PreGE2025 Othman Masoud Othman: Miaka 61 ya Muungano, Zanzibar inakandamizwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mshukuru Watanganyika wamelala usingizi wa pono, muungano unawanufaisha nyinyi wazanzibari kuliko watanganyika, labda mseme hamridhiki na kiwango mnachoinyonya Tanganyika mnataka kingekuwa kikubwa zaidi.

Ajira mnachukua asilimia ishirini na moja jambo ambalo sio haki. Jiulize woajiriwa wa muungano wanaofanyia kazi zanzibar kama polisi wanafikia asilimia 21 ya polisi wote? Nje ya muungano mngeajiri hiyo asilimia 21 kwq ajili ya utumishi wa zanzibar tu?
 
Tanganyika tunafaidika nini na Muungano, maana kila raisi anaung'ang'ania
 
Muungano ukivunjika ndiyo mwisho wa CCM, muungano ulipatikana kinajimu
 
Uchaguzi ukiisha wanapewa shavu wanatulia. 😁
ACT wanachekesha sio kidogo.
 
Kabisa bhana! Ndio maana mkakandamizwa kwa Kupewa Urais wa Tanzania.

Ikulu ni Mzigo- Nyerere
Kinacho nishangaza mimi kwa hotuba hizi, ni kuona hata hao viongozi hawataki tena muungano uvunjwe. Hii ni sura mpya kabisa kutoka kwa viongozi hawa.

Maana yake ni kwamba, wote wametambua sasa jinsi Zanzibar inavyo faidi kuwa kwenye muungano.

Hakuna anayetaka muungano uvunjwe. Wanachotaka sasa ni kurekebisha baadhi ya mambo ili Zanzibar inufaike zaidi na zaidi kwa hasara ya Tanganyika.
Hasara moja wapo kubwa sana ni kuletewa viongozi wabovu kama huyu Samia.
 
Muungano uvunjwe na watumishi wote wa kiserikali na taasisi mbali mbali walio wazenjibara warudi kwao
 
Kifo cha Maalim Seif ni pigo kubwa sana, unaambiwa kila kitu kizuri sasa hivi kinapelekwa Zanzibat
 
Zanzibar ndo inaikandamiza Tanzania bara, yani wana serikali yao ardhi yetu ni yao ila yao sio yetu, viongozi wao wanatutawala ila sisi hatutakiwi kupata uongozi kwao, lazima Raisi au makamu atokee kwao, na wao ni kasehem kadogo tu ka nchi
Ili muungano uwe wa kweli wasingekuwa na serikali yao
 

VIjana munawachukulia poa sana CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…