Oya Mwanenu mapenzi yanataka Kunitoa Roho

Oya Mwanenu mapenzi yanataka Kunitoa Roho

Hypochondria.
Shida hata upewe shule vipi huelewi ... Wewe was kuachwa uchapike Hadi uelewe ndio tukushauri.
 
Vijana siku hizi munafeli Sana!!

Hivi munapata Wapi huo Muda wa kutongoza hao munaowaita mademu....

Huyo demu kama umemwelewa uliza price tag inasomaje kwa siku hiyo, Unayo chukua kapige ujichane na moyo wako ufurahi.....

Hakikisha umemalizana naye kabisa, usimkope wala kumpa siasa za kujenga mahusiano....

Endelea kumtumia pale unapohitaji huduma yake, Hao mademu wamevurugwa na kitu inaitwa kikoba Sijui muchezoo....


Hapo usikute Anadaiwa rejesho kwenye kikoba Au kwenye micro-finance fulani. Kijana hii ni miezi ya Vikoba kuvunjwa , Kurenew rent n.k,Hao mademu zenu wako race kinoma!

Usijipendekeze sahizi, we Maliza hamu zako muLIPE amsha.....


Pole..!
 
Hii kitu isikie Kwa mwenzio tu, Kuna Motivational Speakers watakuambia achana nae, wanawake wako Wengi
Utamshaurije mtu aliyepo katika hali kama hiyo zaidi ya kumwambia aachane na huyo kahaba ??

Mwanamke yupo katika mitandao ya kujiuza ,utamshauri mwanaume mwenzio aendelee kujibembeleza na kujikombakomba kwake?

Hili sio suala la motivation speaker brother, ni issue ya kukaza roho kuukubali ukweli na uhalisia kuwa huyo Malaya hamfai. Kwanza amshukuru Mungu kamuepusha na mabalaa ambayo angekumbana nayo siku za usoni.

Kwa kipato chake anao uwezo wa kutafuta mwanamke atakayemfaa zaidi kuliko huyo CHUDA
 
Daaah mkuu move on Wanawake wapuuzi sana aisee. Na uking'ang'ania utapigwa tukio moja Takatifu kabisa.

Mimi niliwahi mpenda Manzi ivo ivo nika show Love la Maana lakini Guess what?? Sikuambulia Chochote zaidi ya Neno "em naomba Tuachane"

kimoyo moyo Nikajisemea Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe[emoji2][emoji2], kiukweli nilimpenda sana yule Manzi.

Lakini baada ya kunambia ivo Moyo ulizima alafu ukawa Tena. Yaani ni kama nili reboot Compyuta After Then ikawaka tena But iyo situation mkuu sio Rahisi kabisa aisee kama huna Strong Heart unaweza kuzimia.

Basi mimi nilijibu "Oh Ni sawa tu" After apo nikaderete Kumbukumbu zote kwanzia namba, Picha, messages zotee yani hadi Recycle bin sikuacha ushahidi wowote. Then Guess what?? It works now nishamsahau kabisa na life linasonga mbele.
 
One man down, ana kipi cha ziada ambacho wengine hawana?

Hiyo familiya haikufai kuoa wanakuzidi uwezo.utateseka maisha yako yote.

Ukitaka heshima ya ndoa oa familiya unayoizidi uwezo.
Wanaume wa siku hizi mnapenda show off waone una dem fulani?

Maskini yeye ana gari bado umpe ka mshahara kako aiiiiiiiiiiiiiiiiiiii pole

Mimi ningekuwa mwanaume kamwe nisingeoa kwenye familiya inayonizidi uwezo.
 
Daaah wanangu, Mwenzenu niko Hoi hapa Nilipo! Sina Usingizi, wala Siwezi hata Kula. Nimekuwa Fara Kinyama Kisa Mapenzi.

Ngoja Niwape Hii stori kwa Ufupi.

Kuna Dem mmoja, nilikutana Naye Supermarket, (ilikuwa Mwezi wa tatu 2022) nilimpenda na kumfungukia Hisia zangu, akawa Amenipa Namba!! Tukaanza Kuwasiliana.

