Orodha yangu ya Marais bora kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho tokea tupate uhuru

Orodha isiyo na chembe ya unazi wala upendeleo!!
1. Nyerere!!
Huyu kafyeka msitu mnene sana wa ujinga maradhi na umaskini! Katufumbua macho!! Alikuwa na uthubutu wa kushangaza!! Aliiheshimisha sana Tanzania kwenye medani za kimataifa!! Alikuwa jasiri na aliwajali sana watu wake. Aliweka msingi imara sana wa anayekuja kujenga juu yake!! Kilichomwangusha ni matokeo ya nchi kufilisika kutokana na vita vya Kagera ikifuatiwa na ukame wa kutisha miaka ile ya themanini!!

2. Magufuli!!
Huyu alikuwa na uthubutu wa hali ya juu. Hakuanzisha kitu kigeni bali alikuta miradi mingi iliyopkuwa kwenye makaratasi lakini hakuna aliyekuwa na uthubutu wa kuitekeleza!
(a). Ujenzi wa makao makuu Dodoma!! Ilikuwepo kwenye makaratasi, ramani zilikuwepo! Maamuzi yalikuwepo!! Sheria ilikuwepo!! Lakini hakuna aliyekuwa na ubavu wa kufanya utekelezaji maana wote waliona HATUWEZI!!! Magufuli alifanya maamuzi ya kujenga makao makuu mara moja japo haikuwepo hata kwenye bajeti! Leo hii tunavyozungumza, makao makuu nyamehamia Dodoma!! Mradi ulikuwepo tangu enzi za Mwalimu!!
(b). ujenzi bwawa la mwalimu Nyerere la kufua umeme (Stigler's bGeorge). Mradi huu ulikuwepo tanmgfu enzi za mwalimu!! Michoro ilikuwepo, ramani ilikuwepo, lakini hakuna aliyekuwa na ubavu wa kuyaweka haya kwenye utekelezaji. Leo hii tunavyozungumza bado asilimia kadhaa tu mradi ukamilike. Mradi huu ulikuwa unapigwa vita sana maana utawakatia mirija mabeberu wanaoinyonya nchi yetu kupitia miradi yao wanayotuuzia umeme kupitia CAPACITY CHARGE!! Utumie usitumie malipo lazxima ulipe kutokana na uwezo wa mitambo kuzalisha umeme! Visingizio eti mradi utaharibu mazingira ni uongo mtupu!
(c). Reli standard gauge (trani ya umeme). Huu mradi ulikuwepo kwenye makaratasi tangu enzi za nyerere!! Uthubutu haukuwepo! Magufuli alithubutu na tunapoongea kitu kinachanja mbuga na makandarasi wako kazini!
(d). Madaraja ya juu, vivuko eg busisi, miradi ya barabara (lami) kote nchini, hususan njia nane kimara-kibaha. Hii miradi ilikuwepo toka enzi za Mkapa lakini ilikosa uthubutu!!
Na mengine mengi!!
Huyu bwana alikuwa na uthubutu wa hali ya juu. Amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi sana lakini amefufua miradi ambayo ni ya manufaa sana na hakuna aliyekuwa anadhani inawezekana! Kapambana na ufisadi wa wazi kwenye madini, na kusambaratisha sheria ya madini ikliyokuwa ya kifisadi na kutuwekea sheria m,pya ambayo ina manufaa kwa Taifa!! Mnyonge mnyongeni lakini hsaki yake apewe!!

3. Mkapa!!
Huyu Bwana alisimamia uchumi vizuri sana. Kipindi chake chote fedha haikushuka thamani kivile! Alirudisha nidhamu ya kazi na heshima ya watumishi wa umma! Kipindi chake unaweza kupanga mipango ikapangika!!

4. Kikwete!!
Huyu bwana ni mwungwana sana! Watumishi wa umma walifaidi sana kipindi chake!! Ajira zilikuwepo. Walimu wote walikuwa wanapata ajira!! Ni mwanademokrasia!! Aliruhusu kukosolewa na wengine walimwona ni dhaifu kumbe huo ni uungwana! Hadi kesho ni kipenzi cha watanzania! Anaweza kutembea kariakoo bila ullinzi na asipate madhara yoyote! Aligoma kutumiwa kidini na watu wa dini yake! na wengine walimwona kama kafiri kumbe siyo!

