Oya shituka betting ni uteja

Umechukua uamuzi sahihi achana na akili zilizoathiriwa na majini ya kina Kanji ambao wanakukebehi. Shikilia hapo hapo Mkuu.

Mwenye ushuhuda wa mafanikio ya betting atuoneshe hapa.

Betting Ina filisi, Ina madhara, This is a fact. And a fact is opposed by another fact.
 
Pole sana kijana... Lakini nakupa hongera KWa kufanya maamuzi ya kishujaa... Vijana sikuhizi wamezibwa masikio na macho.. ukiwaambia acheni kubeti, hizo fedha wekeni akiba mkalime au kufungua biashara ama kujaribu fursa yoyote ile tofauti na kamali... Wanasema ooh!! Hizo kejeli acha Kazi wewe uvae uhusika wetu... 😂😂 SAsa najiulizaga kukusihi wewe uache kamali ili pesa zako ufanyie JAMBO la maana inahusikaje na mimi kuniambia kuacha Kazi? Ni ujiingaa!!!

SAsa naomba nikupe kisa kimoja... Kuna jamaa kwao wote wapambanaji... Kasoro yeye tu!! Ni mtu wa home.. ni mtu wa kulialia hovyo mara kusema KWa mama au baba, afu cha ajabu lina miaka 30 na zaidi.....

Kuna mwaka mama yake akastaafu Kazi. Akapokea mafao yake... Lijamaa kama kawaida yake... Likalia lia... Eti mama hinipendi..... Akaligea milioni 3. Baada ya siku 2 halina hata mia... Linaulizwa ulitaka pesa umefanya nini.. eti nimeenda kubeti nipate nyingi.. ila mkeka umechanikaaaa.... Huku linalia... Nikajisemea tu... Stupid kabisa
 
Nashukuru mkuu..... Kifupi hili Jambo limekuwa na madhara makubwa kw kizazi hiki kuliko faida zake na dhahiri vjana hatutaki kukubali hili ila binafsi nimeamua mwenyewe tu niseme nashukuru kw nasaha
 
NO RETREAT,NO SURRENDER....hakuna hustler anatupa taulo mapema mkuu,hapo ni kubadili mbinu tu maana shida yetu unaweka timu 20 na unategemea kula 20mil kwa 200tsh huon huo ni ujuha?au pesa ya ugali wew unabet ili upate ya wali?...BET KISTAARABU
Sawa mkuu
 
Mleta uzi ngoja nikurudishe mchezoni.
Kanuni ya kudumu ni 1 bet=small odd + high stake.
Fanya leo singida vs yanga: yanga to win and total goals more than 1. Odds 2.45 betpawa. Stake laki.

Hakika
 
Wengi wanadhan kubet ni bahat mtu ana tick tick tu anaishia ku chase loss na allucination.
bet kwa akiri nyingi, uchambuzi makini, kiasi unachoweza kupoteza usipasuke moyo, na kwa malengo.
Mf kudevelop roll over kwa bet ya kila siku, na ukaweka kias hutathubutu kuzidi.
Kuchase loss au kuwa na expectation kama vile Mungu mjombako ndo inawafilis wengi.
Binafs hela ya pombe, malaya/mpenzi, sadaka kwa akina mackenzie, kafara, kurushia watumbuizaji, bora nizibet kwa sabab betting ni uwekezaji sema ni high risk.
 
Miaka 10,?
Bila bila?

Jitafakari!

Nakumbuka bado nikiwa pale UDOM nilikuwa nmejiwekea utaratibu wa kutenga 5000/- kila nipokeapo boom.

Nikaweka 2000=228000/-
2000 ikayeyuka.

Ikapita km miezi mi4 bila kupata.

Semister iliyofuata nikaweka 1000/-=169000/-

Tukahitimu.

Nikapata temple huko hometown,
Take home ya kwanza 250000/-,
Nikaweka 500/-for 24 matches=6,224,000/-

Nikanunua plots mbili,zipo nimeaanza ujenzi kwenye plot mojawapo.

Kuliwa kupo ila zingatia mambo kadhaa;

1. Usitegemee ku bet.
2.Matumiziyasizidi kipato.
3. Tenga kiwango cha fedha kwa ajili ya ku bet na koma tu mara baada ya kuwa kimekwisha.
4. EPUKA ku bet LIVE MATCHES kwa 7bu unalazimika kukaa betting station muda wooooooote.
5. Weka mkeka wako,nenda kafanye shughuli zingine za kukuingizia kipato.
6.EPUKA ku bet ki shaabiki.
7. Hakikisha familia KAMWE haipitii magumu kisa wewe una bet.
 
Hivi hapo najaribu kuwaza inakuwaje ghafla anapata million 800. Hivi haya maneno yatakuwapo tena? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
C kwmba ndan ya muda cjawah kula nimemuotea kanji Mara nyingi tu lkn huwa nikipima huwa naona km napiga duara tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…