Oscar Oscar uache kuwaita wachungaji ni matapeli! Chambua soka, achana na wachungaji kabisa

Hakuna aliye wahi kuibiwa ......
Hakuna aliye shurutishwa ......
Wanatoa kwa hiari tena kwa moyo wa kupenda ....

Kwanza hakuna ibada isiyo kuwa na sadaka ...... kama ipo niambie hapa
Wewe uliyeguswa namna hiyo unashangaza hadi unaboa!

Oscar katoa tongo tongo za masikini wanaokandamizwa na "bhangi" za dini.

Ulisikia wapi kwenye kadamnasi watu wanalazimishwa kutoa?

Watu wanatoa kutokana na motivation inayokuwa imetolewa eneo husika na siyo kulazimishwa lakini kiuhalisia ni wizi mtupu huo!

Kwa hiyo anapowafungua akili zao usimlaumu kwa sababu hawalazimishi kumkubalia anachokisema, kama ilivyo kwako wewe mhamasishaji wa kutoa sadaka ambavyo hulazimishi watu kutoa.
 
Unajua watu wengi ni wajinga sana hamuelewi maana ya ibada mnavyoenda kutambika au Kwa mganga huwa mnabeba mawe? Hakuna shuruti kwenye ibada ukiona mtu anatoa sadaka jua kuna kitu kimetokea kwenye maisha yake kaamua kushukuru,
Wewe hauelewi lolote kuhusu hizi sadaka kandamizi.

Unadhani watu wote wanaotoa sadaka kwamba kuna miujiza wameipata na sasa wanashukuru!

Mbona nyie M/Mungu mnamuweka katika nafasi ya binadamu ya kupokea ili atoe?
 
Dini imekuwa taasisi ya kukusanya mapato kama tra..najiulza hv hapo zamani ilikuaje?
 
Ushahidi unao,peleka mahakamani.
Upumbavu mwingine huu umeuandika hapa, ushahidi unapelekwa police baada ya kufungua docket au kwa detective anayeshikilia docket, matatizo ya kuishi in a pithole country
Unajua mwamposa alianzaje huduma?unajua hadi alitengana na mkewe kisa umasikini na ubize kwenye huduma,leo huduma imefanikiwa wapuuzi kama wewe mnaanza kumuita tapeli,wakati anaanza huduma mlikua wapi kumuita tapeli?wapuuzi ninyi.
Mwaposa ni mwizi aliye ona gap ya upumbavu wa watanzania na kutake advantage, ndio maana kwa president kagame upuuzi huu haupo, nchi hii ipo kama public toilet
 
Ww utakuwa umejiunga Jana humu jf, watoa sadaka wapo humu na Kuna nyuzi nyingi tu za kulalamikia huo utitir wa sadaka makanisani

Wanaolalamika sadaka ni kwamba sadaka wanatoa kimwili na sio kiroho ,shida ya watu wanaona ibada ni utaratibu kama wa kwenda shule but hawamtafuti kumjua Mungu ndio maana hata maana ya sadaka wahajui na wanatoa sadaka kimwili na siyo kiroho but Walio rohoni wanajua sana maana ya sadaka
 
Ndo kwa karne hii mnashauri watu watoe mpaka sadaka za kujimaliza yaani hadi nauri waishiwe waanze kuomba omba kwa Konda??
 
Ndo kwa karne hii mnashauri watu watoe mpaka sadaka za kujimaliza yaani hadi nauri waishiwe waanze kuomba omba kwa Konda??

Wewe unafikiri wajinga wale ,wewe ndio unaonekana mjinga Kwa kua hutambui nguvu ya sadaka
 
mfano mmi nikikuhamasisha kutoa na pia nikakufundisha kwanini unatoa sadaka maanayake ninakuibia siyo kwa mtazamo wako....... ngoja niseme ivi waganga wengi wakienyeji wana wapa watu masharti flani ukishundwa masharti labda ya kuleta machozi ya simba unampa pesa yeye atajua pakupatia na watu wana toa hadi zaidi wanayo toa kanisani ..... tukija upande wa pili watu wakogundishwa namna yakumtolea MUNGU kupitia watumishi wake mnasema tunawaibia .....


Ngoja niseme ivi katika maisha haya ili ufanikiwe lazma uwe na upande moja kati ya hizi ..... MUNGU /SHETANI .... na huko kote lazma utoe ndipo uvuke hatua nyingine kimapato ...... kama mtu akienda kanisani na hana sadaka hajashikiwa bunduki ili atoe just hiari
 
Angeanza na matapeli walioko Ikulu kwanza.
 
Huu Uzi unaonesha ni kwanamna gani Osca amegusa maslahi yako mwizi mkubwa wee, kenge kabisa! Wewe ni Mwizi og
 
Kama muumini umekalia benchi ni Lazima utoe, labda mchungaji na wanakwaya!

Waulize utoaji sadaka wa Kanisa RC, ni benchi kwa benchi mzee.

Hata hivyo Mungu hatoi thawabu kwa binadamu kwa masharti hadi amtolee sadaka bhana.
Hakuna sadaka yenye thamani kama ile inayotolewa kwa wahitaji kv: masikini, wazee na wajane.
Lakini kwenu ninyi watu wanatoa dhabihu kwa moyo safi lakini mnaibadilishia malengo ya matumizi yake kwa visingizio vyenu na kuzitumia kujitajirisha pamoja na maisha mengine ya anasa.

Na Mungu ninayemzungumzia mimi hapa ni yule Mungu kweli, yule Mungu wa miungu yote na ulimwengu akiwemo Shetani.

Mungu aliyeumba vitu vyote vyenye kuonekana na visivyoonekana.

Wazungu humwita "Lord", maana yake anajitosheleza bila ya kutegemea matoleo kutoka kwa binadamu aliyewafinyanga mwenyewe.

Binadamu tunabeba dhambi nzito sana kuendelea kudanganya watu kwa udhaifu wao wa kifikira kwamba ili mtu afanikiwe ni lazima atoe matoleo kwa M/Mungu.

Mnanemeka sana kwa hadaa zenu kwa watu wajinga, lakini siku ya hukumu tutakataana.
 
K
Tumia namba hizi za simu ,Jina litasoma Boniface mwamposa au Macha, au Malisa . Hiyo sadaka ya kiroho au michango ya WAROHO
 
Ndugu yangu Asante Kwa maono mazuri ,lakini ukumbuke kwamba mtu anapokuvua nguo ,usikubali kabisa akuvue mpaka utupu uonekane !
 
Mawazo Yako yanafanana na ya yuda iskarioti ,alipoona mwanamke kahaba ametoa sadaka ya mafuta safi ya Nido ,akaingiwa na roho ya kishetani kuhisi kwamba itakuwa hasara yesu akiyatumia ,hivyo akashauri wayauze na pesa wakaigawe kwa maskini ,sikiliza majibu ya yesu kwa yuda! Kwa hiyo hujazuiwa kwenda kuwatembelea maskini na kutoa kwa ajili Yao ! Hiyo haiingiliani na sadaka ya kanisani acha umbumbumbu!
 
K

Tumia namba hizi za simu ,Jina litasoma Boniface mwamposa au Macha, au Malisa . Hiyo sadaka ya kiroho au michango ya WAROHO
Ulitaka isome jina gani ? Roman Catholic au isome buguruni Islamic centre ! Na baada ya hapo inakwenda wapi si vatcan na bakwata ? Na Huko anaitumia nani ,ofisi kuu pope ,kadinari na maaskofu? Au kule mnautupa chooni ? Ibilisi na roho ya utumwa ndiyo inakusumbua kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…