Orodha yangu ya Marais bora kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho tokea tupate uhuru

Watoto wa 2000's mnashida sana unamuweka Mwinyi wa mwisho hakuna mtu aliyekuta nchi ikiwa juu ya mawe kama Mwinyi
 
Kwa sababu media zote zilifungwa midomo kama mtu ni mwema kwanin unafunga media midomo ndo kitu alichokua ananshangaza jiwe
Watu wanajitoa ufahamu TU, wote tulihamia jamhuli ya wasifiaji.
 
Watu wanajitoa ufahamu TU, wote tulihamia jamhuli ya wasifiaji.
Nchi ilikua imefunikwa na wingu la hofu na mashaka, watu wanapotea anatokea Siro au mambosasa anasema ni watu wasiojulikana kirahis nchi ilipitia wakati mgumu sana

Kinachombeba Samia ni watu wana-aman ya Rohoni despite magumu wanayopitia
 
Falsafa nzuri iliyotuzamisha kwenye shimo la umasikini?
 
Nimekupata mkuu, ila sikutaka kujikita huku...Cha muhimu tumpe muda. Muda ndio utasema
 
Watoto wa 2000's mnashida sana unamuweka Mwinyi wa mwisho hakuna mtu aliyekuta nchi ikiwa juu ya mawe kama Mwinyi
Kwa bahati mbaya kwako ni kwamba mimi si mtoto wa 2000!! Nilizaliwa kabla ya uhuru na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa chama cha TANU. Ninazijua awamu zote nikiwa na akili yangu timamu!! Mwinyi hakufanya mikakati yoyote ya kuinua uchumi, bali aliruhusu maisha ya akili kichwani! Fedha ikapoteza thamani, vijana wakadharau ajira wakawa wanatembea na maburungutu ya fedha! Maisha hayakuwa halisi!
 
Falsafa nzuri iliyotuzamisha kwenye shimo la umasikini?
Inategemea na mitizamo ya watu tofauti tofauti , enzi zetu za miaka ya 60 mpaka miaka ya 70 tulikuwa tukiamini pesa sio msingi wa maendeleo bali kazi ndio msingi wa maendeleo !! Na kopimo cha umasikini ni kujilinganisha na matajiri !! Kwahiyo Enzi zile tofauti kati ya wenyenacho na wasionacho haki kuwa kikubwa kama ilivyo sasa !! Enzi zile ukiambiwa elimu bure ni bure kweli mpaka tickets za basi na treni tulikuwa tukipewa bure !! Watu walikuwa wakifurahia maisha sana tu kuliko ilivyo sasa ambapo ni wachache tu ndio wenye huo utajiri unaoufikiria. ! Wakati ule hatukuachana sana lakini leo mmh !!!
 
.
Mkuu unamuachaje Mkapa? Huwezi kuongelea maendeleo nchi hii bila Mkapa. Fanya utafiti wako taratibu utaelewa ninachosema.
 
samia.

Anakazi ya kumalizia miradi iliyoachwa na Magufuli na kutembea duniani.
Huyu nchi inajiendesha yenyewe..migao ya umeme na maji vinamvua nguo

Kikwete.

Alikuwa mwanasiasa na sio kiongozi.

Nchi ilikuwa na migao ya umeme, maji n.k.
Inaonesha kiasi gani bufuru tupu,unadhani shida ya umeme ni ya kutatua siku mbili kwa nchi fukara wa pesa Kama tz!?..maji ya Viktoria yaliyosambazwa tabora yamekula zaidi ya bilioni 700...inatoka wapi pesa Kama hiyo kutatua suala la maji nchi nzima!?..anamalizia miradi ya magufuli,magufuli aliacha pesa ya kumalizia miradi!?..si alikua anapora Hadi kwa wauza hardware!!...we unafikiri rais anazurula tu!!
 
Hatukuachana Sana kiuchumi sababu ya ujamaa..elimu Bure mpaka tiketi za mabasi,palikua na wasomi wangapi!!!?..tuliwekewa kiasi gani kwenye bakuli huko duniani!?
 
Mwinyi alifungua mipaka ya nchi pawe na biashara huria,mlipojijenga kibiashara akaanzisha tra kuvuna Kodi,unaposema vijana hawakujali ajira unaonesha mapungufu yako kwenye uwanda wa uchumi,hayo maburungutu ya pesa waligawiwa Bure na benki kuu!?..nyinyi watu wa TANU ndiyo mliokua na kauli wakulima na wafanyakazi,mkiona kilimo si kazi
 
Sawa hatukuachana...lakini tulifanana wote kukosa viatu, tulifanana wote kukosa sukari na mafuta. Inshort tulilingana katika umasikini.
Sasaivi ni kweli gep limeongezeka kati ya tajiri na masikini...Lakini atleast saivi masikini ana ndoto akifanya A, B, C atakuwa tajiri...kipindi hiko hizo ndoto hazikuwepo.
 
Hiyo fedha kipindi ina thamani, ilitusaidia nini?
 
Hatukuachana Sana kiuchumi sababu ya ujamaa..elimu Bure mpaka tiketi za mabasi,palikua na wasomi wangapi!!!?..tuliwekewa kiasi gani kwenye bakuli huko duniani!?
KIla zama na kitabu chake
huenda ilibidi tuwe hivyo kwanza ili tuwe wamoja tusio baguana !! Na hiyo imetusaidia sana kupunguza ile dharau ambayo ingekuwepo kutokana na gap kubwa iliyopo kwa sasa !! Kidogo ile mentality ya kuvaa viatu rangi moja bado ipo vichwani mwa watu imerithishwa na wazee kwa watoto na wajukuu wao kwamba zamani tulikuwa tukiishi bila kudharauliana !!
 
Ondoa j weka nkapa
 
Umeandika kama umekatwa shingo.
 
Mambo ya kauli huumba ni myth, kwa wanaomini Samia ni geresha wakiamini kuna 'nguvu' behind the curtains controlling wana haki ya kutoa maoni yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…