YAH: UTEUZI WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR
Tafadhali husikeni na mada iliyotajwa hapo juu.
Ofisi ya Baraza la Mapinduzi inapenda kutoa taarifa kwa Vyombo vya Habari na Umma kwa ujumla kuwa, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua tena Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Uteuzi huu umeanza rasmi tarehe 18 Septemba, 2026.
Hali kadhalika, Mheshimiwa Makamu wa Kwanza wa Rais ataapishwa siku ya Jumanne, tarehe 22 Septemba, 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ikulu ya Zanzibar.
Wako katika Ujenzi wa Taifa,
Pia soma: ACT Wazalendo yateua Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar