PreGE2025 Othman Masoud Othman: Miaka 61 ya Muungano, Zanzibar inakandamizwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
View attachment 3316493
Wakati leo Tanzania inaadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema Zanzibar ilianza kupambana na changamoto za Muungano tangu yakiwa mambo 11 na hivi sasa yamefikia 41.​

Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema ipo haja ya kufanyika kwa mabadikiko mkubwa ya mfumo wa Muungano ili Nchi zote mbili za washirika zipate haki sawa.

Othman ameyasema hayo leo April 26 katika ukumbi wa Samael Chakechake Pemba alipokua akizungumza na maelfu ya vijana wa Chama hicho katika kongamano maalumu la maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.
Alisema uwepo wa Muungano huu kwa muda mrefu unaikandamiza Zanzibar licha ya kuwa na rasilimali zake nyingi inashindwa kupata maendeleo na kukuza uchumi kama Nchi huru.

Alisema pamoja na uwepo wa kasoro nyingi za Muungo na kulalamikiwa, watawala wanashindwa kujali na wamekua wakiongeza mambo mengine mapya kujinufaisha na familia zao.

"Tulianza kulalamimia mambo 11 ya Muungano hapo awali lakini sasa tunalalamikia mambo 41 bila wenzetu kujali lolote huku mambo yote hayo yakinufaisha upande wa pili wa Tanzania Bara" alisema.

Aidha Othman ambae pia ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amesema kwa nyakati tofauti viongozi mbali mbali wamekua wakifanya jitidaha kumaliza, changamoto hizo lakini hakuna mafanikio ambayo yanapatikana kwa sababu wenye nguvu ndio wenye maslahi.

"Zimeundwa zaidi ya kamati 10 kushughulikia kero za Muungano lakini zote zimeishia njiani na hakuna kilichotimia hadi leo na ndio maana tunasema wenzetu hawana ukweli" alisema.

Sambamba na hilo alisisitiza changamoto hizo zinaiathiri zaidi Zanzibar ikiwemo kukosa mamlaka ya kukopa nje ya Nchi fedha ambazo zingeweza kuendesha miradi na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Ismail Jussa amesema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umekua na vikwazo vingi,kwa muda mrefu ambavyo viongozi mbali mbali wamekua wakivisemea.

Alisema vikwazo hivyo ni pamoja na kukoseka Kwa usawa na Nchi zote mbili za washiriki ambazo kabla kuundwa kwa Muungano huo zilikua Nchi huru.

"Nyinyi vijana wakati tunaadhimisha miaka 61 hii ya Muungano ni lazima mufahamu vita hii haikuanza leo na nyinyi muna wajibu wa kuendeleza mpaka tutakapoleta heshima ya Zanzibar kuwa Nchi huru yenye haki na usawa katika Muungano huu.

Sambamba na hayo Jussa alisema watawala waliilazimisha Zanzibar kuingia kwenye Muungano bila ya wahusika kurusika.

Akitoa salam za vijana Makamu Mwenyekiti Ngome ya vijana Taifa wa Chama hicho Nassor Ahmed Marhoun alisema vijana wapo tayari kuendelea kupambana kwa njia za kidemokrasia.

Alisema njia pekee ya kuzifanya Zanzibar kupinga hatua zaidi za kimaendeleo ni lazima washirikiane kwa pamoja kuiondoa CCM madarakati katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia soma ~ Ismail Jussa Ladhu: Kuna haja ya kutazamwa upya mfumo wa Muungano ili uweze kuleta usawa
Mshukuru Watanganyika wamelala usingizi wa pono, muungano unawanufaisha nyinyi wazanzibari kuliko watanganyika, labda mseme hamridhiki na kiwango mnachoinyonya Tanganyika mnataka kingekuwa kikubwa zaidi.

Ajira mnachukua asilimia ishirini na moja jambo ambalo sio haki. Jiulize woajiriwa wa muungano wanaofanyia kazi zanzibar kama polisi wanafikia asilimia 21 ya polisi wote? Nje ya muungano mngeajiri hiyo asilimia 21 kwq ajili ya utumishi wa zanzibar tu?
 
View attachment 3316493
Wakati leo Tanzania inaadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema Zanzibar ilianza kupambana na changamoto za Muungano tangu yakiwa mambo 11 na hivi sasa yamefikia 41.​

Wakati Tanzania ikiadhimisha miaka 61 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amesema ipo haja ya kufanyika kwa mabadikiko mkubwa ya mfumo wa Muungano ili Nchi zote mbili za washirika zipate haki sawa.

Othman ameyasema hayo leo April 26 katika ukumbi wa Samael Chakechake Pemba alipokua akizungumza na maelfu ya vijana wa Chama hicho katika kongamano maalumu la maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.
Alisema uwepo wa Muungano huu kwa muda mrefu unaikandamiza Zanzibar licha ya kuwa na rasilimali zake nyingi inashindwa kupata maendeleo na kukuza uchumi kama Nchi huru.

Alisema pamoja na uwepo wa kasoro nyingi za Muungo na kulalamikiwa, watawala wanashindwa kujali na wamekua wakiongeza mambo mengine mapya kujinufaisha na familia zao.

"Tulianza kulalamimia mambo 11 ya Muungano hapo awali lakini sasa tunalalamikia mambo 41 bila wenzetu kujali lolote huku mambo yote hayo yakinufaisha upande wa pili wa Tanzania Bara" alisema.

