Orodha yangu ya Marais bora kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho tokea tupate uhuru

Paschall mayalla Kuna wakati unakua na akili sana lakini pia Kuna wakati unajawa na uccm hapo ndio nakutoaga kabisa kwenye watu wenye hekima
 
Vyama vipo; bahati mbaya hatuna chama chenye itikadi kwamba ujiunge nao kwa kuvutiwa na kile wanachokiamini.

Wapowapo tu nao wakisubiri zamu yao walambe asali.
Umenena!
 
Huyo wa mpaka Sasa tayari ameshafeli
 
Kauli Umba ! Karma itatenda very soon kwa wale wote wanaoendeleza udhalilishaji kwa wengine !! Tuseme Ameen !!
 
Mkubwa, ishu ya kuchelewa kuzaliwa haimaanishi utashindwa kuyajua au kuyafanyia tathmini yale ambayo hukuyaona. Kuna njia nyingi za kuyajua yale ambayo hatukuyashuhudia na ukafanya tathmini sahihi kabisa. By the way sijamtoa Nyerere kwenye hiyo list anabaki kuwa wa kwanza. lkn to me nchi inamuhitaji zaidi mtu atakayeendesha mambo yake kidikteta na kibabe kuliko kubemblezana, cha kuomba Mungu tu huyo mbabe awe na nia ya dhati ya kuletea watu wote maendeleo.

Demokrasia na mifumo imara inajengwa baada ya watu kunyooshwa na ubabe au adhabu kali bila ubaguzi kitu ambacho Afrika ikiwemo Tz hatuwezi kuvifata kwa sasa,
 
Interesting, kwahyo kwako mkapa na mwinyi hawajafanya mchango wowote?
Hakuna rais hana mchango kwenye nchi hii iwe positive au negative. Hii nchi imejaa wavivu, wezi, wazembe, matapeli, na watu wasio na maono ya mda mrefu, Inahitajika nguvu ya ziada kuwarudisha watu kwenye mstari, kama walivofanya wachina. Hata wazungu wenyewe kabla ya civilization ulaya, Walichapana na kunyongana sana mpaka walivoona sasa imetosha tuanze kuheshimu sheria na taratibu tulizojiwekea, Hapo ndipo mifumo ilipowekwa na kuheshimiwa.

Sisi huku ni kama vile tunataka kuanza kutembea kabla ya kutambaa. Ni mtizamo tuu lkn
 

samia.

Anakazi ya kumalizia miradi iliyoachwa na Magufuli na kutembea duniani.
Huyu nchi inajiendesha yenyewe..migao ya umeme na maji vinamvua nguo

Kikwete.

Alikuwa mwanasiasa na sio kiongozi.

Nchi ilikuwa na migao ya umeme, maji n.k.
 
Naunga mkono hoja !
 
Mimi kwa upande wangu anaanza Nyerere then anafata Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan maana amefanya maendeleo mengi tena ndani ya siku 594 za utawala wake maendeleo ambayo wengine wangefanya ata kwa miaka 3 au zaidi
 
Hapa nisehem ya kusema ukweli ,hata kama ni mchungu.

Hakuna kipindi ambacho rushwa ilitamaraki kama awamu ya Tano chini ya Rais wa 5.
 
Orodha isiyo na chembe ya unazi wala upendeleo!!
1. Nyerere!!
Huyu kafyeka msitu mnene sana wa ujinga maradhi na umaskini! Katufumbua macho!! Alikuwa na uthubutu wa kushangaza!! Aliiheshimisha sana Tanzania kwenye medani za kimataifa!! Alikuwa jasiri na aliwajali sana watu wake. Aliweka msingi imara sana wa anayekuja kujenga juu yake!! Kilichomwangusha ni matokeo ya nchi kufilisika kutokana na vita vya Kagera ikifuatiwa na ukame wa kutisha miaka ile ya themanini!!