Kumbe Ile Supermarket ni yake (nina uhakika maana alifunguliwa na mzee wake). Me aikujali wala nini sababu nina Kipato changu, nimeajiliwa Mahari. Nalipwa Kama 2 Mil.

Kweli Mwanzo Mapenzi yalikuwa Matamau sana, Tulikuwa tunaonana mara kwa Mara, tunachat na kuongea san, na alikuwa hana Hiyana Game alinipa La kibabe sana. Wazee mapenzi yalinikolea Vibaya Mno!! Nikaona Nimepata Dem wa Maana.

Baada ya miezi miwili...!!!
Siku moja mwanangu mmoja Ofisini, akanidokeza Jambo ambalo lilinishitua sana. Mwana Aliniletea Simu yake ambayo alikuwa ndani ya Mtando wa malaya Unaitwa Tagged, akaniambia Mzee embu angalia demu wako ambavyo hajatulia.

Mwana alikuwa amechati naye, na Kumtongoza kabisa, na Dem alikuwa anaelekea Kukubari ila alitaka kwanza waonane na Mwamba lakini pia alimpa namba yake ya simu ambayo nayo hiyo ilikuwa ni ile ile ya Dem, nilipoicheki( Mwamba hakuqa ameweka Picha yake!)

Daaah!!! Iliniuma Sana, ikabidi nichukue screen shot na Kumtumia Dem!!
Dem alikana Balaa na Kusema Kuna watu wanamchezea na wanataka Kutuvuruga. Sikumwambia kama Alikuwa anachati na Rafiki yangu. Alinifata hadi ofisini kuomba radhi na Kunisih nisiamini maneno ya watu.

Niliamua Kupotezea Tu wakuu.. si wajua Uanaume ni kazi. Ile account ikawa Imefutwa kule faster. Baada ya Muda wa Mwezi kama mitatu Tena, jamaa mwingine aliniletea tukio kama lile la mwanzo, daaah!! Hapa nilichoka zaidi na ukizingatia Dem namuelewa kinoma aisee!!

Nilitaka niachane naye kimya kimya, nikimuona kama ni malaya asiyejielewa!! Lakini nilishindwa kabisa. .... niliamua tena kumuuliza kuhusu jambo hili, lakini na wakati huu alikataa pia na account ikafutwa.

Maisha yakaendelea, baada ya mwezi alipata Shida ya kama sh. 1 mil. , Akawa aneniomba, mimi nilimwambia kiukweli sitaweza kukupa hiyo pesa sababu ni nusu ya mshahara wangu mzima lakini pia umeiomba leo na unaitaka leo.... ila nilimwambia nitakupa nusu nusu..

Demu alikausha akasepa, ikawa nikimpigia mara nyingi hapokei na akipokea anaongea kwa mkato sana! .... lile jambo lilinisumbua kwa kama wiki hivi nikaamua kumchana live tuachane akawa amekubari.

Baada ya wiki mbili aliwafata washikaji na kuomba samahani kwa kile kilichotokea. Wana wakaja kuniambia na Vile nilikuwa nampenda nikamsamehe maisha yakaendelea...

Nikawa nimemeahidi ile pesa aloomba kwakuwa aliamua kuikopa (alinambia hivyo) basi mimi nitamrejeshea taratibu kwa kumpa laki tano tano kila mwezi kwa miezi miwili.

Basi, mwez wa kwanza mambo yalikuwa mengi nikawa nimempa laki 4 tu. Nikamwambia mwezi ujao nitampa 6 ilobaki ili akamalizie deni. Akakubari na kusema ameweka juu laki moja so imekuwa tano akalipa.

Mwezi ulopita Ofisini walifanya ubwege wa kuchelewesha mshahara, ile tarehe ua demu kumpa hela ikafika lakini sina pesa. Nilijaribu kumwambia hali halisi, lakini akawa haelewi, kila siku anaulizia pesa...

