Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Wiki hii imenibidi nipande daladala baada ya gari langu kupata hitilafu ndogo. Sasa katika safari hizo za kila siku, kuna jambo moja limenivutia sana.
Karibu kila daladala niliyopanda, nilisikia kauli ileile:
"Oya abiria... sogea upande wa pili!"
Ni kauli ambayo imekuwa sehemu ya utamaduni wa daladala. Kila konda anaitumia kwa kujiamini sana, kiasi kwamba unaweza kudhani kuna sehemu maalumu inayoitwa "upande wa pili."
Lakini nilipoanza kutafakari, nikajiuliza...
Huo upande wa pili ni upi hasa?
Maana ukikaa dirishani unaambiwa sogea upande wa pili. Ukihamia katikati, bado unaambiwa sogea upande wa pili. Ukisimama karibu na mlango, bado kuna mwingine anaambiwa aende upande wa pili.
Mwishowe unajiuliza, hivi huu upande wa pili una mwisho kweli, au ni eneo la kufikirika?
😂
Kuna siku nilimuona mama mmoja akihama mara tatu ndani ya dakika mbili. Kila alipohama, konda alikuwa bado anarudia:
"Mama... sogea upande wa pili."
Mwisho mama akamjibu:
"Mwanangu, huo upande wa pili wenyewe uko wapi? Nionyeshe nifike mara moja."
Daladala nzima ikapasuka kwa kicheko.
Na ukifuatilia vizuri, mara nyingi hata konda mwenyewe haonyeshi huo upande anaouzungumzia. Yeye anasema tu kwa mazoea, huku lengo likiwa ni kutengeneza nafasi ya kubeba abiria wengine.
Hata ukiwa umejibana kama dagaa kwenye kopo, bado utasikia:
"Sogea upande wa pili!"
Sasa naomba mnisaidie jambo moja.
Kwenu wana JF wa kipato cha chini, ambao bado mnatumia daladala kila siku, mnaijua hiyo sehemu inayoitwa "upande wa pili"? Au ni siri ambayo makonda wameamua wasiituambie?
Karibuni kwa hoja, uzoefu na ushuhuda wenu. Labda leo tutafanikiwa kuugundua huo upande wa pili ambao Watanzania tumekuwa tukiutafuta kwa miaka mingi. 😂