Package ya kiongozi bora hapa tanzania ifanyiwe reforms. Awe anajua masuala ya kijamii,ngaz ya jamii yanavyotatuliwa.

Package ya kiongozi bora hapa tanzania ifanyiwe reforms. Awe anajua masuala ya kijamii,ngaz ya jamii yanavyotatuliwa.

NYOLODO

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2020
Posts
12,206
Reaction score
27,987
Wqkuu salama?

Ni imani yangu tuko vizuri kwa namna yake. Wale wanaokutana na magumu kama ilivyo utofaut kat yetu, niwatie moyo! Nawaombea mpate salama, afua na siha iliyo njema mbeleni.

Taifa linapitia mambo mengi sana yanayozua sitofahamu. Mfululizo wa maswali kulingana na matukio kadhaa yaliyowah kutokea, uadilifu wa viongozi na zoezi zima la upatikanaji wa viongozi, ubadhilifu na matumiz mabaya ya madaraka. Mahitaj ya kutaka kutukuzwa, kusifiwa kila wakati na KUOMBWA kutimiza wajibu kama viongozi! Bado hali ni tete, haijetengemaa!

Naiona haja, katika haya ya kwamba mfumo, vigezo na yanayoshabihiana na hayo katika upatikanaji wa viongozi upitiwe, urekebishwe au uondolewe. Kwan, ndio huo unotuletea balaa ngazi ya utekelezaji wa mambo ya kijamii, kiongozi asione kama "yale ni maisha yake, na wananchi waishi maisha yao". Hoja hii niliwh kuiskia kwa kiongozi mmoja ngaz ya ukoo wake hapo jijini dareslaam

Awali ya yote mfumo uweze kutoa kiongozi aliyee na uwelewa wa kina wa masuala ya kijamii, matabaka na kuvaaa uhusika wa jamii yake. Na dunia hii ya sasa package ya kiongozi bora iongezewe nyama. Uadilifu, uwajibikaji na uzalendo bado haiwez kuwa sayansi kamili kwani haviwez kupimika.

Kiongoz ni 'cold hearted', anaona kama yuko pale kwa shani ya mungu!. Rehema na baraka kama si muujiza wa bwana, hajali! Haheshimu wala haoni shida za wanachi wake kama za kwake. That is unfair

Kiongozi hajui ni nn kipaumbele kati ya kumotisha au kuokoa. Jiulize, ni vipaji vya vijana wangapi mitaani vinateketea kwa sabab ya "Outreach plan" ya kuvisogeza mbele kulipigania taifa?. Leo hii changamoto zoooote wizara ya michezo ambazo zimekwama kisa hela sio kipaumbele ila kuleta watu maarufu kwa hela nyingi kupiga nao picha bungeni ndio inafaa?. Wanasaidia nn kukua kwa vipaji vya watoto huko vijijin shinyanga? Tunduru? . Huoni kama huu mkakat wenyewe ni wa watu wachache?
Screenshot_20260517_192807_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom