Pablo Franco Kocha Mpya wa Simba SC

Pablo Franco Kocha Mpya wa Simba SC

Ana ujuzi kabambe ,anaweza kuwaingiza uwanjani wachezaji wawili tu uwanjani ,Manula golini halafu Kagere ndo forward na utopolo mnafungwa goli 5 safi
Na mkiponea kwenye penalty mnaanza kusema GSM anahonga timu pinzani.
 
Sasa Simba Tuachane na Matola, Tuachane na Hitimana Na Wapuuzi wengine kwenye lile Benchi, ili Kocha Aanze upyaaaaaaa, Aangalie wachezaji yeye ajifumze yeye na kuamua.

Ila siku zote Simba Huanzaa Na Wengine huiga.

Kumleta huyu kocha sio Kitoto. Unafahamu Soka La Ulaya Na Uarabuni linavyo Lipa?
 
Simba imemtangaza Pablo Franco (41) kuwa Kocha Mkuu mpya akichukua nafasi iliyoachwa na Didier Gomes Da Rosa

Kocha huyo alikuwa anainoa Al Quadsia ya Kuwait. Pia amewahi kuzinoa Fuenlabrada, Getafe na amewahi kuwa Kocha Msaidizi Real Madrid.

Swali Je Ana uzoefu upi wa Soka la Kiafrika?

CV yake inaonyesha hajawahi kufundisha barani Afrika. Changamoto za soka la kiafrika anazitambua.


Hapa naona Simba wamejipiga na kitu kizito kingine.

View attachment 2001189
Apewe Muda apewe ushirikiano, aachwe atumie taaluma yake mwisho tutaona mafanikio yake
 
Simba hawana mikakati yoyote ya kufanya makubwa katika soka la Afrika,kocha huyo wamemchukua awasaidie katika NBC primier league,kama wangekuwa na mikakati ya kufanikiwa klabu bingwa ya Afrika basi wasingewauza wachezaji wao Chama na Miqussone,tena wamewauza kwa mahasimu wao.
😂😂
 
Sawa Mkuu...Ila kwanini imekua ni big story?

Kukaaa Benchi la Madrid si jambo rahisi mkuu..Tena madrid ile[emoji1]

Nimeangalia hata pale Al-Qadsia timu inacheza ki-mfumo, Pira biriani tena Biryan Moto[emoji91], yaan sijui itakuaje wana UTO[emoji2]
Tunawapa muda

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
 
Hizi pumba hata kwa Sven mlizitoa
Walisema wanamtaka asie na jina wala CV kubwa aje kuvipatia vyote Simba SC, hii kamari ngoja tuone kama italipa.

Hivi unaweza kuwa na malengo ya kufika mbali kwenye mashindano ya nje na ndani halafu ukamchukua kocha asie na experience ya mashindano husika?

Wanasema wanamtaka asie na jina ili awe na kiu ya mafanikio, kwani mwenye jina ndio anaweza kukubali kuharibu CV yake kizembe kwa kutofikia malengo ya kazi yake?

Hapa naona bora wangetupa sababu nyingine ya kumchukua huyo kocha asiyefahamika, kama ni issue ya mshahara tujue, lakini tusidanganyane na sababu zao walizotoa kwa kumchukua huyo kocha, Simba SC kwa level waliyofiki sio timu ya kuwajaribu makocha, sioni maana ya kumuacha Gomes halafu unaenda kumchukua mwenye CV ndogo zaidi.

#madness.
 
hans pope apumzike kwa amani Ila aturudishie Simba yetu kwakweli alikua anaipenda nawasiwasi ameondoka nayo
 
Back
Top Bottom