Aidha Othman ambae pia ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amesema kwa nyakati tofauti viongozi mbali mbali wamekua wakifanya jitidaha kumaliza, changamoto hizo lakini hakuna mafanikio ambayo yanapatikana kwa sababu wenye nguvu ndio wenye maslahi.

"Zimeundwa zaidi ya kamati 10 kushughulikia kero za Muungano lakini zote zimeishia njiani na hakuna kilichotimia hadi leo na ndio maana tunasema wenzetu hawana ukweli" alisema.

Sambamba na hilo alisisitiza changamoto hizo zinaiathiri zaidi Zanzibar ikiwemo kukosa mamlaka ya kukopa nje ya Nchi fedha ambazo zingeweza kuendesha miradi na kukuza uchumi wa Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Ismail Jussa amesema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umekua na vikwazo vingi,kwa muda mrefu ambavyo viongozi mbali mbali wamekua wakivisemea.

Alisema vikwazo hivyo ni pamoja na kukoseka Kwa usawa na Nchi zote mbili za washiriki ambazo kabla kuundwa kwa Muungano huo zilikua Nchi huru.

"Nyinyi vijana wakati tunaadhimisha miaka 61 hii ya Muungano ni lazima mufahamu vita hii haikuanza leo na nyinyi muna wajibu wa kuendeleza mpaka tutakapoleta heshima ya Zanzibar kuwa Nchi huru yenye haki na usawa katika Muungano huu.

Sambamba na hayo Jussa alisema watawala waliilazimisha Zanzibar kuingia kwenye Muungano bila ya wahusika kurusika.

Akitoa salam za vijana Makamu Mwenyekiti Ngome ya vijana Taifa wa Chama hicho Nassor Ahmed Marhoun alisema vijana wapo tayari kuendelea kupambana kwa njia za kidemokrasia.

Alisema njia pekee ya kuzifanya Zanzibar kupinga hatua zaidi za kimaendeleo ni lazima washirikiane kwa pamoja kuiondoa CCM madarakati katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia soma ~ Ismail Jussa Ladhu: Kuna haja ya kutazamwa upya mfumo wa Muungano ili uweze kuleta usawa
Tanganyika tunafaidika nini na Muungano, maana kila raisi anaung'ang'ania
 
Haki sawa na ninyi wapumbavu, mnachota pesa zetu nyingi halafu mnalalamika. Mnakandamizwa kivipi? Mna serikali yenu bado mnachukua pesa zetu huku bara. Eti mnakandamizwa, mnasaidiwa kila kitu na hakuna mnaloliweza paka ninyi....kelele nyingi hamtaki kufanya kazi...kupiga domo tu.
Muungano ukivunjika ndiyo mwisho wa CCM, muungano ulipatikana kinajimu
 
Uchaguzi ukiisha wanapewa shavu wanatulia. 😁
ACT wanachekesha sio kidogo.
 
Kabisa bhana! Ndio maana mkakandamizwa kwa Kupewa Urais wa Tanzania.

Ikulu ni Mzigo- Nyerere
Kinacho nishangaza mimi kwa hotuba hizi, ni kuona hata hao viongozi hawataki tena muungano uvunjwe. Hii ni sura mpya kabisa kutoka kwa viongozi hawa.

Maana yake ni kwamba, wote wametambua sasa jinsi Zanzibar inavyo faidi kuwa kwenye muungano.

Hakuna anayetaka muungano uvunjwe. Wanachotaka sasa ni kurekebisha baadhi ya mambo ili Zanzibar inufaike zaidi na zaidi kwa hasara ya Tanganyika.
Hasara moja wapo kubwa sana ni kuletewa viongozi wabovu kama huyu Samia.
 
Muungano uvunjwe na watumishi wote wa kiserikali na taasisi mbali mbali walio wazenjibara warudi kwao
 
Kinacho nishangaza mimi kwa hotuba hizi, ni kuona hata hao viongozi hawataki tena muungano uvunjwe. Hii ni sura mpya kabisa kutoka kwa viongozi hawa.

Maana yake ni kwamba, wote wametambua sasa jinsi Zanzibar inavyo faidi kuwa kwenye muungano.

Hakuna anayetaka muungano uvunjwe. Wanachotaka sasa ni kurekebisha baadhi ya mambo ili Zanzibar inufaike zaidi na zaidi kwa hasara ya Tanganyika.
Hasara moja wapo kubwa sana ni kuletewa viongozi wabovu kama huyu Samia.
Kifo cha Maalim Seif ni pigo kubwa sana, unaambiwa kila kitu kizuri sasa hivi kinapelekwa Zanzibat
 
Zanzibar ndo inaikandamiza Tanzania bara, yani wana serikali yao ardhi yetu ni yao ila yao sio yetu, viongozi wao wanatutawala ila sisi hatutakiwi kupata uongozi kwao, lazima Raisi au makamu atokee kwao, na wao ni kasehem kadogo tu ka nchi
Ili muungano uwe wa kweli wasingekuwa na serikali yao
 
Mkuu siyo kama najiamini (umetumia neno msijiamini, sijui hata mimi na kina nani). Naelezea kutokana na uhalisia wa mambo. Tume ya uchaguzi ni ile ile, na sheria ni zile zile au niseme zimefanywa mbaya zaidi. Wanachotakiwa kufanya ACT ni kudai kwanza tume na sheria zibadilike. Kingia kwenye uchaguzi bila mabadiliko hakutakuwa na jipya.

VIjana munawachukulia poa sana CCM
 
Back
Top Bottom