5. Samia Suluhu Hassan.
Japo amepata hiyo nafasi hivi karibuni, lakini namwona akiwa amempiku mzee ruksa kwa mbali! Ana huruma, na kete yake kubwa ni kwamba anaenda sambamba ni miradi yote mikubwa iliyoanza utekelezaji kipindi cha Magufuli na hajatetereka! Huo umekuwa ni mwiba mkubwa sana kwa maadui zake wa kisiasa ndani na nje ya chama chake!! Amecheza karata yake vizuri na mabeberu akapata mikopo ya korona lakini hakuiweka kwenye korona bali aliiweka kwenye elimu na afya kwa kigezo cha korona hiyo hiyo. Amejenga shule za msingi na sekondari nyin gi sana!! Amekarabati mashule mengi sana! Amejenga zahanati na nyingi sana! Mama yuko SMART!! Kawadanganyia tu mabeberu na barakoa na chanjo kidogo halafu wakaachia pesa zikaenda kwenye elimu na afya! Akiwa kwenye kamera anawekelea barakoa yake vizuri kudanganyia mabeberu! Anajua kula na vipofu!1

6. Mwinyi!!
Mzee Ruksa!! Tunamheshimu mzee wa watu na hakuwa na matatizo na watu. Kwake ni ruksa tu ili mradi usivunje sheria! Uhuru mkubwa!! Lakini kwa mambo ya kusimamia nchi, naweza kusema tulipigwa!1
Watoto wa 2000's mnashida sana unamuweka Mwinyi wa mwisho hakuna mtu aliyekuta nchi ikiwa juu ya mawe kama Mwinyi
 
Kwa sababu media zote zilifungwa midomo kama mtu ni mwema kwanin unafunga media midomo ndo kitu alichokua ananshangaza jiwe
Watu wanajitoa ufahamu TU, wote tulihamia jamhuli ya wasifiaji.
 
Nchi ilikua imefunikwa na wingu la hofu na mashaka, watu wanapotea anatokea Siro au mambosasa anasema ni watu wasiojulikana kirahis nchi ilipitia wakati mgumu sana

Kinachombeba Samia ni watu wana-aman ya Rohoni despite magumu wanayopitia
 
Kijana wa miaka ya 90 huwezi kujua ya 60 na ya 70 ! Sana sana utadanganywa tu !! Na huwezi kumlinganisha Rais wa miaka ya 60 wakati hakuna hata hiyo simu unayoitumia leo na Rais aliyepo dunia hii ya sasa !! Tunachotakiwa kukilinganisha ni falsafa zao !! Nani alikuwa na falsafa nzuri na alikuwa na uchungu na watu wake na nchi yake !! Na pia tunaangalia nani hakujilimbikizia Mali kupitia ofisi aliyokabidhiwa na wananchi !! Mwisho namalizia kwamba kila zama na kitabu chake !! Kwangu Mimi wa kwanza ni Nyerere !! Wengine wanafuata kwa wakati wao !!
Falsafa nzuri iliyotuzamisha kwenye shimo la umasikini?
 
Duh...!. Mkuu Afrocentric view , kwanza neheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo!, ila kiukweli watu mmeathiriwa vibaya sana na mfumo dume!, kuna watu mitazamo yao imeathiriwa na kitu kinachouitwa "mind suggestibilty" ambao kamwe bado hawakubali kuwa mwanamke anaweza kuwa rais wa nchi, hivyo hata wakimtazama Mama Samia akisimama, due to their mind suggestibility, wao macho yao hawamuoni Samia!, wanaona tuu kivuli na sauti ya samia ila nyuma yake wanaona kuna kiongozi mwanaume, hivyo kwao Samia wanamuona tuu kama geresha!.

Samia ndiye rais wa JMT, kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT ni absolute president, anachosema na anachofanya ni yeye Samia, hata kama ameshauriwa au ameandikiwa yeye ni kusoma tuu na kusema, ni yeye!.

Na kuna kitu wengi hawakijui kuhusu viongozi wapole na wa kimya kama Samia!, mimi nakijua lakini naomba nisikiseme maana sisi wengine kauli zetu huumba, nisije nikakisema hapa ndio nikawa nimekiumba watu wakaja kuishia kwenye vilio na kusaga meno kwa sababu kauli huumba!.