2. Magufuli!!
Huyu alikuwa na uthubutu wa hali ya juu. Hakuanzisha kitu kigeni bali alikuta miradi mingi iliyopkuwa kwenye makaratasi lakini hakuna aliyekuwa na uthubutu wa kuitekeleza!
(a). Ujenzi wa makao makuu Dodoma!! Ilikuwepo kwenye makaratasi, ramani zilikuwepo! Maamuzi yalikuwepo!! Sheria ilikuwepo!! Lakini hakuna aliyekuwa na ubavu wa kufanya utekelezaji maana wote waliona HATUWEZI!!! Magufuli alifanya maamuzi ya kujenga makao makuu mara moja japo haikuwepo hata kwenye bajeti! Leo hii tunavyozungumza, makao makuu nyamehamia Dodoma!! Mradi ulikuwepo tangu enzi za Mwalimu!!
(b). ujenzi bwawa la mwalimu Nyerere la kufua umeme (Stigler's bGeorge). Mradi huu ulikuwepo tanmgfu enzi za mwalimu!! Michoro ilikuwepo, ramani ilikuwepo, lakini hakuna aliyekuwa na ubavu wa kuyaweka haya kwenye utekelezaji. Leo hii tunavyozungumza bado asilimia kadhaa tu mradi ukamilike. Mradi huu ulikuwa unapigwa vita sana maana utawakatia mirija mabeberu wanaoinyonya nchi yetu kupitia miradi yao wanayotuuzia umeme kupitia CAPACITY CHARGE!! Utumie usitumie malipo lazxima ulipe kutokana na uwezo wa mitambo kuzalisha umeme! Visingizio eti mradi utaharibu mazingira ni uongo mtupu!
(c). Reli standard gauge (trani ya umeme). Huu mradi ulikuwepo kwenye makaratasi tangu enzi za nyerere!! Uthubutu haukuwepo! Magufuli alithubutu na tunapoongea kitu kinachanja mbuga na makandarasi wako kazini!
(d). Madaraja ya juu, vivuko eg busisi, miradi ya barabara (lami) kote nchini, hususan njia nane kimara-kibaha. Hii miradi ilikuwepo toka enzi za Mkapa lakini ilikosa uthubutu!!
Na mengine mengi!!
Huyu bwana alikuwa na uthubutu wa hali ya juu. Amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi sana lakini amefufua miradi ambayo ni ya manufaa sana na hakuna aliyekuwa anadhani inawezekana! Kapambana na ufisadi wa wazi kwenye madini, na kusambaratisha sheria ya madini ikliyokuwa ya kifisadi na kutuwekea sheria m,pya ambayo ina manufaa kwa Taifa!! Mnyonge mnyongeni lakini hsaki yake apewe!!

3. Mkapa!!
Huyu Bwana alisimamia uchumi vizuri sana. Kipindi chake chote fedha haikushuka thamani kivile! Alirudisha nidhamu ya kazi na heshima ya watumishi wa umma! Kipindi chake unaweza kupanga mipango ikapangika!!

4. Kikwete!!
Huyu bwana ni mwungwana sana! Watumishi wa umma walifaidi sana kipindi chake!! Ajira zilikuwepo. Walimu wote walikuwa wanapata ajira!! Ni mwanademokrasia!! Aliruhusu kukosolewa na wengine walimwona ni dhaifu kumbe huo ni uungwana! Hadi kesho ni kipenzi cha watanzania! Anaweza kutembea kariakoo bila ullinzi na asipate madhara yoyote! Aligoma kutumiwa kidini na watu wa dini yake! na wengine walimwona kama kafiri kumbe siyo!

5. Samia Suluhu Hassan.
Japo amepata hiyo nafasi hivi karibuni, lakini namwona akiwa amempiku mzee ruksa kwa mbali! Ana huruma, na kete yake kubwa ni kwamba anaenda sambamba ni miradi yote mikubwa iliyoanza utekelezaji kipindi cha Magufuli na hajatetereka! Huo umekuwa ni mwiba mkubwa sana kwa maadui zake wa kisiasa ndani na nje ya chama chake!! Amecheza karata yake vizuri na mabeberu akapata mikopo ya korona lakini hakuiweka kwenye korona bali aliiweka kwenye elimu na afya kwa kigezo cha korona hiyo hiyo. Amejenga shule za msingi na sekondari nyin gi sana!! Amekarabati mashule mengi sana! Amejenga zahanati na nyingi sana! Mama yuko SMART!! Kawadanganyia tu mabeberu na barakoa na chanjo kidogo halafu wakaachia pesa zikaenda kwenye elimu na afya! Akiwa kwenye kamera anawekelea barakoa yake vizuri kudanganyia mabeberu! Anajua kula na vipofu!1

6. Mwinyi!!
Mzee Ruksa!! Tunamheshimu mzee wa watu na hakuwa na matatizo na watu. Kwake ni ruksa tu ili mradi usivunje sheria! Uhuru mkubwa!! Lakini kwa mambo ya kusimamia nchi, naweza kusema tulipigwa!1
 
Kweli Nyerer atabaki kua namba moja maana bila yeye tusingekua hapa leo
wa pili Rais Samia Suluhu ndani ya siku 594 kafanya maendeleo mengi sana
 
Mfano magufuli na manyoka wake wakina biswalo, makonda, sabai, mnyeti n.k walifanya ufisadi, ua watu na ufedhuli ambao haijawahi kufanywa tokea inchi ipate uhuru alafu Leo ndo rais wako Bora a serial killer anakua rais bora
 
Hii hata mimi naikubali,kweli hii naona iko sahihi sana.
 
Hapa nisehem ya kusema ukweli ,hata kama ni mchungu.

Hakuna kipindi ambacho rushwa ilitamaraki kama awamu ya Tano chini ya Rais wa 5.
Kwa sababu media zote zilifungwa midomo kama mtu ni mwema kwanin unafunga media midomo ndo kitu alichokua ananshangaza jiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…