Tetesi: Pacome aomba kuondoka Yanga

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054

Hizi inaweza kuwa taarifa kubwa zaidi hapa Tanzania kwenye dirisha hili Kubwa la Usajili 2024.

Taarifa za uhakika kutoka kwenye chanzo changu zinadai Paccome Zouzoua amepata offer kubwa kutoka kwa Mabingwa wa Africa, Al Ahly.

Kumbuka Pacome Zouzoua Peodoh amebakisha Mwaka 1 kwenye Mkataba wake na Yanga Africa hivyo amewaambia ni bora Kumuuza sasa kuepusha hatari ya Kuondoka bure msimu ujao kwasababu hana mpango wa Kuongeza Mkataba mpya

Paccome anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji peke yake ambae amefunga Goli dhidi ya Al Ahly kwenye CAF champions league msimu uliopita.

Kiungo huyo ambae ni Raia wa Ivory coast Alifunga bao hilo Dakika ya 90+1 katika sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Kundi D uliochezwa Desemba 2 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,Dar es salaam

Wananchi yapi yanaweza kuwa Maamuzi Mazuri hapa? Kumbakisha Paccome Zouzoua kwaajili ya CAF champions league msimu huu aondoke Bure msimu ujao? au Kuchukua Pesa Mapema na kufanya uwekezaji kwasababu dirisha la Usajili bado ni changa?
 
Hii habari umei copy kwa mchambuzi kanjanja anayejiita Wilson pasipo na wewe kutumia akili ukaileta hapa. Pacome bado yupo sana Yanga na anaingia Tanzania hivi karibuni na ataongeza mkataba wa miaka miwili kusalia Yanga. Poleni mnaotamani Yanga ianze na upya project
 
Unaonekana Rohoni umeumia sana Pole Mkuu
 
Kwa hiyo miwili mingine tayari, jumla mitatu sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…