu mzee wa hapa kazi tu kachukua nchi ikiwa katika kinara cha rushwa, ufisadi, uvivu na sera mbovu. Alifanya kazi kubwa kuziba mianya ya wizi huku akihamasisha Watanzania kujituma na kuwajibika ili kupata kipato halali.
Alizuia wizi wa mali ya umma akapunguza matumizi ya serikali yasiyo ya lazima na hela akazipeleka kwenye miradi ya maendeleo kama Standard gauge, Stigglers, madaraja na mengineyo. Alifanikiwa kuirudisha nchi katika mstari wa uadilifu na hata maofisini wafanyakazi walikuwa wanafanya kweli kazi.
Kutokana na sera za rushwa za tawala za nyuma kuanzia Mwinyi, ilisababisha kuongezeka kwa pengo la madaraja ya tajri na masikini. Lakini kwa muda mfupi alioongoza JPM aliboresha huduma nyingi za kijamii ili kuwafikia mpaka watanzania masikini, na akasawazisha uwanja kwa ajili ya Mtanzania yeyote. Yale mambo ya 'unajua mimi ni nani?', kama sio kupungua yaliisha kabisa.
Mapungufu yake: Kubwa ni kuzuia vyama pinzani kwa kubaka uchaguzi wa 2020, kuzuia siasa za wapinzani, kuteka na kuua asiokubaliana nao, kuwaonea matajiri na kuwapora mali, kutotaka kukosolewa na kuleta udikteta.
5.Julius Kambarage Nyerere
Hatupendagi sana kumzungumzia huyu mzee tena kwa mabaya, lakini ngoja nianze na mazuri aliyofanya;
a)Kupigania Uhuru: Hili jambo ni kubwa na kwa watu wengi linatosha kumfutia makosa yote aliyofanya katika utawala wake.
b) Vijiji vya ujamaa: Hivi vijiji vilisaidia kusogeza huduma za kijamii kwa watanzania wengi, maana zamani nyumba zilikuwa zimetawanyika sana ikawa ngumu kupeleka shule, maji, hospitali kwa watu. Pia ilikuza miji, maana zile center zilikua zaidi na kuwa miji.
b)Kuondoa Ukabila: Kiukweli siasa za ujamaa zilisaidia kuondoa ukabila na kuleta umoja wa kitaifa, kuondoa uchifu, kusambaratisha watu wa kabila tofauti kupitia elimu, kazi n.k. Kifupi alikuwa na mbinu nyingi sana alizotumia kuondoa ukabila ambazo kutokana na muda sitazitaja.
c)Kujenga mashule: Nyerere alihakikisha kila kata ina shule ya msingi hivyo kuleta mwanga wa elimu kwa watanzania tena bure.
Mapungufu:
Kiukweli ujamaa ulifeli, kuegemea kilimo ili kukuza uchumi, kilimo chenyewe cha jembe la mkono ni ndoto isiyowezekana. Kiuchumi nchi ilidorora sana na umasikini ulitamalaki hasa baada ya vita vya Uganda. Kujitegemea hakuwezekani maana hapa duniani binadamu tunategemeana.
Azimio la Arusha iliharibu sana uchumi wa nchi hii. Kutaifisha sekta za uchumi iliharibu sana uchumi. Pia alikuwa muongeaji mzuri jukwaani ila siyo msimamizi mzuri kiutendaji. Mpaka anaiacha nchi ilikuwa katika shimo kubwa la umasikini kuliko alivyoikuta.
Muungano wa zanzibar alilazimisha ambapo inaonekana Karume hakuutaka sana. Kwahiyo walifanya kauhuni fulani ambako mpaka leo kanatugharimu.
*Samia Suluhu Hassan.
Huyu ndiyo kwanza ameingia kwahyo nimeshindwa kum-rank naona tumpe kwanza muda. Ila kwa mwenendo wake huu mpaka sasa sijaelewa mlengo wake ni upi, yaani ana siasa za bendera kwenda na upepo, hajaonesha msimamo wake binafsi na mipango yake anataka aifikishe nchi wapi kwa mikakati ipi.
Ila ni kama tunarudi zama za awamu ya nne, ila safari hii keki siyo ya wote, keki ni kwa wateule.
Pungufu kubwa aliloonesha ni ile kuonekana kuwa yupo kama kivuli kuna mtu nyuma yake.
Wewe mkuu orodha yako ni ipi?