Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
Hizi inaweza kuwa taarifa kubwa zaidi hapa Tanzania kwenye dirisha hili Kubwa la Usajili 2024.
Taarifa za uhakika kutoka kwenye chanzo changu zinadai Paccome Zouzoua amepata offer kubwa kutoka kwa Mabingwa wa Africa, Al Ahly.
Kumbuka Pacome Zouzoua Peodoh amebakisha Mwaka 1 kwenye Mkataba wake na Yanga Africa hivyo amewaambia ni bora Kumuuza sasa kuepusha hatari ya Kuondoka bure msimu ujao kwasababu hana mpango wa Kuongeza Mkataba mpya
Paccome anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji peke yake ambae amefunga Goli dhidi ya Al Ahly kwenye CAF champions league msimu uliopita.
Kiungo huyo ambae ni Raia wa Ivory coast Alifunga bao hilo Dakika ya 90+1 katika sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Kundi D uliochezwa Desemba 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar es salaam
Wananchi yapi yanaweza kuwa Maamuzi Mazuri hapa? Kumbakisha Paccome Zouzoua kwaajili ya CAF champions league msimu huu aondoke Bure msimu ujao? au Kuchukua Pesa Mapema na kufanya uwekezaji kwasababu dirisha la Usajili bado ni changa?