Mazee, ilikuwa tarehe za mwanzo wa mwezi huu, aliamua kwenda kufunga mzigo, ila kila siku lazima aulizie pesa, na mimi nilkuwa bado sijapata...
Demu alichukia na kunitumia sms kuwa anajiona kama mwenye mikosi kila akitaka msaada toka kwangu anafeli ( ikumbukwe aba Supermarket, na ana drive gari kali, mimi sina hata baiskeli).

Keshoye nilimtumia Voice note, kumueleza hali ilivyo, na vile nilitarajia yeye angenielewa na kunishika mkono katika kipindi hiko!!

Aisee, voice note ilizua balaa!! Ugomvi ukawa mkubwa, ikabidi nionbe radhi lakini wapi...

Tukachuniana kama wiki hivi hatuongei, nikaja kumtafuta ili mambo yaishe akanikataa, nakunambia sifai kuwa nae!!

Niliumia sana, lakini nikajipa tumaini la kusonga mbele!! Jana akaja rafiki ake katika Stori, akanambia Amemuona Zaidi ya week yule dem anazurula na mwamba Mmoja Hapa mjini japo wanakaa Sehemu za Maficho..

Kwa Kweli imeniuma sana, coz nilikuwa nampenda na nimejitolea sana Kwake, kuanzia muda wangu, hadi jasho langu!!!

Lakini mwisho wa siku kaamua Kunitenda Kibwege sana.... kila Nikijaribu kumfuta Akilini wanangu, naona Kama naelemewa, sijui nilimpendaje Kifara namna hii....

Nimekwama hapa chakula hakipiti, kazi haziendi na sitaki kumrudia. Sijui nifanye nini
Mazeee.

Narudia tena kwa mara ya 300 kwa faida yako na vijana wengine...

Kijana, at any time t, hakikisha una wanawake angalau WATATU wakali kwenye cycle yako ya uchakataji.

Hii tabia ya kuwa na mwanamke mmoja tu kama roho itakufanya uwe fala kwake! Utaanza kujikuta unampenda, unamuwaza mda wote, unampa hela nyingi, nk.. Mwisho mkija kuachana unajikuta kwenye maumivu makali.
 
Nyie ndo watu mlioanza kushika doh nyingi bila msoto. Wengi wenu mapenzi yanawavuruga sana.

Yani inakua kama huna shida ila unaanza kuzitafuta kwenye mahusiano, tena kwa lazima kabisa.

Hakuna kingine zaidi ya kufocus na malengo yako, pesa uliyokua unampa wekeza kwenye kitu kingine.
 
kama wewe ni mkristu sali sana.. kila mawazo ya kumrudia au kumuwaza yanapokuja sali sala ya baba yetu!
.
.
kuachana kwenye mapenzi kupo, una mshahara mzuri, ukitulia na kumpata mwanamke ambae anapaswa kuwa mke, mtafika mbali, acha kucheza na afya yako, najua unadhani utapata status flani kisa una mwanamke mzuri, wanaume hatupo hivyo, tafuta mwanamke anaejiheshim na kujitambua na naekuvutia, tuliza kichwa mwombe Mungu utampata,
.
.
kwa nyakati hizi potea kwenye mazingira yake, namba futa usiwe wa mitandaoni, baki na call na text za kawaida, fanya mazoezi, kula vizur, ukimaliza, anza kutembelea maeneo ambayo wanawake wazuri na wanaojiheshimu hupenda kwenda, Utampata!
.
.
ukimpata acha zinaa, kamtambulishe nyumbani mkae wote kama mke na mume, ujana una mengi, pole kwa yanayokusibu ila ni ya kawaida na tumeyapitia wengi, na tumevuka!
 
Jasho lako ulilompa ni ahadi ya 1m, ambayo umeshindwa ukampa laki 4 tena ya maneno.

Unaumia kwa sababu ya ujinga, huwezi mhudumia, wewe tafuta single Mama au Mama ntilie.

Huyo wewe waachie wanaume wenye uwezo, unalipwaje 2m mtu anakuomba 1m miezi 4 huwezi msaidia?
ubaya kashamtajia demu kiasi anacholipwa haha, akili ndo kitu alikosa anyway ajifunze
 
Back
Top Bottom