ORYX Gas mnatujazia mchanganyiko wa Gas na Maji? Je, ni wizi au utapeli?

ORYX Gas mnatujazia mchanganyiko wa Gas na Maji? Je, ni wizi au utapeli?


Tumekuwa tunahimizwa kutumia Gas badala ya mkaa ili kulinda mazingira. Lakini nashindwa neno sahihi la kukiita sijui ni wizi au ni Utapeli Kwa kujaziwa sijui ni mchanganyiko wa Maji na gas katika mitungi ya gas.
Nimenunua mtungi wa ORIX gas wiki iliyopita na kutumia lakini chakushangaza badala ya gas Sasa inatosha unyevunyevu wa Maji Maji. Na mtungi Bado uko na uzito wa karibu nusu.
Sasa mnatumia fursa hii ya kutokuonekana Kwa kilichomo ndani ya mtungi kutujazia sijui Maji ili uzito uwe ni Sawa?
Hii inaonyesha kuwa ni MAKUSUDI hiki kitendo mnakifanya na waTanzania wengi tunaathirika.
Upatapo tatizo hilo beba mtungi upeleke ulipoununua wakupe mtungi mwingine kisha wao wamalizane wenyewe.
 
SHIDA NI HIYO BURNER YAKO MKUU..

Inaonekana imekula chumvi ya kutosha, haifanyi kazi ipasavyo, badala ya kuleta gas inaleta maji..

Kumbuka hiyo mitungi ina "LIQUIFIED GAS", hivyo kama burner ina fault itashindwa kuiconvert hiyo liguid gas into gas, mwisho wa siku ndiyo unapata matokeo kama unayoyapata hapo.

Kanunue burner ingine uone kama utaendelea kupata hilo tatizo.
Hapa kuna elimu nzuri sana
 
Badilisha burner hiyo mkuu. Ila ORYX nawaasa wawatembelee mawakala wao huku maduka madogo ya mangi unakuta mtungi unauzwa ukiwa na gesi pungufu. Brand yao inauliwa taratibu.

TBS waweke msisitizo / sheria kwa wabadilisha gesi ni lazima wawe na mizani!
 
Back
Top Bottom