Hata naniliu unadhani ndio alikuwa vile?, kuna uwezekano ni kauli umba ndizo zilizomuumbia ule unaniliu!. Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Hivyo tutumie kauli njema kumuumbia mema Samia "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba?. Shuhudia.. tukiendelea kusema mnamuona kama kivuli, haijakaa sawa!.
P
Nimekupata mkuu, ila sikutaka kujikita huku...Cha muhimu tumpe muda. Muda ndio utasema
 
Watoto wa 2000's mnashida sana unamuweka Mwinyi wa mwisho hakuna mtu aliyekuta nchi ikiwa juu ya mawe kama Mwinyi
Kwa bahati mbaya kwako ni kwamba mimi si mtoto wa 2000!! Nilizaliwa kabla ya uhuru na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU. Ninazijua awamu zote nikiwa na akili yangu timamu!! Mwinyi hakufanya mikakati yoyote ya kuinua uchumi, bali aliruhusu maisha ya akili kichwani! Fedha ikapoteza thamani, vijana wakadharau ajira wakawa wanatembea na maburungutu ya fedha! Maisha hayakuwa halisi!
 
Falsafa nzuri iliyotuzamisha kwenye shimo la umasikini?
Inategemea na mitizamo ya watu tofauti tofauti , enzi zetu za miaka ya 60 mpaka miaka ya 70 tulikuwa tukiamini pesa sio msingi wa maendeleo bali kazi ndio msingi wa maendeleo !! Na kopimo cha umasikini ni kujilinganisha na matajiri !! Kwahiyo Enzi zile tofauti kati ya wenyenacho na wasionacho haki kuwa kikubwa kama ilivyo sasa !! Enzi zile ukiambiwa elimu bure ni bure kweli mpaka tickets za basi na treni tulikuwa tukipewa bure !! Watu walikuwa wakifurahia maisha sana tu kuliko ilivyo sasa ambapo ni wachache tu ndio wenye huo utajiri unaoufikiria. ! Wakati ule hatukuachana sana lakini leo mmh !!!
 
Binafsi ningetamani nchi hii ingekuwa na marais watatu tu toka uhuru mpaka sasa.
1. Nyerere ambae kazi yake kubwa ingeishia kwenye kujenga umoja wa kitaifa. Miaka 20 ingemtosha.

2. Then afate JPM ambae sasa angeijenga nchi kwa kuongeza au kulazimisha uwajibikaji wa wananchi na viongozi wa umma. Udikteta ndio suluhisho pekee kwa nchi hii. Miaka 25 ingemtosha.

3. Kisha kikwete. Huyu sasa angekuta nchi ishaneemeka kwa hiyo kila mtu sasa angelamba asali ya taifa kulingana na ukubwa wa ulimi wake. Maisha yale wakati wa jk hapa tungefurahia zaidi. Huyu nae tungempa miaka 20. Then tungerudi tena kutafuta mtu wa kariba ya JPM.

Yaani nchi ingekuwa na vipindi viwili. Muhula wa kufanya kazi kujenga nchi kisha muhula wa kula mema ya nchi
.
Mkuu unamuachaje Mkapa? Huwezi kuongelea maendeleo nchi hii bila Mkapa. Fanya utafiti wako taratibu utaelewa ninachosema.
 
samia.

Anakazi ya kumalizia miradi iliyoachwa na Magufuli na kutembea duniani.
Huyu nchi inajiendesha yenyewe..migao ya umeme na maji vinamvua nguo

Kikwete.

Alikuwa mwanasiasa na sio kiongozi.

Nchi ilikuwa na migao ya umeme, maji n.k.
Inaonesha kiasi gani bufuru tupu,unadhani shida ya umeme ni ya kutatua siku mbili kwa nchi fukara wa pesa Kama tz!?..maji ya Viktoria yaliyosambazwa tabora yamekula zaidi ya bilioni 700...inatoka wapi pesa Kama hiyo kutatua suala la maji nchi nzima!?..anamalizia miradi ya magufuli,magufuli aliacha pesa ya kumalizia miradi!?..si alikua anapora Hadi kwa wauza hardware!!...we unafikiri rais anazurula tu!!
 
