Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Uvunaji wa maji ya mvua husaidia sana kuondoa shida ya maji. Kwa paa kama hili ni rahisi kukusanya maji na kuyahifadhi katika kisima ulicho kiandaa.
Wakati wa ujenzi unapanga sehemu ya vyoo na mabafu yawe upande mmoja na septic tanks ziwe upande huo. Upande wa pili unandaa kusima cha maji safi ya mvua. Unaweka na pump kuyavuta juu unapoyahitaji.
Kisima kukubwa cha kukusanya litre 50,000 za maji kinaweza kujaa katika msimu wa masika. Inategemea pia na ukubwa wa nyumba.