GE2025 Oscar Nyerere (Mchekeshaji): Wanaotuchochea tufanye vurugu wapo nje ya nchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Msanii wa Vichekesho Oscar Nyerere amewahimiza Watanzania Kuilinda Amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu akisisitiza kupuuzwa kwa wanaharakati wanaochochea kuwepo kwa Vurugu.

Akizugumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo la Ikungi Magharibi Msanii huyo Amesema iwapo Machafuko yatatokea nchini athari kubwa ni kwa wanaoishi nchini na sio wanaharakati wanaochochea Vurugu wakiwa nje ya nchi

Chanzo: Wasafi FM
 
Nikizungumza kupitia mdomo na siyo speaker za makalio, ndugu zangu Watz nawasihi kumpuuza huyu mchekeshaji, niwazi kabisa anazo hisa flani kwenye taasisi ya wachumia tumbo, kwa nyinyi wengine `Kalagabaho' endeleeni kupaza sauti na kudahi haki hadi kieleweke. Asanteni sana...
 
Sasa nyie mlitaka wanaohimiza maandamano wawepo Tanzania ili muwaondoe kwenye uso wa dunia?
Ruhusuni freedom of speech na freedom ya kuandamana kwa amani muone jinsi watu watakavyojitokeza kupaza sauti.
Waliopo nje ya nchi wanatusaidia maana ni vigumu kuwakamata, so mimi sioni tatizo.
 
Msanii wa Vichekesho Oscar Nyerere amewahimiza Watanzania Kuilinda Amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu akisisitiza kupuuzwa kwa wanaharakati wanaochochea kuwepo kwa Vurugu.

Akizugumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo la Ikungi Magharibi Msanii huyo Amesema iwapo Machafuko yatatokea nchini athari kubwa ni kwa wanaoishi nchini na sio wanaharakati wanaochochea Vurugu wakiwa nje ya nchi

Chanzo: Wasafi FM
Kuiga sauti ya Nyerere hakumfanyi mtu kuwa na akili za Nyerere.

Aibu
 
Mlio karibu na huyo kidampa muulizeni haya maswali.

Je Ben Saanane, Azory Gwanda, Mzee Kibao, Leopold Lwajabe waliuwawa na watu wanaoishi nje ya Tanzania?

Je Tundu Lissu alipigwa risasi 32 akiwa London au Brussels.?

Je Sativa alitekwa na kukutwa mbugani nje ya nchi?

Je Soka, Mdude ,Dionise Kipanya, Jacob Mlay walipotea wakiwa nje ya nchi?

Je Padre Kitima alishambuliwa na vibaka akiwa nje ya nchi?
 
Sasa nyie mlitaka wanaohimiza maandamano wawepo Tanzania ili muwaondoe kwenye uso wa dunia?
Ruhusuni freedom of speach na freedom ya kuandamana kwa amani muone jinsi watu watakavyojitokeza kupaza sauti.
Waliopo nje ya nchi wanatusaidia maana ni vigumu kuwakamata, so mimi sioni tatizo.
Juzi kulikua na kesi ya lisu hamkuwa na taarifa? Mbona Yule kijana kashaambuliwa sahivi ndugu zake ndo wamebeba matatizo ya kumtibu nyie mnawafariji kwa maneno huenda hata Pole huja toa maisha hayako hivo Dada angu usijifikirie wewe tu fikiria na familia zetu sisi masikini tunabakije kama vijana wetu mnawatoa kafara nyie familia zenu ziko salama ushawahi kuwaza walau upeleke mwanao uliemzaa akapigane mahakamani
 
Vijana gani hap wanatolewa kafara? Vijana wanaenda wenyewe kwa matakwa yao, hakuna mzazi wake aliyemtuma
 
Dogo kiazi kweli wewe
Kaka yangu min me, samahani sana huwa sipendi kukukwaza, kuna mtu alikua hajui juzi ni kesi ya lisu, Yule kijana kapamban Sana kaishia kuumizwa, mbona hakusaidiwa mpaka yule mama kajitosa Key board warriors wako upside wa pili wa barabara wanallaaani vikali na kurekodi
 
Vijana gani hap wanatolewa kafara? Vijana wanaenda wenyewe kwa matakwa yao, hakuna mzazi wake aliyemtuma
Sasa mbona wewe ni kama unanilazimisha mimi nikuamini wewe eti ili niwe jasiri niandamane, nyie familia zenu ziko salama kwa nini usisubiri vijana tutapo amua kupambana sisi wenyewe nasi wee ufosi
 
Sasa nyie mlitaka wanaohimiza maandamano wawepo Tanzania ili muwaondoe kwenye uso wa dunia?
Ruhusuni freedom of speech na freedom ya kuandamana kwa amani muone jinsi watu watakavyojitokeza kupaza sauti.
Waliopo nje ya nchi wanatusaidia maana ni vigumu kuwakamata, so mimi sioni tatizo.
Kula pepsi bariiidi, umetisha
 
Juzi kulikua na kesi ya lisu hamkuwa na taarifa? Mbona Yule kijana kashaambuliwa sahivi ndugu zake ndo wamebeba matatizo ya kumtibu nyie mnawafariji kwa maneno huenda hata Pole huja toa maisha hayako hivo Dada angu usijifikirie wewe tu fikiria na familia zetu sisi masikini tunabakije kama vijana wetu mnawatoa kafara nyie familia zenu ziko salama ushawahi kuwaza walau upeleke mwanao uliemzaa akapigane mahakamani
Wewe dada hata kuandika tu hujui
 
Msanii wa Vichekesho Oscar Nyerere amewahimiza Watanzania Kuilinda Amani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu akisisitiza kupuuzwa kwa wanaharakati wanaochochea kuwepo kwa Vurugu.

Akizugumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo la Ikungi Magharibi Msanii huyo Amesema iwapo Machafuko yatatokea nchini athari kubwa ni kwa wanaoishi nchini na sio wanaharakati wanaochochea Vurugu wakiwa nje ya nchi

Chanzo: Wasafi FM
Sielewi kwanini watu wengi hadi viongozi wa dini wanahimiza AMANI na sio HAKI.

Hivi kumbe wanaolia kuonewa wakidai HAKI ni wanapuuzwa kiasi hiki.

Mimi ni mwanaCCM ila nashauri wanaodai haki wasikilizwe oktoba nitatiki lakini lazima tutambue kuwa kuna watu wanaona hawatendewi haki.

Na sio uongo kuna maeneo hawatendewi haki.Ni wakati wakuishi tukiwa wamoja tuimarishe upendo kati yetu.Maana hatupendani na chuki imetamalaki sana katika Taifa hili.

Wenye mamlaka wamefumbia macho kwasababu wanauhakika wa usalama wao.

Tuhamasishe HAKI zaidi ili amani ije yenyewe tusiilazimishe maana watoto/wajukuu zetu watakuja kututukana sana.
 
Back
Top Bottom