Inategemea na mitizamo ya watu tofauti tofauti , enzi zetu za miaka ya 60 mpaka miaka ya 70 tulikuwa tukiamini pesa sio msingi wa maendeleo bali kazi ndio msingi wa maendeleo !! Na kopimo cha umasikini ni kujilinganisha na matajiri !! Kwahiyo Enzi zile tofauti kati ya wenyenacho na wasionacho haki kuwa kikubwa kama ilivyo sasa !! Enzi zile ukiambiwa elimu bure ni bure kweli mpaka tickets za basi na treni tulikuwa tukipewa bure !! Watu walikuwa wakifurahia maisha sana tu kuliko ilivyo sasa ambapo ni wachache tu ndio wenye huo utajiri unaoufikiria. ! Wakati ule hatukuachana sana lakini leo mmh !!!
Hatukuachana Sana kiuchumi sababu ya ujamaa..elimu Bure mpaka tiketi za mabasi,palikua na wasomi wangapi!!!?..tuliwekewa kiasi gani kwenye bakuli huko duniani!?
 
Kwa bahati mbaya kwako ni kwamba mimi si mtoto wa 2000!! Nilizaliwa kabla ya uhuru na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU. Ninazijua awamu zote nikiwa na akili yangu timamu!! Mwinyi hakufanya mikakati yoyote ya kuinua uchumi, bali aliruhusu maisha ya akili kichwani! Fedha ikapoteza thamani, vijana wakadharau ajira wakawa wanatembea na maburungutu ya fedha! Maisha hayakuwa halisi!
Mwinyi alifungua mipaka ya nchi pawe na biashara huria,mlipojijenga kibiashara akaanzisha tra kuvuna Kodi,unaposema vijana hawakujali ajira unaonesha mapungufu yako kwenye uwanda wa uchumi,hayo maburungutu ya pesa waligawiwa Bure na benki kuu!?..nyinyi watu wa TANU ndiyo mliokua na kauli wakulima na wafanyakazi,mkiona kilimo si kazi
 
Inategemea na mitizamo ya watu tofauti tofauti , enzi zetu za miaka ya 60 mpaka miaka ya 70 tulikuwa tukiamini pesa sio msingi wa maendeleo bali kazi ndio msingi wa maendeleo !! Na kopimo cha umasikini ni kujilinganisha na matajiri !! Kwahiyo Enzi zile tofauti kati ya wenyenacho na wasionacho haki kuwa kikubwa kama ilivyo sasa !! Enzi zile ukiambiwa elimu bure ni bure kweli mpaka tickets za basi na treni tulikuwa tukipewa bure !! Watu walikuwa wakifurahia maisha sana tu kuliko ilivyo sasa ambapo ni wachache tu ndio wenye huo utajiri unaoufikiria. ! Wakati ule hatukuachana sana lakini leo mmh !!!
Sawa hatukuachana...lakini tulifanana wote kukosa viatu, tulifanana wote kukosa sukari na mafuta. Inshort tulilingana katika umasikini.
Sasaivi ni kweli gep limeongezeka kati ya tajiri na masikini...Lakini atleast saivi masikini ana ndoto akifanya A, B, C atakuwa tajiri...kipindi hiko hizo ndoto hazikuwepo.
 
Kwa bahati mbaya kwako ni kwamba mimi si mtoto wa 2000!! Nilizaliwa kabla ya uhuru na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU. Ninazijua awamu zote nikiwa na akili yangu timamu!! Mwinyi hakufanya mikakati yoyote ya kuinua uchumi, bali aliruhusu maisha ya akili kichwani! Fedha ikapoteza thamani, vijana wakadharau ajira wakawa wanatembea na maburungutu ya fedha! Maisha hayakuwa halisi!
Hiyo fedha kipindi ina thamani, ilitusaidia nini?
 
Hatukuachana Sana kiuchumi sababu ya ujamaa..elimu Bure mpaka tiketi za mabasi,palikua na wasomi wangapi!!!?..tuliwekewa kiasi gani kwenye bakuli huko duniani!?
KIla zama na kitabu chake
Sawa hatukuachana...lakini tulifanana wote kukosa viatu, tulifanana wote kukosa sukari na mafuta. Inshort tulilingana katika umasikini.
Sasaivi ni kweli gep limeongezeka kati ya tajiri na masikini...Lakini atleast saivi masikini ana ndoto akifanya A, B, C atakuwa tajiri...kipindi hiko hizo ndoto hazikuwepo.
huenda ilibidi tuwe hivyo kwanza ili tuwe wamoja tusio baguana !! Na hiyo imetusaidia sana kupunguza ile dharau ambayo ingekuwepo kutokana na gap kubwa iliyopo kwa sasa !! Kidogo ile mentality ya kuvaa viatu rangi moja bado ipo vichwani mwa watu imerithishwa na wazee kwa watoto na wajukuu wao kwamba zamani tulikuwa tukiishi bila kudharauliana !!
 
Binafsi ningetamani nchi hii ingekuwa na marais watatu tu toka uhuru mpaka sasa.
1. Nyerere ambae kazi yake kubwa ingeishia kwenye kujenga umoja wa kitaifa. Miaka 20 ingemtosha.

2. Then afate JPM ambae sasa angeijenga nchi kwa kuongeza au kulazimisha uwajibikaji wa wananchi na viongozi wa umma. Udikteta ndio suluhisho pekee kwa nchi hii. Miaka 25 ingemtosha.

3. Kisha kikwete. Huyu sasa angekuta nchi ishaneemeka kwa hiyo kila mtu sasa angelamba asali ya taifa kulingana na ukubwa wa ulimi wake. Maisha yale wakati wa jk hapa tungefurahia zaidi. Huyu nae tungempa miaka 20. Then tungerudi tena kutafuta mtu wa kariba ya JPM.

Yaani nchi ingekuwa na vipindi viwili. Muhula wa kufanya kazi kujenga nchi kisha muhula wa kula mema ya nchi
Ondoa j weka nkapa
 
Inaonesha kiasi gani bufuru tupu,unadhani shida ya umeme ni ya kutatua siku mbili kwa nchi fukara wa pesa Kama tz!?..maji ya Viktoria yaliyosambazwa tabora yamekula zaidi ya bilioni 700...inatoka wapi pesa Kama hiyo kutatua suala la maji nchi nzima!?..anamalizia miradi ya magufuli,magufuli aliacha pesa ya kumalizia miradi!?..si alikua anapora Hadi kwa wauza hardware!!...we unafikiri rais anazurula tu!!
Umeandika kama umekatwa shingo.
 
Duh...!. Mkuu Afrocentric view , kwanza neheshimu mawazo yako hata kama sikubaliani nayo!, ila kiukweli watu mmeathiriwa vibaya sana na mfumo dume!, kuna watu mitazamo yao imeathiriwa na kitu kinachouitwa "mind suggestibilty" ambao kamwe bado hawakubali kuwa mwanamke anaweza kuwa rais wa nchi, hivyo hata wakimtazama Mama Samia akisimama, due to their mind suggestibility, wao macho yao hawamuoni Samia!, wanaona tuu kivuli na sauti ya samia ila nyuma yake wanaona kuna kiongozi mwanaume, hivyo kwao Samia wanamuona tuu kama geresha!.

Samia ndiye rais wa JMT, kwa mujibu wa katiba ya JMT, rais wa JMT ni absolute president, anachosema na anachofanya ni yeye Samia, hata kama ameshauriwa au ameandikiwa yeye ni kusoma tuu na kusema, ni yeye!.

Na kuna kitu wengi hawakijui kuhusu viongozi wapole na wa kimya kama Samia!, mimi nakijua lakini naomba nisikiseme maana sisi wengine kauli zetu huumba, nisije nikakisema hapa ndio nikawa nimekiumba watu wakaja kuishia kwenye vilio na kusaga meno kwa sababu kauli huumba!.

Hata naniliu unadhani ndio alikuwa vile?, kuna uwezekano ni kauli umba ndizo zilizomuumbia ule unaniliu!. Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni kosa la nani kati yake na aliyetoa kauli hii?

Hivyo tutumie kauli njema kumuumbia mema Samia "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba?. Shuhudia.. tukiendelea kusema mnamuona kama kivuli, haijakaa sawa!.
P
Mambo ya kauli huumba ni myth, kwa wanaomini Samia ni geresha wakiamini kuna 'nguvu' behind the curtains controlling wana haki ya kutoa maoni yao.
 
Back
Top Bottom